SHERIA NA MIFUMO

SHERIA NA MIFUMO

Joined
Jul 6, 2024
Posts
97
Reaction score
72
SHERIA NA TARATIBU ZA KIMFUMO HAZIANGALII MTU KWA KIGEZO CHA HALI YAKE
YA KIUCHUMI
AU KICHEO
TUKO SAWA


Nilisikika huko ndotoni nikiwa nakoroma kukemea maovu na uonevu wa kuwachukulia hatua Mafukara na Watumishi wa Umma huku baadhi ya watu wakilindwa kwenye Vyeo vyao kwa Rushwa zinazonuka uozo wa Dampo na Viongozi Wanafiki wenye kuvaa ngozi ya kondoo huku wakiwa Mbwa Mwitu alificha mikucha ya Unyama wake na hivyo kuonekana akiapa
Kuihifadhi
Kuilinda
Na kuitetea katiba na Sheria za nchi ambamo ndani ya sheria na Taratibu tumekatazwa Vitendo vya
Kubebana katika maovu
Kuchukuwa hatua kwa kuangalia Uswahiba
Upendeleo
Ubaguzi
Rushwa
Muhali nk
yote haya hayakubaliki kufanywa na watu wenye viapo vya utii na Uadilifu walioapa wakiwa wameshika vitabu vya Mwenyezi Mungu kuuaminisha Umma kuwa wao watatenda haki.
Nabii IPM
Wa Kanisa lililopo Mbezi Beach Mbuyuni
Nakumbuka Tarehe 07/12/2024
Alisema
Njooni muniuwe ila Mimi nawaambia Ukweli na (Wala) sitokubali kuto kusema Ukweli
Kwa sababu Mimi ni Mtumishi wa Mungu wa. kweli.
Lazima nizungumze Ukweli.
Mwisho wa kunukuu
Ni Mishetani pekee iliyovaa Miili Kama watu ndiyo hupenda Unafiki na kuutetea Unafiki ule hadharani kutokana na Utamu wa dhulma ya kuwadhulumu Waafrika
Wasiojielewa walioamua kuishi kwa kushangilia mipira na Mambo ya Kichawa yasiyokuwa na faida kwa maisha yao.
Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
Amekuwa akitoa kauli nyingi akitaka watu wafuate Sheria ila Hawa wasaidizi huku chini hawana adabu kwa kauli za Mheshimiwa Rais na hawana adabu kwa ibara 35(1) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 toleo 2005.
Na hii yote inatokana na watu kutokuwa na hofu ya Mwenyezi Mungu kiasi Cha kuwafanya watu hao wajionyeshe Kama wanamtii Mheshimiwa Rais kumbe Mheshimiwa Rais akitoa maelekezo wao hawayafuati
Sisi Kama Taifa ifike mahala Sasa ikitokea kiongozi kapelekewa Malalamiko halafu hakuyafanyia kazi kwa mujibu wa Viapo vyake Kiongozi huyo awajibishwe huku ndiko kutendeana haki kusikoleta Mtafauku wa kisheria .
Mitafaruku yote ya kisheria inasababishwa na baadhi ya Viongozi Wanafiki wanasema hadharani wasivyo vimaanisha huku wakiwa hawana hofu ya kuvunja viapo vyao kiasi kwamba hata Maelekezo ya Viongozi wa Kitaifa kwa Sasa hayana maana kabisa kwa Viongozi waovu waliojawa na ulevi wa vyeo wenye kinga imara zenye kuta zilizosilibwa na Upendo Mkuu wa Rushwa
Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi
Katibu Mkuu CCM Taifa
Aktongea na Wanahabari
Na Wanahabari
Nakumbuka Tarehe 12/ 11/2024
Alisema
Sheria hizi zimewekwa kwa ajili ya kuwasaidia watu.
( Sheria ) zimewekwa ( ili) kuisaidia nchi yetu kuwa nchi ya Maana Zaidi .
Mwisho wa kunukuu
Hayati Dkt John Pombe Joseph Magufuli
Akiwa Mgeni Rasmi katika hafla ya Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri, Miji Manispaa na Majiji kula kiapo Cha Maadili kutoka sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma
Nakumbuka Tarehe 12/07/2016
Alisema
Nataka ( Watumishi wa Umma) mkafanye Yale ( yote) tunayotakiwa ( Watumishi wote) kuyafanya.
Kaondoeni kero kwa wananchi wa maisha ya chini .
Wananchi wa maisha ya chini wanateswa.
Tuliahidi kutoa kero kwa wananchi .
Hatukuahidi kutengeneza kero kwa wananchi .
Mwisho wa kunukuu
Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
Siku ya Demokrasia Duniani
Nakumbuka Tarehe 15/09/2021
Alisema
Nchi yetu inaongozwa kwa mujibu wa sheria ambapo hakuna mtu aliye juu ya sheria .
Kila mtu ana haki sawa mbele ya sheria
Ukivunja sheria Basi utashughulikiwa Kama Sheria zinavyosema
Haichagui ni Nani
Yeyote yule.
Mwisho wa kunukuu
Wakili Onesmo Olengurumwa
Mratibu Kitaifa mtandao wa Watetezi wa haki za Binaadamu ( THRDC)
Siku ya haki za Binaadamu
Nakumbuka Tarehe 10/12/2024
Alisema
Wakati mwingine Rais anaweza akawa anawaza Mawazo mazuri .
Lakini watu wanao mzunguka ...
Mifumo yake iliyoko ...
(Ikawa) haiko Pamoja na Yeye.
Mwisho wa kunukuu
Mheshimiwa Kenan kihongosi
Akiwa katibu Mkuu Uvccm Taifa
Nakumbuka Tarehe 25/06/2021 Alisema
Mheshimiwa Rais alishasema ,
Rais hakosei
Twendeni tukakipiganie Chama Cha Mapinduzi
Mwisho wa kunukuu
Kitendo Cha Viongozi wenye dhamana ya kuwajibisha wanapokuwa hawatimizi uwajibishaji wanapaswa wao wao kuwajibishwa
Huku ndiko kutenda haki kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 toleo 2005 ibara 13(1)(4)(5)

