JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Ili kusitisha ajira kuwe kwa halali mbele ya sheria ni lazima kuwe na misingi na kufuata taratibu zilizoainishwa. Mwajiri anahitajika kua na sababu za halali na za haki za kusitisha ajira.
Mbali na sababu hizi za halali za kusitisha ajira, mwajiri ni lazima afuate taratibu za halali za kusitisha ajira kama zinavyoelezwa chini ya sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi ya mwaka 2004 na Kanuni za Utendaji Bora za mwaka 2007.
Taratibu za kusitisha ajira zinatofautiana kutegemea na sababu za kusitisha ajira lakini zote zina kipengele cha pamoja – Haki ya mfanyakazi kusikilizwa kabla maamuzi ya kusitisha ajira hayajachukuliwa dhidi yake.
37.-(1) Itakuwa si halali kisheria kwa mwajiri kusitisha ajira ya mfanyakazi bila ya kufuata haki.
(2) Kusitishwa kwa ajira na mwajiri si kwa haki ikiwa mwajiri
atashindwa kuthibitisha -
(a) kwamba sababu za kusitisha ni halali;
(b) kwamba sababu ni sababu ya haki -
(i) inayohusiana na mwenendo wa mfanyakazi, uwezo au kuendana; au (ii) inayohusiana na mahitaji ya uendeshaji ya mwajiri; na
(c) kwamba ajira ilisitishwa kwa kufuata taratibu za haki.
(3) Haitakuwa sababu ya haki kusitisha ajira ya mfanyakazi-
(a) kwa sababu kwamba -
(i) amefichua taarifa ambazo mfanyakazi ana haki au anatakiwa kufichua kwa mtu mwingine chini ya
Sheria hii au Sheria nyingine; (ii) ameshindwa au amekataa kufanya kitu chochote ambacho mwajiri hawezi kisheria kuruhusu au kumtaka mfanyakazi kufanya; (iii) ametekeleza haki yoyote iliyotolewa kwa makubaliano, Sheria hii au sheria yoyote nyingine; (iv) amejiunga au alijiunga kwenye chama chochote cha
wafanyakazi; au (v) ameshiriki katika kazi halali za chama cha wafanyakazi, ikujumuisha mgomo halali;
(b) kwa sababu-
(i) zinahusiana na ujauzito; (ii) zinahusiana na ulemavu; na (iii) ambazo ni za kibaguzi chini ya sheria hii.
Upvote
0