Sheria nyingi zilizoundwa na CCM zimelenga kutengeneza mazingira ya kufanyika uovu

Sheria nyingi zilizoundwa na CCM zimelenga kutengeneza mazingira ya kufanyika uovu

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,362
Reaction score
48,879
Taasisi yoyote inapotaka kufanya uovu wowote, kwanza hutengeneza mazingira ya kuwezesha uhalifu kuweza kufanikiwa.

Serikali ya CCM, muda mwingi imekuwa ikiandaa mazingira ya kisheria ya kufanya uovu dhidi ya umma:

1. Serikali ya CCM kwanza iliandaa na kupitisha sheria ya kinga ya viongozi. Sheria hii inawatengenezea mazingira ya viongozi wakuu kufanya uovu wowote wanaotaka bila hofu ya kushtakiwa wakiwa madarakani au wakiwa wametoka madarakani. Sheria inampa kinga ya kutoshtakiwa Rais wa JMT, Makamu wa Rais wa JMT, Waziri Mkuu, Spika wa Bunge na Jaji Mkuu. Tujiulize, kama wewe kiongozi ambaye dhamira yako ni kutekeleza majukumu yako kwa kufuata sheria, Katiba na Kanuni, kwa nini uanze kujihami kwa kujiwekea uwigo wa kuzuia kushtakiwa? Sheria hii imetengeneza mazingira ya viongozi wakuu kuwa watu waovu dhidi ya umma. Karibia mataifa yote Duniani, Rais anaweza kushtakiwa akifanya makosa, lakini Tanzania huwezi kumshtaki Rais wala hata Waziri mkuu, jaji mkuu au spika!!

2) CCM imetengeneza sheria ya Tume ya Uchaguzi inayozuia kuishtaki Tume ya Uchaguzi hata kama itatenda uovu kiasi gani wakati wa kutimiza wajibu wake. Lengo ni lile lile, la kuofanya Tume ya Uchaguzi isiwe na hofu inapopewa maelekezoba viongozi wakuu ya kutenda uovu wakati wa uchavuzi. Duniani karibia kote, matokeo ya kura ya Rais yanaweza kuhojiwa mahakamani, lakini kwa Tanzania, Tume ya Uchaguzi ikiamua inaweza kumtangaza mgombea wa CCM aliyepata kura 1m ikamwacha aliyepata kura 5m, na hakuna anayetakiwa kuhoji!! Hii kweli ni nchi au danguro??

3) Serikali ya CCM imeweka sheria ya Kinga ya Makosa ya Jinai kwa Vyombo vya usalama. Haya yalikuwa ni maandalizi ya watawala kuvitumia vyombo hivi kutenda uharamia dhidi ya umma. Ni wapi Duniani ulikwishawahi kusikia eti vyombo vya usalama hata vitende jinai kwa kiasi gani wakati vikiwa kwenye utekelezaji wa majukumu yake haviwezi kushtakiwa? Kwa sheria hii, wale agents wa usalama walioingia kwenye basi na kumteka ndugu yetu, marehemu Ali Kibao, kama wananchi wangewazuia, maharamia wasimchukue, wangeweza kuwatandika risasi hata basi zima, halafu hakuna wa kushtakiwa kwa sababu wana Kinga Dhidi ya Makosa ya Jinai!! Hii kweli ni nchi au jehanamu? Inaonekana watawala waliojiandaa kutenda uovu kwa kutumia vyombo vya usalama. Waliona dhahiri kuwa vyombo hivi vya usalama vitakuwa na hofu ya kutekeleza amri zao ovu kwa kuhofia kushtakiwa. Sasa ili watekeleze uovu wanaoagizwa bila hofu, na wao wapewe kinga.

Tusishangae siku nyingine kusikia maRC, maDC na viongozi wote wakubwa wa CCM na UVCCM nao wamepewa kinga ya kutoshtakiwa.

Watanzania, tunashangaa nini kwa huu utekaji na mauaji yanayotokea sasa wakati maandalizi ya huu udhalimu yalikuwa dhahiri tangu muda mrefu?

Hivi kweli tunaweza kudanganyika kuwa hawa watekaji wanafanya hivyo kwa maamuzi yao wakati tunajua kabisa hizi sheria za kulinda uovu na uharamia wa hali ya juu, zimeanzia Serikalini, zikapelekwa kwenye lile Bunge lao bandia, halafu Rais kwa vile aliafiki, naye akatia sahihi?

Maadam sheria hizi bado zipo, waliozitengeneza wapo, dhamira yao ya uovu ipo pale pale, uovu wa watawala dhidi ya umma utaendelea kufanyika bila kikwazo chochote, labda umma uamue kuingia kwenye mapambano dhidi ya wadhalimu wa Taifa hili.
 
Back
Top Bottom