Midimay
JF-Expert Member
- Apr 12, 2015
- 3,036
- 5,039
Habari za jioni wana JF wenzangu.
Mtakumbuka kwamba kulikuwa na mada moto moto katika Bunge lililopita, ambalo lilikuwa maalum kwa ajili ya bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2022/2023, kwa maana nyingine ni Bunge Maalum kwa ajili ya kujadili utekelezaji wa mipango ya serikali kwa mwaka wa fedha uliopita na mipango ya serikali kwa mwaka huu wa fedha tulionza.
Katika mada hizo moto moto, kulikuwa na mada mbili zilizoigusa Wizara ya Maliasili na Utalii chini ya mama Pindi Chana kama waziri mwenye dhamana. Mada zenyewe ni;
1. Suala lililohusu Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro(NCA)
2. Suala la upandishaji hadhi Mapori Tengefu(Game Controlled Area, GCAs)
Masuala yote mawili yalipata mapinagmizi kutoka na watu mbali mbali wakiwepo wabunge wanaotokea maeneo yaliyoathiriwa au ambayo yangeathiriwa na maamuzi hayo ya serikali kupitia wizara husika.
Tuachane na suala la NCA, tuangalie suala la upandishaji hadhi mapori tengefu, GCAs;
Mapori Tengefu yapo kwa mujibu wa Wildlife Conservation (Game Controlled Areas) Order, 1974 (G.N. No. 269 of 1974).
Ukisoma katika sheria hiyo, kati ya mapori 49, mapori 14 yapo katika eneo lililokuwa likijulikana kama Maasai District ambayo kwa sasa ni wilaya za;Mtakumbuka kwamba kulikuwa na mada moto moto katika Bunge lililopita, ambalo lilikuwa maalum kwa ajili ya bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2022/2023, kwa maana nyingine ni Bunge Maalum kwa ajili ya kujadili utekelezaji wa mipango ya serikali kwa mwaka wa fedha uliopita na mipango ya serikali kwa mwaka huu wa fedha tulionza.
Katika mada hizo moto moto, kulikuwa na mada mbili zilizoigusa Wizara ya Maliasili na Utalii chini ya mama Pindi Chana kama waziri mwenye dhamana. Mada zenyewe ni;
1. Suala lililohusu Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro(NCA)
2. Suala la upandishaji hadhi Mapori Tengefu(Game Controlled Area, GCAs)
Masuala yote mawili yalipata mapinagmizi kutoka na watu mbali mbali wakiwepo wabunge wanaotokea maeneo yaliyoathiriwa au ambayo yangeathiriwa na maamuzi hayo ya serikali kupitia wizara husika.
Tuachane na suala la NCA, tuangalie suala la upandishaji hadhi mapori tengefu, GCAs;
Mapori Tengefu yapo kwa mujibu wa Wildlife Conservation (Game Controlled Areas) Order, 1974 (G.N. No. 269 of 1974).
1. Arumeru
2. Kiteto
3. Longido
4. Monduli
5. Ngorongoro na
6. Simanjiro
Kwa maneno mengine naweza nikasema ni zaidi ya asilimia 80 ya mikoa ya Arusha na Manyara yalitengwa na Mkoloni Mwingereza kama mapori tengefu na serikali yetu ikarithi kama ilivyo baada ya uhuru.
Mapori katika mikoa hiyo ni:
1. Burunge
2. Kitwai
3. Lake Natron
4. Lolilondo
5. Lolkisale
6. Longido
7. Meserani Dam
8. Mto wa Mbu
9. Ngeju Njiro
10. Ngorongoro
11. Ruvu Masai
12. Sanya Lelatema
13. Simanjiro
14. Enduleni GCA
Sasa kwa hali hiyo unaona kabisa kwamba pamoja na malengo ya uhifadhi lakini wakoloni walikuwa na malengo mengine.
Pamoja na kwamba wakoloni hawakuwepo mwaka 1974 wakati serikali ilipotangaza tena jedwali husika kwenye gazeti la serikali, bado kunakuwa na ukweli kwamba serikali imenakili sheria ya wakati wa ukoloni. Hata hivyo, pamoja na uwepo na sheria hiyo, hakujawahi kuwepo kwa hofu, mgogoro wala mtafaruku katika maeneo husika except Ngorongoro na Loliondo. Sababu ya kuendelea kuwepo kwa utulivu ni busara ya serikali zilizopita katika nchi yetu. Lakini utulivu huo ulitaka kuondoka mwaka huu 2022 na kuja kwa kinyume chake kwa maana ya hofu, migogoro na mitafaruku.
Kabla ya kuendelea, ni muhimu kwanza tujue maana ya Pori Tengefu(Game Controlled Area, GCA) na pia tofauti ya GCA na Pori la Akiba(Game Reserve).
Ifuatayo ni definition ya Pori Tengefu(Game Controlled Area, GCA) kwa mujibu wa Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania(TAWA) kwa Kiingereza;
"Game Controlled Areas are areas declared for conservation of wildlife outside village land where activities detrimental to wildlife are prohibited".
