Sheria na Mikataba inayolinda ushoga ambayo Tanzania imeridhia

Sheria na Mikataba inayolinda ushoga ambayo Tanzania imeridhia

Kama ilivyo ushoga, hakuna haki ya moja kwa moja ya uzinzi kwenye sheria yoyote. Hakuna sheria inayosema moja kwa moja kwamba kuna haki ya kufanya ngono au haki ya kupiga punyeto.

Huwezi kwenda popote kudai haki ya ngono, au haki ya kufanya mapenzi na mchepuko, au haki ya kupiga punyeto, ISIPOKUWA unaweza kudai HAKI JUU YA UHURU WA MWILI WAKO na HAKI JUU YA FARAGHA YAKO.

Hivyo, hakuna mtu yeyote mwenye mamlaka ya kukuzuia kupiga punyeto, au kuingiliwa haja kubwa, au kusagana, au kunyonya sehemu za siri, au kufanya ngono — japokuwa ngono si haki iliyotajwa na sheria moja kwa moja, lakini kupitia msingi wa HAKI JUU YA UHURU WA MWILI WAKO na FARAGHA YAKO, ngono inajumuishwa ndani ya haki hizo.

Ndivyo ulivyo ushoga. Na ndivyo sheria za nchi zinavyosema, pamoja na maamuzi ya kimahakama, ikiwemo na sheria mbalimbali za kimataifa ambazo Tanzania imeziridhia kama ifuatavyo:

1. KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977 (kama ilivyofanyiwa marekebisho):

a) IBARA 12 (1): "Binadamu wote huzaliwa HURU, na wote ni sawa". (FAFANUZI: Hakuna mamlaka yoyote inayoruhusiwa kupora uhuru wa mwili wako na maamuzi juu ya unavyojamiiana na kuingiliana isipokuwa kama vitendo hivyo vinanyang'anya haki ya mtu mwingine).

b) IBARA YA 15 (1): "Kila mtu anayo haki ya kuwa huru na kuishi kama mtu huru". (FAFANUZI, Rejea IBARA YA 12 (1) ).

c) IBARA YA 12 (2): "Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake". (FAFANUZI: Hakuna mamlaka yoyote inayoruhusiwa kuwatweza watu utu wao, kuwadhalilisha, kuwapima vipimo vya haja kubwa bila idhini yao, kuwatesa na kuwaadhibu kwa msingi wa machaguo ya maisha yao, isipokuwa tu kama vitendo vyao vinanyang'anya haki ya mtu mwingine).

d) IBARA YA 13 (1) (2): "Watu wote ni sawa mbele ya sheria.... ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake". (FAFANUZI: Hakuna mamlaka yoyote inayoruhusiwa kuwazuia watu kufanya machaguo juu ya hisia za miili yao, au hisia zao za ngono, kuwadhibiti na kuwaelekeza namna ya kujamiiana au namna ya kuingiliana au namna ya kushiriki ngono, na wakati huo huo, ikiwapa uhuru watu wengine kwa matendo yale yale ya ngono).

e) IBARA YA 16 (1): "Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake, na unyumba wake". (FAFANUZI: Hakuna mamlaka yoyote inayoruhusiwa kuingilia faragha ya maisha binafsi ya mtu, wapenzi wake, ngono anayoshiriki, machaguo ya maisha yake na machaguo ya hisia zake, isipokuwa tu kama vitendo hivyo vinanyang'anya haki ya mtu mwingine).

f) IBARA YA 13 (6): "Kwa ajili ya kuhifadhi haki ya usawa wa binadamu, heshima ya mtu itatunzwa katika shughuli zote zinazohusu upelelezi na uendeshaji wa mambo ya jinai". (FAFANUZI: Ni marufuku kutweza utu wa mtu kwa kumuingizia vidole sehemu yake ya haja kubwa, kumpekua usiri wa maumbile yake au faragha ya mwili wake bila idhini yake) (PIA REJEA: Azimio la umoja wa mataifa kuhusu vipimo vya lazima vya haja kubwa kinyume na mkataba wa kuondosha aina zote za ukatili na zinazotweza utu wa binadamu).

