Said mgoha
New Member
- Jul 6, 2021
- 2
- 2
Katika maisha ya kila siku duniani kote kila haachi kupambana ili kuweza kufikia malengo yake na hatimaye kukamilisha ndoto zake kulingana na wakati alonao katika mazingira aliyopo. Mtu huyo anaweza kuwa anapambana kwa kufanya shughuli tofauti tofauti kulingana fursa inayopatikana katika mazingira yake ili mradi iwe ya halali na si ile iliyokatazwa kwa mujibu wa sheria husika.
Mfano mzuri nchini kwetu (nchini Tanzania) kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ibara 24(1) imeka wazi katika kifungu hicho kwamba, kila mtu ana haki ya kumiliki na kulindwa kwa mali yake. Katika ibara hiyo hiyo ibara ndogo ya pili (2) imepambanua vizuri kwamba, itakuwa si halali kwa mtu yeyote kuchukua mali ya mtu mwingine …. Bila mamlaka ya kisheria. Pamoja na hayo yote kuwekwa wazi katika katiba yetu kama sharia mama, lakini bado imekuwa haki hiyo ikivunjwa katika maeneo mbali mbali japo imelindwa katika sheria. Katika maeneo baadhi kumekuwa na uvunjifu wa sheria kwa kufanya matukio ya wizi wa mali za watu wengine. Kosa hilo la wizi linafanyika katika muda wote, iwe mchana ama usiku. Na ikitokea imefanyika kosa hilo la wizi itatakiwa kuthibitishwa kwa mujibu wa sheria ya ushahidi sura ya 6 kama ilivyofanyiwa marekebisho 2019, katika kifungu cha 119 na 3(2) (a). Na sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai inaipa mamlaka mahakama katika kifungu cha 213 (1) (c) kushughulika na makosa tajwa.
Ingawaje wahalifu hao katika kosa la wizi hufungwa huko magerezani iwe kwa miaka saba (7), akiwa ametenda kosa hilo kwa mara ya kwanza ama kumi na nne (14), kama akirudia kutenda kosa hilo la wizi tena, kwa mujibu kifungu cha 265 na 275 cha kanuni ya adhabu sura 16 kama ili fanyiwa marekebisho 2019 na kifungu cha 341(1) (b) cha mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 kama ilivyofanyiwa marekebisho 2019, ambacho kimetaka ifanyike hivyo.
Lakini imekuwa ni tofauti na vile ambavyo inatarajiwa. Kwamba baada ya mtu huyo kumaliza kifungo chake atakuwa ni mtu mwema katika jamii na mwenye kuheshimu mali za watu wengine kama sheria ilivyotaja. Kwa kitendo hicho kuendelea inakuwwa ni jambo ambalo linaathiri uchumi wa mtu mmoja mmoja na hata taifa kwa ujumla. Kwa kuwa anaeathiriwa na kitendo hicho cha wizi ni mfugaji, mkulima, mfanyabishara, fundi katika nyanja mbali mbali, mabenki na kadhalika.
Pamoja na hayo yote, lakini bado kumekuwa na changamoto kubwa katika kuweza kulipunguza tatizo la wizi kama si kuliondoa kabisa. Kwa maana pamoja na kuwepo kwa sheria husika lakini bado matukio ya wizi yamekuwa yakishamiri kwa wingi sana katika maeneo mbalimbali kwenye jamii zetu. Tena mbaya zaidi imekuwa ni kawaida sasa mtu ambaye alihukumiwa kwa kosa hilo hilo la wizi anapomaliza kifungo tu, haichukui muda mrefu kusikia ama kuona ameiba tena. Wakati lengo la kifungo kile lilikuwa ni kutaka kumbadilisha kuwa mtu mweneye tabia njema katika jamii yake anayoishi. Waweza jiuliza kwamba huenda kukawa kunashida katika sheria zetu husika ama mamlaka husika na kuna tatizo lakini bado unaweza usipate jibu juu ya sababu ambayo inawafanya watuhumiwa kuwa katika hali ile ile ya kufanya makosa ya wizi kila uchwao.
