Sheria ya madini kurudisha Ujamaa wa Nyerere kwa vitendo?

Sheria ya madini kurudisha Ujamaa wa Nyerere kwa vitendo?

Dodoma Demand

Senior Member
Joined
Oct 6, 2021
Posts
130
Reaction score
74
Poleni na majukumu ya kulijenga taifa,

Hapo kabla ya sheria mpya ya madini ya mwaka 2017,haijatungwa na kupitishwa, wakaguzi wa madini migodini walikuwa wanaenda kwenye vituo vya ukaguzi, hasa migodi mikubwa na ya kati kwa utaratibu wa mzunguko/rotations yaani leo upo hapa kesho pale, ili kukwepa mtu mmoja kukaa eneo moja kwa wakati wote kama misingi ya ukaguzi inavyohitaji. Hili lilikuwa linapelekea kuwa na makazi tofauti na sehemu za ukaguzi na kusababisha uthibiti wa biashara ya madini kuwa mgumu.

Baada ya marekebisho ya sheria mpya, mkaguzi anapaswa kukaa eneo la ukaguzi, ikiwa na maana stations kama sheria inavyosema. Hii itapelekea mkaguzi kukaa kituo kimoja aidha mpaka mgodi ufungwe au itokee hali nyingine ya kubalisha. Hili ni jambo jema, inawezekana likasaidia kupunguza matumizi ya wizara kama ilivyoelezwa. Japo pia linaonekana litakuwa na changamoto zake kiukaguzi. Kuanzisha MASOKO YA MADINI KATIKA KILA MKOA AMBAPO KWA SASA, Wizara yenye dhamana na MADINI imejenga masoko 28 katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo.

Soko kuu la Dhahabu Geita
Soko la Dhahabu Kahama
Soko la Dhahabu Singida
Soko la Dhahabu Chunya
Soko la Dhahabu na Vito Ruvuma
Soko la Dhahabu na Almasi Shinyanga
Soko la Dhahabu Katavi
Soko la Madini Kigoma
Soko la Dhahabu Tabora
Soko la Dhahabu Mara
Soko la Dhahabu Madini Mbeya
Soko la Bati Kagera
Soko la Dhahabu na Almasi Mwanza
Soko la Dhahabu Songwe
Soko la Dhahabu na Vito Iringa
Soko la Vito Tanga
Soko la Dhahabu Singida - Sekenke
Soko la Dhahabu Manyara - Mbulu
Soko la Dhahabu Morogoro
Soko la Dhahabu Dodoma
Soko la Dhahabu Manyara - Babati
Soko la Vito Tunduru Ruvuma
Soko la Dhahabu na Vito Lindi
Soko la Madini Mtwara
Soko la Vito Mahenge
Soko la Vito Arusha
Soko la Madini Kilimanjaro – Same
Soko la Madini Dar es salaam


Dhana inayotumika ni sawa kabisa na DHANA ya MASOKO YA USHIRIKA kipindi cha MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE ambapo kulikuwa na SOKO moja KWENYE ENEO MAALUMU - (MKOA KWA SASA). Ni mtazamo wangu tu na kueleweshana mawili matatu, Je watumishi wa WIZARA HIYO WATATUVUSHA KWENYE MAISHA YA KUKAA KWENYE KITI - BADALA YA KUFUKUZA FUKUZA MACHINGA/ PANGA PANGA MACHINGA KILA SIKU....

Nawasilisha

thumb_953_800x420_0_0_auto.jpeg
 
Wazo la haya masoko kila mkoa ni zuri sana. Wazo hilo hilo walifanye kwa mazao muhimu kwa kila mkoa.

Mkulima anapeleka mazao yake sokoni anakutana na wanunuzi, serikali, vyama vya ushirika, taasiso, wafanyabiashara kutoka Tanzania nzima na nje ya Tanzania. Chap chap anauza mazao yake.

Bei zinaweza kuwa zinawekwa mitandaoni kila dakika.

Ingekuwa vizuri pia kuwa na Bima ya mazao na facilities za kununua guarantees price for the futures. Uhakika wa bei kwa miezi na miala michache inayokuja.

Kujua bei, soko, bima in advance kutapunguza mzigo na pressure kidogo kwa mkulima.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Wazo la haya masoko kila mkoa ni zuri sana. Wazo hilo hilo walifanye kwa mazao muhimu kwa kila mkoa.

Mkulima anapeleka mazao yake sokoni anakutana na wanunuzi, serikali, vyama vya ushirika, taasiso, wafanyabiashara kutoka Tanzania nzima na nje ya Tanzania. Chap chap anauza mazao yake.

Bei zinaweza kuwa zinawekwa mitandaoni kila dakika.
Walau mkuu umenena!? Ngoja wasongo wa darasani watasemaje humu humu!. (WANAKITABU CHENYE MAJIBU MWISHONI NA MASWALI WANASOLVE HADI KIFO KINAWAKUTA NASI KINATUKUTA)
 
Back
Top Bottom