2. TAMKO LA ULIMWENGU LA HAKI ZA BINADAMU LA MWAKA 1948 (UDHR):

a) IBARA YA 1: " Binadamu wote wamezaliwa huru na sawa kwa utu na kwa haki". (FAFANUZI: Ni marufuku kwa mamlaka yoyote kutweza utu wa mtu, kufanya ubaguzi, kuonea au kudhibiti watu kiholela na kwa maguvu isipokuwa tu kwa minajili ya kulinda haki za watu wengine).

b) IBARA YA 9: "Ni marufuku kukamata watu kiholela, kuwatia kizuizini au kuwafukuza". (FAFANUZI: Ni marufuku kukamata na kuwafunga watu jela kwa minajili ya mionekano yao, au nguo zao au maumbile yao).

c) IBARA YA 12: " Ni marufuku kuvamia faragha za watu kiholela". (FAFANUZI: Rejea IBARA YA 16 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania).

d) IBARA YA 18: "Kila mtu ana uhuru wa mawazo, utambuzi na uhuru wa dini". (FAFANUZI: Ni marufuku kwa mamlaka yotote kutunga sheria kwa kutumia msingi wa dini fulani, au msingi wa biblia au quran, au kuweka na kupachika vigezo vya kimaadili juu ya watu kwa msingi wa kidini).

3. MKATABA WA KIMATAIFA WA HAKI ZA KIRAIA NA KISIASA WA MWAKA 1966 (ICCPR):

a) IBARA YA 26 : "Watu wote ni sawa mbele ya sheria na wana haki ya kulindwa na sheria bila ubaguzi wowote". (FAFANUZI: Ni marufuku kwa mamlaka yoyote kuonea, kubagua au kudhibiti watu kiholela na kwa maguvu visivyo halali).

HITIMISHO: Hii ndiyo mikataba mikuu miwili ambayo Tanzania imeridhia kuilinda na kuiheshimu kimataifa. Zoezi lolote la kunyanyasa watu kwa msingi wa maumbile yao au hisia zao ni zoezi lililo kinyume na Katiba ya nchi ya Mwaka 1977, kinyume na Tamko la Haki za Binadamu la Mwaka 1948, na kinyume na Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa wa mwaka 1966.

Na Mikataba hii ndiyo ambayo Tanzania ilijiapiza kuilinda na kuiheshimu kupitia Tangazo Rasmi la Serikali la tarehe 04 November 2018.
Watumalizia MB katika ujinga
 
Hahahahaha! Hatari sana. Nyuzi hii ya Bichwa Komwe inanikumbusha kuna jamaa mmoja alikuwa akileta nyuzi za ushoga watu wanamuandama kwa matusi lakini yeye ka-relax.

Ukitaka kupambana na watu kama kina Bichwa Komwe hautakiwi kutumia hasira na matusi. Ni kumbana kwa hoja tu, vinginevyo utaishia kukasirika huku Bichwa Komwe ka-relax.

Sasa mimi mimi naomba unisaidia Bichwa Komwe maswali yafuatayo mana Watanzania wengi kwa sasa wamejikita katika kuwashambulia mashoga na wasagaji bila kujadili chanzo na njia za kuzuia ili mtu asiwe shoga.

1. Chanzo cha mtu kuwa shoga ni nini?

2. Je, mtu anaanza kuwa shoga tangu utotoni au anaweza kuwa shoga hata ukubwani?

3. Je, ushoga ni ulemavu?

4. Kwa mfano, mtu anafumaniwa halafu analatiwa, je, kuna uwezekano wa mtu huyu kuwa shoga?

5. Je, shoga mzoefu anaweza kuacha ushoga? Kama ndio, njia zipi zitamfanya aache?

6. Njia zipi zitumike ili kuzuia watu wasiwe mashoga?
Wewee ndio mwenye uelewa wa mamboo.
[emoji122][emoji122][emoji122]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kweli watu wamevurugwaaa wallah. Khaaaah
Kweli wamevurugwa lakini hata nyie kina dada mnachangia kwa kiasi kikubwa kuomba mizinga kila dakika mpaka mtu anaona isiwe taabu ajichue tu solo.
 