Kwa lugha ya Kiswahili tunaweza kusema: Pori tengefu ni eneo lililotengwa kwa ajili ya uhifadhi nje ya mipaka ya ardhi ya kijiji(vijiji).
Kwa mujibu wa Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009; Mwenye mamlaka ya kuanzisha pori tengefu ni Waziri Mwenye dhamana(soma section 16, ofcourse sheria inasema waziri anaweza akatangaza "any area" of Tanzania kuwa GCA) na sheria ya TAWA section 31.
Hizi definition ni muhimu sana kwa sababu ya kile ambacho TAWA walitaka kuishauri Wizara, Bunge na Mamlaka ya Juu ya Nchi.
Kwa upande mwingine Pori la Akiba(Game Reserve) kwa mujibu wa TAWA ni kama ifuatavyo:
"Game Reserves are categories of wildlife protected areas which are declared for the purpose of conservation. Both consumptive and non-consumptive wildlife utilization are allowed after permit has been obtained from the Director of TAWA. No human activities are allowed, unless, with permit granted by the Director of TAWA."
Ni Rais wa nchi tu ndio mwenye dhamana ya kuanziisha Game Reserve kwa mujibu wa sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori section 14 na sheria ya TAWA section 28.Pamoja na kwamba wakoloni hawakuwepo mwaka 1974 wakati serikali ilipotangaza tena jedwali husika kwenye gazeti la serikali, bado kunakuwa na ukweli kwamba serikali imenakili sheria ya wakati wa ukoloni. Hata hivyo, pamoja na uwepo na sheria hiyo, hakujawahi kuwepo kwa hofu, mgogoro wala mtafaruku katika maeneo husika except Ngorongoro na Loliondo. Sababu ya kuendelea kuwepo kwa utulivu ni busara ya serikali zilizopita katika nchi yetu. Lakini utulivu huo ulitaka kuondoka mwaka huu 2022 na kuja kwa kinyume chake kwa maana ya hofu, migogoro na mitafaruku.
Kabla ya kuendelea, ni muhimu kwanza tujue maana ya Pori Tengefu(Game Controlled Area, GCA) na pia tofauti ya GCA na Pori la Akiba(Game Reserve).
Ifuatayo ni definition ya Pori Tengefu(Game Controlled Area, GCA) kwa mujibu wa Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania(TAWA) kwa Kiingereza;
"Game Controlled Areas are areas declared for conservation of wildlife outside village land where activities detrimental to wildlife are prohibited".
Kwa lugha ya Kiswahili tunaweza kusema: Pori tengefu ni eneo lililotengwa kwa ajili ya uhifadhi nje ya mipaka ya ardhi ya kijiji(vijiji).
Kwa mujibu wa Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009; Mwenye mamlaka ya kuanzisha pori tengefu ni Waziri Mwenye dhamana(soma section 16, ofcourse sheria inasema waziri anaweza akatangaza "any area" of Tanzania kuwa GCA) na sheria ya TAWA section 31.
Hizi definition ni muhimu sana kwa sababu ya kile ambacho TAWA walitaka kuishauri Wizara, Bunge na Mamlaka ya Juu ya Nchi.
Kwa upande mwingine Pori la Akiba(Game Reserve) kwa mujibu wa TAWA ni kama ifuatavyo:
"Game Reserves are categories of wildlife protected areas which are declared for the purpose of conservation. Both consumptive and non-consumptive wildlife utilization are allowed after permit has been obtained from the Director of TAWA. No human activities are allowed, unless, with permit granted by the Director of TAWA."
Nadhani sasa kwa wale mnaosoma, mmelewa maana ya GCA na tofauti yake na GR (Game Reserve).
Ukisoma maelezo yaliyopo mbele ya jina la kila pori katika jedwali la sheria ya uhifadhi ya mwaka 1974, utaona kwamba mipaka iliyotajwa kwa wanaofahaamu, inachukua maeneo ambayo yalikuwa vijiji kabla ama yalianzishwa vijiji baadaye na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mifano mizuri ni:
1. Pori Tengefu la Mto wa Mbu ambalo kwa mujibu wa maelezo ya mipaka yake kwenye jedwali, linachukua tarafa yote ya Manyara na tarafa yote ya Makuyuni na sehemu ya Tarafa ya Kisongo; zote katika Wilaya moja ya Monduli.
2. Pori la Akiba la Lolkisale ambalo nalo linachukua eneo lililobaki la tarafa ya Kisongo ndani ya Wilaya ya Monduli hadi kuja kupakana na mapori ya akiba ya Burunge na Mto wa Mbu.
