Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015: Kwa mkakati huu wa Serikali, Watumiaji wa Mitandao tutapona?

Informer

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,606
Reaction score
6,672

JamiiForums:

ILANI YETU

Tunasimama imara kudai mtandao huru na wazi.

Tunaunga mkono michakato wazi na shirikishi ya kutengeneza sera ya mtandao na uanzishaji wa kanuni tano za msingi:

Kauli: Kutodhibiti mtandao.

Upatikanaji: Kuza upatikanaji wa mitandao ya kasi na nafuu duniani kote.

Uwazi: Kuufanya mtandao wa intaneti kuwa wazi ambapo kila mtu ana uhuru wa kuunganishwa, kuwasiliana, kuandika, kusoma, kutazama, kuzungumza, kusikiliza, kujifunza, kuunda na kubuni.

Ugunduzi: Kulinda uhuru wa kugundua na kuunda bila kulazimika kuomba idhini. Msizuie teknolijia mpya, na msiwaadhibu wagunduzi kwa vitendo vinavyofanywa na watumiaji wa teknolojia zao.

Faragha: Kulinda faragha na kupigania uwezo wa kila mtu kudhibiti namna data na vifaa vyao vinavyotumika.


Muswada huu unatarajiwa kupitishwa Jumanne 31 Machi na Aprili 01, 2015 kwa hati ya dharura.


=======

Wakuu,

Baada ya kuisoma sheria tarajiwa ya makosa ya jinai kwa watumiaji wa mitandao (Cybercrime) ambayo inapitishwa Bungeni kwa hati ya dharura, napata shaka juu ya uhuru wa watanzania watumiao mtandao.

Serikali yetu imeamua kutuumiza watanzania kwa mara nyingine. Inauma, inasikitisha na hatuna wa kututetea.

Wameona kupunguza vifurushi pekee hakutoshi, wameamua kutupangia nini tuongee, nani aongee na aongee vipi. Watoa huduma watalazimishwa kutoa taarifa zetu na wakikataa wataadhibiwa "kwa mujibu wa sheria".

Kwa ufupi, serikali inataka kuamua upi ukweli na upi uwongo. Huu ni ubakaji mkubwa wa Demokrasia. Wengi tutafungwa kwa uonevu wa kipengele hiki.

Napata shaka zaidi kwa watumiaji kutokujua hatari inayokuja mbele yao na hivyo kuchukua tahadhari.
Aidha, nina mashaka sana kama wabunge wetu wanaelewa athari yake kwao pia maana kama walidhani wanalengwa JF tu, basi hii ina upana zaidi ya hapo.

Kwa kiingereza:

Na pia, kipengele cha 21 kinaihusu JamiiForums au wengine wanaotoa huduma kama hizi. Serikali yetu tukufu inataka iwe ni lazima taarifa za watu zitolewe na watoa huduma ili iweze kufanya uchunguzi.

Wanaharakati, wapinzani na wengine ambao Serikali yenu Tukufu huenda inawahofia au kuwatilia shaka, itawalazimisha watoa huduma kutoa siri zenu. (Email zenu hupita kwa ISP na sio encrypted):


Soma pia kuhusiana na watoa huduma:
Aidha, serikali hii tukufu imeamua kutumia kifungu cha 22 kuonyesha dhamira yake si ya kutania endapo itataka kupata taarifa za mtu na mtoa huduma akataka kuua ushahidi kama inayosomeka:
Angalieni kipengele hiki pia:

Tupo salama?

Ni kutaka kudhibiti taarifa wakati wa uchaguzi? Ni kuwalinda kina nani?

Isomeni sheria nzima hapa - http://mst.go.tz/index.php/componen...wnloads?download=24:the-cybercrimes-bill-2015

Nimeambatanisha kipengele ninachoona ni tatizo zaidi.

