Sheria ya miaka 30 kwa bangi na mirungi ipitiwe upya

Sheria ya miaka 30 kwa bangi na mirungi ipitiwe upya

Labyrinth 84

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2017
Posts
1,514
Reaction score
4,531
Hii Sheria ya mtu amekutwa na bangi au mirungi na kupigwa mvua ya miaka 30 naona kama haifai kabisa.
Sheria hii imekua mwiba kwa vijana sana , kijana wa miaka kuanzia 18 mpaka 39 unampa hukumu ya miaka 30 jela hapo unakua unamfunza au kumkomoa?

Stage ya ujana inaaminika ni hatua ya mtu kufanya mambo mengi sahihi na mengine makosa ni hatua ya kujifunza kutokana na makosa ndio maana kuna msemo anapokosea kijana wanasema " akikua ataacha huyu Bado kijana"

Unakuta kijana kapewa gunia la mirungi alisafirishe anapewa hata laki 8 tu kutokana na kutojua au tamaa za ujanani anajikuta kazama kwenye nondo miaka 30 kutoka ni miaka ya uzee 50 huko.

Jela ni sehemu ya mafunzo na marekebisho haswa kwa vijana ila hii ya miaka 30 ni kumkomoa kijana , adhabu inapaswa isizidii miaka 5 kwa vijana hapo anakua amejifunza ila hili la miaka 30 si kujifunza ni kupoteza muelekeo na maisha ya vijana.

Hii ni kwa mirungi na bangi ambapo sehemu nyingine kama Kenya mirungi ni zao la biashara sasa inakuwa vipi huku kwetu Sheria ya miaka 30 ?
 
Bangi imeshakuwa ni zao la biashara, hata majirani wametuacha mbali

1786230434625.png

1786230549115.png
 
Hizi Sheria sijui nan kapitisha yaani mvua 30 kwa kukutwa na bangi, huku mafisadi yakiwa nje yametulia tu
Ni uonezi tu wala sio haki
Leo duniani wanatumia kama dawa
Wenye Parkinson diseases wanapata nafuu pindi wanapotumia, hata wenye kifafa wanapata nafuu sana wakitumia mafuta ya bangi.
Biashara ya Bangi ni nchi nyingi zinafanya na wengine wameamua kukubali
Ni kifungo kikubwa sana hicho na hakina maana kabisa
 
Back
Top Bottom