Mleta mada huna ufahamu wa kutosha kuhusu jambo unalozungumzia. Taratibu za manunuzi zinapaswa kufanana, tofauti kubwa huwa kwenye thamani ya manunuzi ili kufanya manunuzi ya thamani kubwa kuchukuliwa na mamlaka za juu!
Kama dawa zinafikia kununuliwa zikiisha, hilo sio tatizo la sheria za manunuzi. Ni udhaifu katika demand forecast, au long lead times, au reorder points kuwa karibia na sifuri, au kukosekana kwa safety stock na mambo mengine kama kuwa na supplier asiyefaa. Madhaifu hayo sio ya sheria za manunuzi, ni wa mipango ya manunuzi (acquisition au requirements planning).