Lakini pia pamoja na hayo yote, hata katika jamii zetu tunazoishi kwa namna moja ama nyingine imekuwa ikichangia katika hali hiyo ya kutenda uhalifu kwa kuwatenga wakosaji ambao tayari walikwisha tumikia vifungo vyao huko katika magereza ama vifungo vya nje kulingana na uzito wa makosa yao kwa kufanya kazi za kijamii katika ofisi za umma na maeneo mengine kwa mujibu wa sheria. Katika kitabu kilichowahi kuandikwa na N.V. Paranjape, (2003), Criminology and Penology, 11th Edition, Central Law Publications, ukurasa wa 26. Ameandika kwa kufananisha na kanuni za kimahesabu, kuwa kosa jumlisha adhabu ni sawa na mtu mwema. Kwa maana hiyo mtu anapokuwa amefanya kosa na kuadhibiwa basi huwa anakuwa ametakaswa anapokamilisha kutumikia kifungo chake. Hivyo basi tu huyo anakuwa huru na mwenye kupaswa kushirikiana na watu wengine bila kutengwa kwa namna yoyote ile. Kwani mtu kuwa muhalifu huchukuliwa kama mgonjwa, hivyo hupaswa kutibiwa ili apone. Mfano mzuri anapofungwa ndiko hudhaniwa kama amepelekwa hospitali ya wagonjwa, uhalifu ndo ugonjwa wenyewe na endapo atafanikiwa kubadilika ndiko kupona kwa ugonjwa (kuwa na tabia inayokubalika na jamii (termed as a good citizen)).
Jambo lingine ni kule kuwa na mazoea na watu walopewa mamlaka ya kuwasimamia na kuwarekebisha wawapo magerezani ama kuzoea mazingira ya kule ndani, kwani inakuwa ni sehemu ambayo haifanyi kujutia makosa yake, hivyo hata akitoka nirahisi kufanya tukio tena bila kujali, kwani hajapata mabadiliko yoyote.
Lakini pia wengine huona kuwa gerezani ni sehemu salama zaidi kwake na urahisi wa maisha yake awapo ndani ya magereza kuliko kuwa uraiani, hivyo hufanya kosa makusudi arudi tena alikokuwa mwanzo kulingana na ugumu wa kimaisha anaoukuta baada tu ya kumaliza kifungo chake, iwe ni miaka 7 ama 14 au zaidi. Kwani hukutana na hali ambayo kila kitu kimepanda bei ni tofauti na alivyoacha kabla ya kuhukumiwa. Mfano nzuri ni sasa hivi kulingana na mabadiliko ya sheria ya kodi ama za kodi, vitu vingi vimepanda bei kitu ambacho wengi wanaporudi uraiani hukuta kila kitu kimebadilika.
Kuharibikiwa zaidi wawapo magerezani. Kwani kunawengine wamefanya makosa madogo zaidi lakini walifungwa kutumikia adhabu zao magerezani, hivyo wanapokuwa huko huaribikiwa zaidi kutokana na kuchanganywa na wale walofanya makosa makubwa zaidi yao, hali ambayo ikitokea wakapata mazoea ya kupiga hadithi za kwanini yupo tatizo hilo, na kujua kumbe mwenzie alifanya nini na alifanya namna gani, hiyo huona kama yeye kaonewa, hasa pale atakagundua kosa lake ni dogo zaidi ya yule mwingine, japo kwenye sheria hakuna kosa dogo. Mbaya zaidi ni pale atakapokuwa jifunza kufanya ulifu kwa ufanisi zaidi kwa wale ambao wazoefu zaidi yake, kwa kutumia silaha na awatazipata wapi, wakati yeye aliiba kuku ama pili pili za jirani alipokuwa anakata kachumbari nyumbani kwao Tandale.
