Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 441
- 1,065
TANZANIA TUNAHITAJI SHERIA YA MSAMARIA MWEMA ILI KUWAOKOA MAJERUHI
Ndugu Viongozi wetu
Imefika wakati sasa Tanzania tunahitaji sheria ya Msamaria mwema au kwa kiingereza Good Samaritan Law. Sheria hii itawezesha kuokoa maisha ya watu wengi waliojeruhiwa, hasa na ajali za barabarani tofauti na ilivyo sasa.
Ilivyo sasa ikitokea ajali, wenye ujasiri wa kuokoa majeruhi na kuwafikisha hospitali ni wachache sana. Ikiwa ni boda boda basi watafunga njia magari yasipite huku miili ya waliofariki na majeruhi imelala chini hadi polisi wafike. Kama bodaboda hawajafunga njia, basi wale waliokaribu na ajali watajitahidi kuwatoa watu kwenye magari, mtihani utakuwa kuwafikisha hospitali. Hapa ndipo kwenye kutafutana kila mtu anakwepa, hataki ushahidi.
Inasemekana ukimsaidia majeruhi ukampeleka hospitali, unaweza jikuta wewe ndio unawajibika kwa kila kitu. Maana utaandikishwa wewe pale. Chochote kikitaka kufanyika lazima wewe ndio utapigiwa simu. Kuna wakati utaitwa polisi na huko unaweza uwekwe ndani hadi uchunguzi ukamilike, au uwe unatakiwa kuripoti tu au uunganishwe kwenye kesi. Hizi ndizo hofu walizonazo wananchi. Lakini tukiwa na sheria ya Msamaria mwema hofu hizi zitaondoka.
Sheria ya Msamaria Mwema itaruhusu mtu yeyote ambaye kwa nia njema na huruma aliyonayo, bila kutarajia malipo, kwa hiyari yake anaamua kusaidia majeruhi wa ajali, iwe kwa kufanya uokoaji, kumtibu, au kumsafirisha na kumfikisha hospitali au kumuuguza akiwa hospitali, na mtu huyo atalindwa na sheria kwa matendo au makosa yanayotokana na usamaria wema wake.
Zipo nchi tayari zina sheria hii ikiwemo India. Juhudi zetu zote za kuzuia ajali hazina faida yoyote kama tunashindwa kupunguza vifo vinavyotokana na majeruhi wa ajali. Ndio sababu dunia imejikita katika kupunguza vifo na majeruhi zaidi kuliko kuzuia ajali ambazo kimsimgi hatuwezi kuzimaliza kutoka na kuwa kwa asili yake, binadamu daima ni mkosaji tu, hata ungeweka askari kila baada ya mita 1. Badala yake tunazuia madhara yatokanayo na ajali kwa kujenga barabara bora, salama, na zinazosamehe, pia kuwa na magari bora, salama na yanayosamehe makosa ya dereva.
Usaidizi tunaotaka kwa majeruhi wa ajali kwa sasa hauongozwi na sheria yoyote. Ndio sababu, askari anaweza kusimamisha gari akaomba dereva apakie majeruhi dereva akakakataa. Askari wanalazimika kulazimisha tu gari kubeba maiti au majeruhi. Hao wanaolazimishwa wakati mwingine hawabishii sana wakishafikiria suala la utu. Lakini wengine wanakataa kabisa.
Katika nchi ambayo hatuna magari ya kutosha ya wagonjwa, hatuna ambulance za helkopta, hatuna madaktari wa kutosha, wala waokoaji wa kutosha, ingekuwepo sheria ya madereva kulazimika kutoa msaada barabarani kama sehemu ya wajibu kwa umma (public duty) katika hali ya dharura, kama inavyosemwa katika ibara ya 25(3)(c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ingekuwepo sheria ya namna hiyo usiongeona mwili wa mwandishi wa Millard ayo aka Zuchy (RIP) kulala barabarani kwa muda mrefu huku Polisi wakisubiriwa waje, baada ya kuwa imetokea ajali. Madaktari wanasema dakika 3 hadi 4 (critical moments) baada ya kutokea ajali ni muhimu mnoo kuokoa uhai. Hivyo, wajibu wa watu wanaoshuhudia ajali (by-standers) ni muhimu sana katika kuokoa uhai.
Ni imani yangu viongozi wetu na watunga sheria mtaliona hili na kulifanyia kazi.
Copy and Paste from[emoji3596]
RSAadmin1
RSA Tanzania
Usalama Barabarani ni Jukumu Letu Sote