Sheria ya kuanzisha Serikali ya Mseto Zanzibar kujadiliwa leo

Sheria ya kuanzisha Serikali ya Mseto Zanzibar kujadiliwa leo

Luteni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
2,274
Reaction score
302
Baraza la Wawakilishi Zanzibar linaanza mkutano wake leo ambapo pamoja na mambo mengine litajadili muswada wa kihistoria wa sheria ya kuanzishwa kwa serikali ya Mseto.

Idadi kubwa ya wakazi wa Zanzibar wakiwamo wanachama wa CCM na CUF, wasomi na wanasheria mbalimbali wameendelea kusisitiza kuwa kuupigia kura za maoni muswada huo ni kupoteza fedha na muda kwa kuwa tayari Baraza la Wawakilishi lilishatoa uamuzi kwa niaba ya Wanzibari.

Je nini maoni yako kuhusu kupigiwa au kutopigiwa kura ya maoni kwa huo muswada
Je kama BLW likiamua kutopigiwa kura ya maoni litaonekanje kwa baadhi ya viongozi hasa wa Ccm bara wanaodai kura ya maoni kabla ya kuundwa kwa serikali ya mseto.
 
Baraza la Wawakilishi Zanzibar linaanza mkutano wake leo ambapo pamoja na mambo mengine litajadili muswada wa kihistoria wa sheria ya kuanzishwa kwa serikali ya Mseto. Idadi kubwa ya wakazi wa Zanzibar wakiwamo wanachama wa CCM na CUF, wasomi na wanasheria mbalimbali wameendelea kusisitiza kuwa kuupigia kura za maoni muswada huo ni kupoteza fedha na muda kwa kuwa tayari Baraza la Wawakilishi lilishatoa uamuzi kwa niaba ya Wanzibari.

Je nini maoni yako kuhusu kupigiwa au kutopigiwa kura ya maoni kwa huo muswada
Je kama BLW likiamua kutopigiwa kura ya maoni litaonekanje kwa baadhi ya viongozi hasa wa Ccm bara wanaodai kura ya maoni kabla ya kuundwa kwa serikali ya mseto.
Luteni, nadhani wanajadili kesho na sio leo. Naangalia kama nitapata nafasi, nitadamkia barazani na kuwapasha mjadala utakavyokuwa. Kama kweli ni leo, basi nimeshachemsha!.
 
Luteni, kwa uhakika kikao cha BLW kinaanza kesho na ajenda ya kwanza ilikuwa ni kujadili muswada wa kura za maoni. Taarifa kutoka Zenj, kesho kikao kinaanza ila mjadala wa kura ya maoni sio kesho.
 
Mabadiliko ya katiba lazima yawahusishe watu,kwa tafsiri halisi,wawakilishi mamlaka yao yanaishia kutoa maamuzi kwa yale mambo ambayo sheria inaelekeza.Lakini kutungwa kwa kipengele cha sheria ambacho hapo awali hakikuwepo,na hasa mabadiliko ya katiba ,umma lazima ushirikishwe kikamilifu.Huo ndo uwakilishi makini.
 
.Lakini kutungwa kwa kipengele cha sheria ambacho hapo awali hakikuwepo,na hasa mabadiliko ya katiba ,umma lazima ushirikishwe kikamilifu.Huo ndo uwakilishi makini.

Mayenga, huo ushilikishwaji ni lazima uwe referendum? Katiba zetu zina viraka vingi tu, lakini sikumbuki kama kuna kura ya maoni iliwahi kupitishwa ili kupata maoni ya watz/zanzibari kwa kila mabadiliko yaliyofanywa kwenye katiba hizo. Mambo ya muungano ni mfano mmojawapo.
 
