Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 302
Baraza la Wawakilishi Zanzibar linaanza mkutano wake leo ambapo pamoja na mambo mengine litajadili muswada wa kihistoria wa sheria ya kuanzishwa kwa serikali ya Mseto.
Idadi kubwa ya wakazi wa Zanzibar wakiwamo wanachama wa CCM na CUF, wasomi na wanasheria mbalimbali wameendelea kusisitiza kuwa kuupigia kura za maoni muswada huo ni kupoteza fedha na muda kwa kuwa tayari Baraza la Wawakilishi lilishatoa uamuzi kwa niaba ya Wanzibari.
Je nini maoni yako kuhusu kupigiwa au kutopigiwa kura ya maoni kwa huo muswada
Je kama BLW likiamua kutopigiwa kura ya maoni litaonekanje kwa baadhi ya viongozi hasa wa Ccm bara wanaodai kura ya maoni kabla ya kuundwa kwa serikali ya mseto.