Mi nacheka mwenzenu huu Uzi mpaka rafiki yangu kapewa ban Tena.
 
Ndio maana unaposikiliza hotuba za rais pale anapozungumzia maadili ya jamii anakwepa kutaja moja kwa moja wimbi hili liloibuka ghafla kama upepo uvumao. Itakuwa anakwepa kuvunja katiba aliyoapa kuilinda na kutoingiza serikali katika kuvunja mikataba ya kimataifa juu ya haki za binadamu. Hii ngoma wengine wanatamka waziwazi kwa kuwa kauli zao hazichukuliwi kama ni kauli ya serikali. Ndio maana hii ngoma imesogezwa mbele ili upembuzi ufanyike kisha itinge bungeni kujadiliwa na marekebisho ya sheria yafanyike kuhusu mambo hayo ya mahusiano
Anaelewa sana ndio maana hataki kuingia mtegoni.

Anapigana vita za uvunguni.
 
HUJAONESHA namna gani ambavyo sheria mama inakinzana na ile sheria inayoeleza kosa la kuingiliwa kinyume na maumbile.

Kusema tu kwamba inakinzana bado sio hoja,hoja ni uelezee namna gani inakinzana,wewe bado mkuu hujatufafanulia.
Soma tena na tena mpaka uelewe.
 
Wrong citation and quotations by referring our constitution.
Even before our constitution it was different every thing you are doing under the sun please don't refer it else where just refer it from holy bible, even your reference i.e the constitution of the united republic of Tz many words quoted from the holy bible. It is just because you are cursed that's why you are hiding the constitution, turn to the right way you are messing towards that direction. Oooh offsprings of snake who bewitched you?.
Kingereza cha Ugoko kutoka kwa mtanganyika.
 
Jamaa ametetea hoja yake kwa kutoa ushahidi[emoji23] mnaopinga msimkaripie, nanyi toeni ushahidi....
Yeah, hata mimi nilitegemea watu humu wamjibu kwa hoja za kisheria badala ya kumtukana. Inawezekana unamtukana mtu kumbe yupo sahihi, na usichokipenda hakijaletwa na yeye, bali watunga sheria na serikali yako
 
Yeah, hata mimi nilitegemea watu humu wamjibu kwa hoja za kisheria badala ya kumtukana. Inawezekana unamtukana mtu kumbe yupo sahihi, na usichokipenda hakijaletwa na yeye, bali watunga sheria na serikali yako
Humu pamejaa mihemko ya mangumbaru, ndio maana watu wa serikali wanaojua mambo wako makini na swala hili.

Samia kaamua apigane vita za uvunguni, anarusha mishale kimya kimya huku anachungulia kwenye kitobo. Anajua akileta taharuki atabinywa mahali panapouma.

Manguli wa kimataifa kama MAHIGA walilijua vema hili swala ndio maana wakamruka Makonda futi mia saba.

Hawa VINYANGARIKA wa mitandaoni wamejaa MIHEMKO hawana DETAILS.
 
Zaidi ya 30% ya bajeti ya nchi inategemea nchi wahisani
Naam.

Zile LANDCRUISERS ZA MAWAZIRI unafikiri zinanunuliwa kwa TOZO ZA NYANYA??? THUBUTUUU! ile ni PESAA YA MABEBERU.

Unaijua VIEITEE WEWEE?? [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Katiba yetu ya sasa ina uzuri wake.
 
Mwanaume Unalegezaje Masharti Kirahisi
Uuache Mgongo Wako Wazi Uanze Kupindwa
Halafu Nawe Unapondika Tu
 
Back
Top Bottom