Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015: Kwa mkakati huu wa Serikali, Watumiaji wa Mitandao tutapona?

Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015: Kwa mkakati huu wa Serikali, Watumiaji wa Mitandao tutapona?

Inasikitisha sana wakati dunia inakwenda mbele, Tanzania tunalazimishwa kupiga rivasi kurudi nyuma! Zinatungwa sheria za kutufunga midomo na kupata sababu za kuwafunga jela watoto wa wenzao! Mungu ni wa haki na atatupigania.

Nimesoma na kukirudia hicho kifungu siamini! Hata uwe na akili chache kiasi gani unajua kimetungwa specifically for JF!

Its a sad day!
 
Sasa kutofautisha habari za uongo na ukwel kwa mwananchi wa kawaida ni ngumu sana, Serikali inawajibu wa kukanusha na kuwaeleza wananchi wake ukweli, ni mjinga pekeeanaeweza kuisimamisha dunia kwa sasa.....

Kuna namna nyingi sana za kupashana habari, hii siyo nchi ya ki kommunist, wala inayoamini unyerere tena na hakuna wa kutuziba mdomo, kinachoshangza serikali yenyewe ndio inayochapisha vitu vya uongo, nimepatwa sana na hasira nikikumbuka umaamuma uliokuwa unatengenezwa huko Tanga, na bado ni ujanja wa kutumanage...

Kama kufungwa tu hakuna tatizo na mtufunge wote..will never shut up.... go tell your kids in international schools abroad..these poor, illiterate, un informed, extremists or whatever has decided... mtufunge na mtuuwe we will never let you and your family rule us forever...
 
Lakini mkuu, katika ile sheria ya taarifa za uongo mimi binafsi sioni kama kuna tatizo.

Kumekuwa na upotoshaji mwingi sana kupitia mitandao nadhani hii sheria itasaidia kidogo
 
bagamoyo;

Ni kweli mkuu hii sheria ni ya muhimu sana kama kweli itatekelezwa bila upendeleo kwa kuzingatia The rule of law
 
Last edited by a moderator:
eeeee ibariki Tanzania wabariki viongozi na wananchi wake
Ameen Ameen Ameen Ameen.
 

Natumai muwazima;

Wakati JF kwa wengine inakuwa ukumbi wa mijadala ni muda sasa mkapitia Sheria nje na JF rules.

Maoni yenu hata kwa kulobby kupitia wabunge wenu ambao wengine humu ni Member ndiyo muda wake ,kabla hawaja sema ndiyoooooooooooooooo! Na Spika kumalizia waliosema ndiyoooooooo wameshinda.




Mimi na anza na huu utamaduni mbaya wa Kikoloni.
Nini maana ya Utawala wa Sheria kama Mtu mmoja anaweza kuamua jambo kwa uzito uleule wa Mahakama Kuu.

Na hili la Waziri kutunga Kanuni. Kuna haja Kanuni hizi pamoja na Kanuni zingine zote kujadiliwa na wadau na pia Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria kuijadili na kuipigia Kura tena ya Wazi-kinyume na hivyo hakuna utawala wa Sheria.


Lazima Mswada wa Sheria hii wadau wengi washirikishwe ilikuleta ufanisi na kuwa Sheria Bora.


50.-(1) Bila kuathiri sheria nyingine inayotumika Tanzania Bara, Mkurugenzi wa Mashtaka, muda wowote kabla ya mwenendo wa mahakama kuanza na kwa kuzingatia tamko la kukiri kosa kwa hiari la mshitakiwa anaweza kufifilisha kosa na kuamuru mtu huyo alipe kiasi cha pesa atakachokitaja ambacho hakitazidi kiasi cha faini kwa kosa hilo.
(2) Amri ya kufifilisha kosa chini ya kifungu kidogo cha (1) itakuwa -
(a) ya maandishi, ikiainisha kosa lililotendeka, kiasi cha fedha zitakazolipwa na tarehe ya kufanya malipo ikiambatanisha tamko la kukubali kosa lililorejewa chini ya kifungu kidogo cha (1);
(b) ni uamuzi wa mwisho na hautakatiwa rufaa; na
(c) na uwezo wa kutekelezwa katika namna sawa na amri ya Mahakama Kuu.
Mamlaka ya kutengeneza Kanuni


51. Waziri anaweza kutunga Kanuni kuhusiana na jambo lolote ambalo linatakiwa kuainishwa na Sheria hii au ambalo ni la umuhimu au uharaka kwa ajili ya utekelezaji wa masharti ya Sheria hii.


CC EMT Mzee Mwanakijiji Pasco Ben Saanane Yericko Nyerere n.k
 
Last edited by a moderator:
Me nafikiri kabisa hatuwezi kufanya lolote kuzuia hizo sheria.. na kila nchi zina hizo sheria za kudhibiti matumizi ya mitandao ya kijamii!