Pendekezo kulingana na tatizo
Kutoa elimu katika jamii yao. Hii itaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kwani imekuwa ni shida katika jamii zetu kujua ama kuelewa kwamba mtu akihukumiwa kifungo iwe kwenda jela ama vinginevyo, mtu huyo akikamilisha kutumikia kifungo chake, mtu huyo anakuwa ni mwema (mathematical equation of crime that, guilt plus punishment is equal to innocent), hivyo hutoka na kurudi uraiani kwa mujibu wa sheria na jamii inapaswa kushirikiana nae kama watu wengine wanyoshirikiana nao. Na elimu hiyo yaweza tolewa kupitia vipindi katika televisheni na redio kama “IJUE SHERIA” na “KONA YA SHERIA” na TBC 1 na ITV, lakini kwa sasa ni wakati wa kuenda mbele zaidi kwa kuifikia jamii moja kwa moja kama vile kwa kufanya mikutano nao kila mwezi, kwani si wote ambao wanasikiliza redio, ama kuangalia televisheni ama kusoma magazeti na ukizingatia jamii zilizonyingi teknologia imewacha nyuma hali ya kuwa teknologia inaenda kasi. Pia ni pamoja programu mbali mbali zinaweza kusaidia kutowatenga watu walomaliza vifungo vyao.
Mahakama zinatakiwa kujikita zaidi adhabu zingine hasa kwa yale makosa madogo madogo ambayo yanaamuliwa hususani katika mahakama za mwanzo. Kwani kulingana na uzito wa kosa mahakama inaweza kumtaka mkosaji alipe faini ama kumfunga kifungo cha nje, lakini ni baada ya mahakama kujiridhisha kuwa mkosaji anastahili kupatiwa adhabu hiyo, hiyo yote ni ili kupunguza kuwafanywa wafungwa wengi kuwa sugu (habitual) kwa makosa yao ya kuiba kuku, viatu, pili pili, na vitu vingine katika mitaa yao. Kwani wakiwa sugu inakuwa ni hatari zaidi.
Kuweka utaratibu wa kutowachanganya na wale walofanya makosa makubwa zaidi katika jamii. Kwani sidhani kama itamjenga na kumfanya kuwa bora endapo utamchanganya na yule ambaye alivunja na kuiba, ama aliiba kwa kutumia silaha nzito nzito, kwa kuwachanganya nirahisi kuwa na genge lingine la wahalifu ambao wanajifunza kutenda makosa kutoka kwa wale wengine ambao wao walitenda makosa makubwa zaidi. Hivyo ni bora wakatenganishwa kulingana na uzito wa makosa yao na vifungo vyao.
Angalau wawewanalipwa kwa kushiriki katika miradi ya serikali mbali mbali ya kazi za ujenzi. Kwa kufanya hivyo inaweza kuwasaidia kwani akitoka pamoja na kupata mafunzo kule gerezani ataweza kujianzishia kazi yoyote kwa mtaji alokuja nao toka huko. Kwani ukiangalia zaidi wakati anatenda kosa la wizi huenda alifanya akiwa hana kitu, ametumikia kifungo anatoka hana kitu, ni rahisi kufanya tukio tena, mpaka hapo reformation theory inakuwa imefeli, ukizingatia hata hivyo imepitwa na wakati inahitaji marekebisho. Na ni pamoja na kuwapatia angalau hata asilimia kadhaa kila mwezi katika akaunti watakazofunguliwa wakiwa jela kama wanavyofanya China na maeneo mengine, ili akitoka tu itamrahisishia kuwa na mwanzo mzuri wa kimaisha na si kutenda uhalifu tena.
Uhitaji wa kuboresha nadharia ya urekebishaji (reformation theory). Tangu ilipogundulika kwamba nadharia hiyo imekuwa ikikumbwa na changamoto nyingi katika utekelezwaji wake inahitajika kuchukuwa hatu zaidi ili kuioboresha kwa kuchukua hatua madhubuti ili kuifanya ifanye kazi na kleta matokeo chanya na si kuwafanya wahalifu kuwa sugu.
Kuepuka mazingira ya urafiki na wafungwa yasio lazima, kwani hali ya kuwa nao karibu zaidi huwafanya waone kuwepo kwao jela hakuathiriwi kwa namna yoyote ile, kwa kuwa tu wanaurafiki na watu wa mamlaka inayowashikiria kitu ambacho kinaweza kuwafanya wasiwajibishe ipasavyo hadi kumaliza kutumikia vifungo vyao. Kitu ambacho kinaweza kuitafsiri kwamba kazi iliyofanyika ni sawa na sifuri kwa muda wote, hiyo yote inatokana na namna walivyoishi. Kitu ambayo kinakuwa hakiisaidi serikali katika kuwarekebisha watu wake vile ambavyo ingestahili kwa mujibu na taratibu za nchi.

Upvote
1