Mheshimiwa Julius K Layzer
Mkuu wa Wilaya ya Karagwe
Akiongea kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera katika Uwepo wa Askofu Dkt Benson Kalikawe Bagonza
Nakumbuka Tarehe 10/12/2024
Alisema
Sisi huku Serikalini tunazo sheria nyingi saana
Lakini katika Imani zetu hizi hasa Imani za kikristo tunazo amri kumi za Mungu .
Na Mimi huwa nawaambia ( Watumishi) wenzangu ,
( Ya kwamba) Kama ( laiti) tungetimiza amri hizo kumi tu peke yake Taifa letu lingekuwa ni Mahala pa Bora na salama saana Duniani kuishi kwake vizuri.
Na msingi huu tunafundishwa katika misingi ya imani tangu mtoto anapozaliwa anafundishwa amri kumi za ( Mwenyezi) Mungu .
Na Hakuna mtu asiyekuwa
Mwisho wa kunukuu
Tusome katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 toleo 2005 ibara 34(4) na ibara 35(1) ibara 09 a,b,f na h.
Ilani ya CCM 2020 ibara 04 uk 01.
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Askofu wa Makanisa ya Moravian
Ex Mhadhili wa literature.
Akiwa katika Maadhimisho ya siku ya haki za Binaadamu
Nakumbuka Tarehe 10/12/2024
Alisema
Katika Biblia zile amri 10 za Mungu zimejaa Mambo ya Utetezi
Ni mtetezi wa haki za Binaadamu
Mwisho wa kunukuu
Dhulma imekuwa tamu kiasi Cha watu Sasa kuamuwa kulindana wazi wazi na kuteteana kwenye maovu.
Tusiposema Hali itakuwa mbaya zaidi.
Kwa kuzingatia katiba ya CCM 1977 toleo 2022 ibara 05(16)(17)(18)
Katiba ya Jamhur ya Muungano wa Tanzania 1977 toleo 2005 ibara 26(1)(2) na ibara 09a,b,f na h
Ilani ya CCM 2020 uk 01 ibara 04 uk 161-168 uk 08 ibara 10 na 11
Tunataka kuona
Zile hatua ambazo Mafukara na Watumishi wa Umma huwa wanachukuliwa dhidi yao ...
Kipimo kile kile tunataka kukiona kikitumika kwa Viongozi wote Wachafu wanaonuka uvundo wa Uvunjifu wa Mifumo ili kuitendea haki katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 toleo 2005 ibara 13(1)(4)(5).
Mkuu wa Wilaya ya Arusha
Akiongea na Madiwani
Nakumbuka tarehe 07/12/2024
Alisema
Mimi niwaambie ,
Hakuna mtu ( awaye yeyote) wa kujidai kwamba eti ana network...."
"Sijuwi ana Nini ..."
( Kwa jeuri tu ) anakanyaga sheria
Hakuna mtu wa Design hiyo katika nchi yetu hii.
Wote tunafanya kazi kwa mujibu wa sheria na Taratibu za nchi .
Ukiwa na vijisenti usidhani kwamba uko juu ya Nini !?!?
( Juu ya Sheria)
Never
Never
Never on this Earth
Mwisho wa kunukuu
Tusome Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 toleo 2005 ibara 34(4) ibara 35(1) ibara 26(1)(2) ibara 09a,b,f, na h ibara 12(1)(2) ibara 13(1)(4)(5) ibara 29(1)(2)
Nikashtuka katika Kongamano la Kiroho huko kwenye Ulimwengu wa Kiroho huko Ndotoni nikiwa kimya.



Kidumu Chama Cha Mapinduzi

Mathias Mugerwa Kahinga
 
Ndefu sana.

Nitasoma siku nyingine. Ila kwa vile umemamaliza na mambo ya CCM itakuwa pumba tu.
 
Back
Top Bottom