Jf ambacho wanatakiwa kujifunza au kuchukua tahadhari ni kuanza moderatio ya aina yake ambayo haitokuwa na huruma na mtu anaye vunja kanuni makusudi na wasitegemee tena watu mpaka wa report abuse kinacho takiwa ni kukakagua kila kinacho anzishwa kwenye majukwaa na kusiwe na huruma tena!

Kwa hali ilivyo ni lazima sheria za namna hii zije japo zinahitaji marekebisho lakini tusitegemee kwa ukuaji wa technology kusiwepo na sheria za namna hii!
 
Le mutuz

Njoo huku umekuwa mdau wa Kipengele hii.Pengine unaweza kuleta maboresho mazuri.


Unyanyasaji kwa kupitia mtandao

23.-(1) Mtu hataanzisha au kukadimisha mawasiliano yoyote ya kielektroniki kwenda kwa mtu yoyote kwa kutumia mfumo wa kompyuta, kwa lengo la kurubuni, kulazimisha, kutisha au kunyanyasa au kusababisha maudhi ya hisia.
(2) Mtu akataye kiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na atawajibika, iwapo atatiwa hatiani, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni tatu au kutumikia kifungo kwa kipindi cha kisichopungua mwaka mmoja au vyote.

CChttps://www.jamiiforums.com/member.php?u=14452 @W.J.Malecela
 
Lakini mkuu, katika ile sheria ya taarifa za uongo mimi binafsi sioni kama kuna tatizo.

Kumekuwa na upotoshaji mwingi sana kupitia mitandao nadhani hii sheria itasaidia kidogo

Ukiwa sio muongo, mdaku sheria ni murua Kabisa...

Itasaidia tusome vitu vya ukweli sasa sio mazagazaga. Sometimes we waste a lot of time kusoma maujinga ambayo mtu Hana hakika naye.

kenya ma-blogger mbalimbali waliingia kwenye mikono ya Pilato kwa kucheza na sheria kama hii.
 
Ukiwa sio muongo, mdaku sheria ni murua Kabisa... Tutaanza kusoma Vitu vya ukweli sasa sio mazagazaga. Sometimes we waste a lot of time kusoma maujinga ambayo mtu Hana hakika nayo.
Watawala wenyewe wanapotosha mangapi kwa maslahi yao ya kisiasa?

Huu ni ushahidi kuwa CCM wana hali mbaya na si vinginevyo.
 
Hivi hapo kwenye kifungu cha 16 neno sahihi lilipaswa kuwa ni mfumo wa computer au mfumo wa ki-electronic?

Na mimi sasa nimekaa kama kamati nyuma ya keyboard yangu nikitunga sheria(sheria kandamizi) kupitia hapa JF.
 
cyber laws zipo kila nnchi lakini kwa hii yetu imetungwa kwa hasira Sana.
yaani sheria inamakosa mengi Sana,ilankwa kuwa hapa Tz ni wapole sijui tumerogwa,hakuna hata wana harakati wa kwenda mahakamani kuipinga hii sheria kandamizi.
majuz hapa kenya walipitisha sheria shenzi ,tuliona upinzani na wana harakati kukimbilia mahakamani na vipengele flan vikakosolewa na mahakama.
hapa kwetu yupo kimyaaaaa,wapi wana harakati .
 
Mi naona ni sawa maana uongo na taarifa za kuchafua watu vimezidi
 
Lakini mkuu, katika ile sheria ya taarifa za uongo mimi binafsi sioni kama kuna tatizo.

Kumekuwa na upotoshaji mwingi sana kupitia mitandao nadhani hii sheria itasaidia kidogo

Nimemshangaa mleta Uzi kwa kujaribu kutuaminisha ndivyo sivyo,sasa ulitaka kupost habari za uzushi ili ikusaidie nini mkuu ama napata mashaka kidogo yawezekana na wewe ako ndo katabia kako ...kama uko smart why worry?
 
Huyo ndo makamba mchumia njaa anayetaka uraisi?huu ni upuuzi wa kiasi cha juu sana ukipitisha muswada namna hii

January Makamba na Membe wanapenda vitu kama hv kwa kuhofia watu kuwaumbua matendo yao nyuma ya pazia.
 
Nukushi zingine zako wakati mwingine zinawalakini mkubwa sana! Jaribu kufanya utafiti wa kina badala ya kuwa projected na western media ... Ghadaffi na Assad ??? how? ... USA na Russia wanafanya kimya kimya siyo kupitisha sharia za kipuuzi kama hii ya CCM... Anyway nakubaliana na wengi kuwa Sheria hii inalenga kupunguza uwezo wa wananchi kutoa taarifa kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu!!! Wanajua wananchi wengi wana simu zao ambazo watakuwa wanapiga picha ya matokeo kwenye vituo na kuzisambaza kabla tume ya uchaguzi haijachakachua kama kawaida yao ..

Ndiko tulikofika? All Assad na Gadaf walifanya hivyo, lakini hali ya kibinadamu ni ngumu na ya hatari sana,

Uchina na Urusi walijaribu havyo lakini utandaridhi vimewashinda,

Sasa kwetu si watafunga kila wanayemhisi tu bila ushahidi?
 
Back
Top Bottom