CC EMT, Mzee Mwanakijiji, Nguruvi3, Mchambuzi na wengine mnaoweza kututoa wasiwasi





 

Attachments

Ndiko tulikofika? All Assad na Gadaf walifanya hivyo, lakini hali ya kibinadamu ni ngumu na ya hatari sana,

Uchina na Urusi walijaribu havyo lakini utandaridhi vimewashinda,

Sasa kwetu si watafunga kila wanayemhisi tu bila ushahidi?
 
Ila itasaidia kwa upande mwingine
Sheria yoyote inasaidia, hatupingi hilo. Ila, vipengele kadhaa vimechomekwa kwenye sheria hii ili kuzima mitandao na kuibaka Demokrasia.

Wanaharakati wetu wameangalia upande mmoja wa traditional media, wamesahau kuwa the world is going digital
 
sasa mtakubaliana na mimi gogo la shamba nilipowaambieni viongozi wa ccm wataanza kutushughulikia sisi tunaowaambia ukweli au kulalamika na jinsi mambo yanavyokwenda huku kwenye vyombo yva habari, ila walichoshindwa kuelewa ni kwamba watajiumbua zaidi na yote hii ni kwa sababu wanafanya vitu kwa hila na hila sasa hivi haifichiki kwani watanzania wengi sasa hivi ni waelewa wa mambo kinachotakiwa kwa sasa ni kusema yaliyo kweli kama wafanyavyo viongozi wa chadema japokuwa ccm hawapendi ukiwaambia hivyo
 
Huyo ndo makamba anayetaka uraisi? huu ni upuuzi wa kiasi cha juu sana ukipitisha muswada namna hii
 
Nadhani wadau, JamiiForums kati kuhakikisha ukweli wa habari tuko mbele sana na ndiyo maana tunaona wana-Jamiiforums wako mstari wa mbele kuhoji uhalali wa habari /thread kwa ku-demand source, picha, video, nyaraka, kuchallenge data, trends n.k hii yote ni katika kuhakikisha thread imebeba habari za kweli na za kuaminika.

Kazi ipo kwa wanasiasa kudai wapinzani ni magaidi, wanajilipua kwa mabomu ktk mikutano, wanapanga njama za kupindua serikali n.k bila uthibitisho na wala hatuoni POLISI wakifuatilia madai hayo.
 
Wakati kina Mange Kimambi wanaita watu Malaya, wanatusi watu pasina hatia hakuna sheria inayowaba. Wakati kila mtu siku hizi anaweza fungua blog na kutusi watu hakuna sheria inayombana.

Wapo wajinga wengi tuu wanao tuma picha za watu uchi na kuzisambaza kwenye whatsapp na hakuna sheria ya kuwabana.

Cyber law zipo kila nchi, USA leo ukidelete hard drive yako ni crime evidence alteration. Kutaka mtandao uwe free kila mtu atukane watu atakavyo sio haki.

Nadhani swala la msingi liwe ni kuifanyia marekebisho sheria ili isizuie Uhuru wa Kuzungumza. Lakini mchezo wa matusi ukome.
 
Sijafuatilia vyombo vya Habari na bunge kwa ukaribu kipindi Hichi Ila kwa kusoma bandiko lako Mkuu kama hali ndio hii na CCM wapo radhi kwa hili Basi kweli naamini Serikali ya mtaa wa lumumba ina hali mbaya, imeanza mpk kuogopa Raia wake wema eti wasipeane Habari, nini wanaogopa,kwamba yericko na wenzake ipo Siku watawataja waliopokea mgao wa singasinga.......Nchi inarudi kinyume nyume badala ya kwenda mbele, Kwanini wasipeleke Sheria kali za kuwabana mzee wa makengeza na Co.yake.........
 
Kazi ipo.

Ilza wasisahau kuwa sheria ni "Msemeno" Hivyo aita kula kwetu tu bali ata kwao pia. Wapi Kova na mtekaji wa Dr. Ulimboka? Mwigulu na kauli zake za Ugaidi?

Zaidi naona itakula sana kwa Nape Nnauye maana yule bila kuongea uongo na kusingizia watu hawezi fanya uenezi.

Time will tell
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…