Sheria ya Mafao (Tanzania)

Sheria ya Mafao (Tanzania)

Bright Jr

New Member
Joined
May 7, 2018
Posts
2
Reaction score
0
Hello,
Naomba kufahamu kuhusiana na sheria ya mafao (Pension). iwapo nina wafanyakazi ambao ni part time, mfano daktari anayefanya kwenye kituo cha afya kwa masaa, sheria inanitaka nifanye makato ya pension? au ikiwa wafanyakazi wako kwa muda wakisubiri ajira nyingine, suala la pension kwao likoje?
Natanguliza shukurani.
 
Kama daktari huyo wa part time anasehemu nyingine anayofanya kazi na kuchangiwa pensheni wewe hautalazimika kumchangia ispokuwa utampa mshahara wake wote bila makato. Kama hachangii, hata kama anafanya kwako kazi nusu saa kwa siku afu unamlipa mshahara, huyo inabidi umchangie kwa lazima.

Au mnaweza kukubaliana na yeye uwe unamchangia ila michango yake utaipeleka kwenye mfuko wa hiyari (suplementary scheme) atakaouchagua yeye (m.f. NSSF Hiari, GEPF-VSRS, PSPF -PSS, PPF-Wote Scheme). Mifuko hii haitoi pesheni ispokua hua inarudisha michango na faida ya uwekezaji kama ipo. Atachukua hela zake anytime akimaliza mkataba na ww au akiamua kufanya hivyo anytime.

NB. Sheria ya Usimamizi Hifadhi ya Jamii (SSRA) hairuhusu mtumishi kuwa na mfuko wa pensheni zaidi ya mmoja. Na pia hairuhusiwi mtumishi mmoja kuchangia pensheni zaidi ya mara moja kwa mwezi uleule.
 
Ok, Asante sana
vipi ikiwa wafanyakazi wako kwa muda wakisubiri ajira nyingine, suala la pension kwao likoje?
Nina Nurses wanaosubiri ajira walizoomba serikalini ila kwa sasa ninafanya nao kituoni kwangu. Ninalazimka kuwalipia?
 
Back
Top Bottom