Luteni, kwa uhakika kikao cha BLW kinaanza kesho na ajenda ya kwanza ilikuwa ni kujadili muswada wa kura za maoni. Taarifa kutoka Zenj, kesho kikao kinaanza ila mjadala wa kura ya maoni sio kesho.
Nimekupata mkuu nini mawazo yako kuhusu referendum
 
pasco tupe habari za kinachoendelea

.Ilikuwa nitie timu huko leo ili kesho niamkie barazani, lakini mjadala wa kura ya maoni sio kesho, nimeahirisha mpaka nitakapojuzwa ni lini.Interest yangu kubwa kwa Wazanzibari kuhusu hii kura ya maoni kwa kitendo cha SMZ kuivalia njuga hayo maoni kuruhusu serikali ya umoja wa kitaifa.Katiba ya Zanzibar inamruhusu rais kuteua yoyote kuwa waziri, sio lazima atoke chama chake, kwa maoni yangu, hii kura ya maoni ni wastage of time and resources wakati ni wazi itapita kwa asilimia 100.Kitu cha kushangaza ni issues muhimu, nyeti na zinazogusa sovereinity ya Zanzibar kama nchi, zimeachwa zikipita juu kwa juu, bila hata kuwauliza Wanzazibari ama kura za maoni, ukiwemo muungano na mpaka leo wanaishia kupiga kelele na kulalama kutwa kucha, wamepata nafasi ya kura ya maoni, wanauliza swali moja tuu la kujibu ndiyo au hapana!. Hiki ni kichekesho!.
 
Nimekupata mkuu nini mawazo yako kuhusu referendum

Luteni, referendum ni kitu kizuri kufanyika kabla ya kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu mustakabali wa taifa lolote. Binafsi suala ya serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar halikuhitaji referendum, kama jambo kubwa kama kuupoteza utaifa wa Zanzibar na kujiingiza kwenye muungano, limefanyika bila referendum, hiyo serikali ya mseto/umoja wa kitaifa is nothing!.
 
.Interest yangu kubwa kwa Wazanzibari kuhusu hii kura ya maoni kwa kitendo cha SMZ kuivalia njuga hayo maoni kuruhusu serikali ya umoja wa kitaifa.Katiba ya Zanzibar inamruhusu rais kuteua yoyote kuwa waziri, sio lazima atoke chama chake, kwa maoni yangu, hii kura ya maoni ni wastage of time and resources wakati ni wazi itapita kwa asilimia 100.
Naamini kabisa kuna kitu ambacho hatujaambiwa ambacho ndicho hasa kinachotafutwa na haya tunayoyaona ni kama kanyabwoya tu. many time will tell
 
Naamini kabisa kuna kitu ambacho hatujaambiwa ambacho ndicho hasa kinachotafutwa na haya tunayoyaona ni kama kanyabwoya tu. many time will tell

kitu kama kipi Mkuu!!!!?
Kuvunjwa Muungano?
Kuanzishwa Serikali tatu?
Au Serikali moja?
Sema nini wasi wasi wako mkuu??
 
Mabadiliko ya katiba lazima yawahusishe watu,kwa tafsiri halisi,wawakilishi mamlaka yao yanaishia kutoa maamuzi kwa yale mambo ambayo sheria inaelekeza.Lakini kutungwa kwa kipengele cha sheria ambacho hapo awali hakikuwepo,na hasa mabadiliko ya katiba ,umma lazima ushirikishwe kikamilifu.Huo ndo uwakilishi makini.
Mbona kuna mambo mengi tu wananchi hawajashirikishwa? umesahau suala makamo wa rais lilivoondolewa? na mengi tu yapo.. lkn kwa sababu ya wapinzani kuingia kwenye madaraka,ndio vitatokea vijisababu vingi...
 
baraza la wawakilishi zanzibar linaanza mkutano wake leo ambapo pamoja na mambo mengine litajadili muswada wa kihistoria wa sheria ya kuanzishwa kwa serikali ya mseto. Idadi kubwa ya wakazi wa zanzibar wakiwamo wanachama wa ccm na cuf, wasomi na wanasheria mbalimbali wameendelea kusisitiza kuwa kuupigia kura za maoni muswada huo ni kupoteza fedha na muda kwa kuwa tayari baraza la wawakilishi lilishatoa uamuzi kwa niaba ya wanzibari.

Je nini maoni yako kuhusu kupigiwa au kutopigiwa kura ya maoni kwa huo muswada
je kama blw likiamua kutopigiwa kura ya maoni litaonekanje kwa baadhi ya viongozi hasa wa ccm bara wanaodai kura ya maoni kabla ya kuundwa kwa serikali ya mseto.
kura ya maoni ni muhimu.
 
Back
Top Bottom