3. Mapori ya akiba ya Lake Natron na Longido ambayo yanachukua Wilaya nzima ya Longido.
4. Mapori ya akiba ya Kitwai, Simanjiro na Ruvu Masai ambayo yanachukua ardhi yote ya Wilaya ya Simanjiro.
5. Mapori ya akiba ya Endulen, Ngorongoro na Loliondo yanayochukua ardhi yote ya Wilaya ya Ngorongoro.
Sasa natamani kila mmoja atakayesoma hapa na mwenye nia njema na Taifa letu na watu wake aone jinsi ambavyo tumerithi sheria kandamizi iliyopitwa na wakati kwa sababu ni ya wakati wa kikoloni.
Hivyo basi:
1. Maeneo yote tengefu yaliyotajwa yana vijiji na wananchi wakiendelea na shughuli zao za kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni.
2. Hakuna pori lililopo nje ya ardhi ya vijiji kama ambavyo TAWA wanatambua GCA kwa mujibu wa maelezo yao kwenye tovuti yao.
3. Uanzishaji wa mapori ya akiba ulikuwa kandamizi na ya kibaguzi kwa sababu uliaelemea upande mmoja wa nchi na hivyo kuwa na risk(uhatarishi) wa kuumiza kijamii na kijiografia.
4. Hatukupaswa kurithi sheria kandamizi na ya kibaguzi ya wakati wa ukoloni.
Hata hivyo kama nilivyosema juu kwamba hali ilikuwa shwari hadi pale wizara ya Maliasili na Utalii kupitia makadirio ya mapato na matumizi ya wizara katika mwaka wa fedha 2022/2023 walipokuja na mapendekezo ya kupandisha hadhi(kinyume cha sheria), mapori yafuatayo, kutoka mapori tengefu(GCA) kuwa mapori ya akiba(Game Reserve);
1. Lake Natron
2. Loliondo
3. Lolkisale
4. Longido
5.Mto wa Mbu
6. Simanjiro
7. Ruvu Masai
8. Ruvu Same
Na mengine ambayo sijayataja kwa sababu sio msingi wa hoja zangu katika post hii. Ila jumla yalikuwa mapori 12; 8 kati ya hayo yakienda kuathiri shughuli za kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni katika maeneo yale yale yaliyolengwa na mkoloni kwa sababu walizozijua wao na sisi kujua kupitia historia.
Kwa hiyo wizara ilirithi sheria kandamizi na ya kibaguzi na bado ikataka kutumia bila busara kwa kutaka kuipotosha umma wa Watanzania, kulipotosha Bunge na Mamlaka ya Juu ya Nchi.
Maswali yangu hapa ni:
1. Kwanini wizara ilikuja na proposala ya kibaguzi bungeni? 67% ya mapori yaliyopendekezwa yalikuwa yanakwenda kuathiri jamii inayoishi katika maeneo yanayoelekeana kiuchumi na pia mapori hayo yakiwa yameungana kijiografia. Ule uaminifu kwa Jmahuri ya Muungano ulienda wapi kwa Maafisa wa Ngazi ya Juu katika Wizara ya Maliasili na Utalii?
2. Kwanini Mamlaka ya Wanyamapori yaani TAWA ilitaka kuidanganya wizara? Uaminifu wa Mtendaji Mkuu na Bodi ya Wakurugenzi ulienda wapi? Ulikuwa wapi? Je, waliwajibika au kuwajibishwa? Hawastahili kuwajibika au kuwajibishwa?
3. Nani yupo nyuma ya upandishaji hadhi mapori mengi kwa ndani ya msimu mmoja wa mwaka wa fedha katika maeneo yaliyoungana?
Nishukuru kwamba Waziri Mkuu alisitisha mapendekezo hayo kwa kuwaeleza wahusika matakwa ya kisheria kabla ya kupandisha hadhi mapori tengefu.
Lakini:
1. Je, sisi tutaoishi maeneo hayo, tuna uhakika wa mustakabali wetu kama sheria za kikoloni zitaendelea kutumika?
2. Je, hakuna haja ya kufuta baadhi ya mapori tengefu na kuruhusu wananchi kuishi kwa uhakika wa kesho?
3. Kama kufuta, haiawezekani, hakuna haja ya kupunguza ukubwa na kuchora mipaka kwa upya ili tunaoishi maeneo hayo tujue pa kuishia katika kufanya shughuli zetu za mandeleo?
4. Je, hakuna haja ya kuangalia uwiano wa kijiografia katika kutenga maeneo ya kuyahifadhi katika nchi yetu? Kwanini sisi mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro tuumizwe na uhifadhi? Kwanini tubebe mzigo wa uhifadhi wa nchi hii?
5. Je, tuna haja ya kuwa na mapori tengefu wakati tuna mapori ya akiba na hifadhi za Taifa? Na bado tuna maeneo yaliyohifadhiwa na TFS kwa ajili ya misitu.
6. Hilo katazo la Waziri Mkuu wakati akiahirisha Bunge la Bajeti, litadumu kwa muda gani?
7. Je, Kwanini tunaendelea kuanzisha vijiji katika mapori hayo? hali inayosababisha Wanakijiji kutumia rasilimali zao kuanzisha makazi, kulima, kufuga wakati uhakika wa kesho hakuna?
Karibuni kwa mjadala.