Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015: Kwa mkakati huu wa Serikali, Watumiaji wa Mitandao tutapona?

Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015: Kwa mkakati huu wa Serikali, Watumiaji wa Mitandao tutapona?

Nimeufurahia sana huu muswada hakika utaturudisha kwenye mstari gud job January makamba uchochezi na chuki zisizo namsingi uongo nafikir vitapungua km sio kuisha kabisa.
Haya yanayofanyika humu tunayaona madogo ila yanaimpact kubwa sana hususan kwenye jamii yetu nakizazi kijacho hatuna sababu yakuleta habar ambazo zitaleta chuki ama udhalilishaji kila mtu anawajibu wakulinda maadili ya nchi hii sambaza upendo na siyo chuki
 
jani watunga sheria wetu ndio wahusika wakuu wa mauaji ya albino
Tume ya uchaguzi ikisema kuwa chama chetu kimeshinda chama chao kwa asilimia 63% Hatutaki ipingwe kama matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo kuna watu walikuwa wanajitokeza na taarifa za kweli, halisi, zilizosainiwa na mawakala wa vyama vyote kuwa Chama chao kilishinda chetu kwa asilimia 53%. Hao wanaosema hivyo hata kama ni kweli lazima watiwe msukosuko. Tusopofanya hivyo tumekwisha!
 
Utekelezaji wake ni mgumu ukizingatia SIRIKALI haina mfumo madhubuti wa kudukua mawasiliano. Il kwa upande mwingine mswaada huu utatumika kama silaha ya kusigina Uhuru wa habari na kutoa maoni kama inavyoainishwa na katiba yetu..
 
Kama wangejiwekea sheria kali kama hizi kuzuia ufisadi wao na kujilimbikizia mali hovyo kama machizi tungefika mbali kama taifa.

wako bize kuwaweea sheria wanaowatawala, ila wao watawala, rushwa na takrima wameziweka kundi moja, na posho ni kubwa kuliko mishahara yao. wanaonaje wakimaliza hii bill waje na bill ya kutenganisha biahsara na uongozi wa nchi?then walete bill ya kupiga marufuku posho zote pamoja na matumizi ya anasa ya kodi za wananchi?
 
[h=3]Wabunge watano watikisa Bunge la 19[/h]
Mbunge huyo wa Mkanyageni aliibuka Machi 20 na kutoa hoja ya kutaka muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Uhamiaji namba 54 wa mwaka 2014, kutojadiliwa bungeni kwa sababu unagusa mambo ya muungano, ambapo katika hoja yake alisema kama uhamiaji ni eneo la muungano, iweje muswada huo upitishwe na Bunge hilo bila theluthi mbili ya wabunge kutoka Zanzibar kama Katiba inavyotamka.


Je na huu mswada utafuata Mkondo huu au lah!


Application
2. Save for section 50, this Act shall apply to Mainland Tanzania as well as Tanzania Zanzibar.
 
Ni sheria madhubuti nilimsikiliza 'Mike' akiwa mkasi anasema JF sio content owner wa habari za humu ndani sawa, lakini surely they have that responsibility ya kuhakikisha jamii aipotoshwi.

Kama ni sawa kwao kufuta habari ambazo za uongo walizozibaini pia wanawajibu wa kuwataja watunga uongo if you have over a million views daily and people write all sorts of lies about other people and events unawajibu wa kuwataja vievile kwa sababu umejitoa kwenye umiliki wa maandishi mtu anapofungua civil case au serikari inapoona imetungiwa uongo.

Imefikia hatua watu wanatunga story kwa kuweka fake letters or accounts (mfano diamond kupata barua ya TRA) ambazo wametengeneza wenyewe na kutuaminisha wengine vitu vya uongo surely lazima hizi tabia zikomeshwe. Au hizi blogu ambazo kila kukicha ni hadithi tu zisizo na kichwa wala miguu zimezidi.

Ethics za habari ni ukweli unaweza kuwa na perpsective yako lakini si kutunga from the beginning to end na kutuaminisha wasomaji vitu vya uongo ukiongeza na magazeti yanayoandika habari za watu kuzaa nyoka na upuzi mwengine yamezidi it is about time we head towards ethical reasoning in informing the public upuuzi umezidi kwakweli.
 
inasikitisha kuona kuwa wanatunga miswada mikali kwa mambo ambayo athari zake kiuchumi na kijamii ni ndoga sana kulinganisha na mambo kama ufisadi, wizi wa kura, mauwaji, uharibifu wa miundombinu, ajari za barabarani n.k. Hii hiwezi kusaidia taifa kusonga mbele!
 
Mimi nadhani JF kama mtandao wenye watumiaji wengi zaidi Tanzania ingewakusanya wadau wa tovuti nyingine kubwa na watumiaji wa mitandao wanaojulikana kama Mzee Mwanakijiji nk wafanye kitu kama brainstorm halafu waandike mapendekezo ya marekebisho wanayodhani yanafaa na kuyawasilisha kwa kamati iliyohusika na kuandaa huu muswada badala ya kuishia kulalamika hapa. Hivi ndivyo wenzetu wanavyofanya kazi, hata Facebook, Google, Twitter etc kukiwa na bill inayotaka kupitishwa huwa wanafanya lobbying Washington kama ilivyokuwa kwenye muswada wa wahamiaji ambao ungewaathiri maelfu ya wafanyakazi wa makampuni hayo ambao wengi ni raia wa Asia na Amerika Kusini.
 
Mkuu kwa serekali kuamua kudhibiti taarifa au habari tunazozipata sisi wananchi ni suala la kawaida kabisa.hii ni kuepuka kiliingiza taifa kwenye machafuko.china wameblock facebook,twiter,youtube na links nyingine nyingi tuu ili ku control taarifa wanazopata wananchi.and believe me,kwa sisi wananchi wa kawaida kuna mambo mengi ambayo ili kuishi kwa amani na furaha ni vizuri kama hatutayajua.serekali haziendeshwi kwa namna tunavyofikiria.be blessed!
 
Waongeze ukubwa wa magereza maaana nahisi yaliyopo hayatatosha!
 
Hii si sawa watu tutafungana sana ila ccm wakipigwa chini october hyo sheria itanoga sana
 
sasa tupeane mawazo what to do????

maana ikishapitishwa ni hatari
 
sioni haja ya kua na muswada wenye kurasa nyingi wakati wangeweza kuweka maneno machache kua serikali haitaki wananchi tutumie internet basi sio kuuma uma maneno huku dhamira iko wazi




eti usi tume picha ya mtu Bila permission utampata wapi Messi umwombe permission

hii mijitu iliyitunga huu mswada haifai mbinguni wala duniani
 
baada ya kuweka sheria Kali kwa mafisadi,upuuz mtupu
 
wanachi tuweke petition kupinga muswada huu

kwa anaye weza kutengeneza online petition atengeneze tuweke sign zetu kupinga ufedhuli huu
 
Back
Top Bottom