Iwapo mh.Raisi atasaini muswaada wa makosa ya mtandao na kuwa sheria,moja ya matakwa ya utekelezaji wa sheria hiyo itakuwa ni kuwataka watoa hudumu(wamiliki wa mitandao na blogs) kutoa taarifa mbalimbali za watumiaji zikiwemo taarifa za majina halisi ya watumiaji wa mitandao na blogs mbalimbali na itakuwa ni kosa,kwa mujibu wa sheria,mtoa huduma kutotoa taarifa hizo pindi zinapotakiwa.
Sasa wadau,kwa sheria hii,haya majina ya bandia(fake ID) tunayotumia yatakuwa na maana na umuhimu wake wa awali?
Sipati majibu kabisa!
mkuu hakuna mfumo wa kutambua jina halisi na mtu mfano wewe unatumia salary slip lakini ukitaka jina halisi maana yake utaitwa mfano john joseph ila lakini hakuna mfumo wa utambuzi wa jina la mtu halisi maana unaweza ukaregister kwenye system ya JF kwa jina lolote ilimradi halimo kwenye database yao ingekuwa Tanzania imeendelea mfumo ambayo ungetumiwa ni mtu akifanya registration kunakuwa na fingerprint ya kumtambua