wana jf naomba kufahamu kama mtu mwenye umri uliozidi miaka 18 na ni mtoto wa nje ya ndoa ana haki ya kurithi mali za marehemu babake ikiwa babake hakuwahi kumthibitisha kuwa ni mtoto wake na alishathibitisha kwa mandishi kuwa mali zake fulani warithi watoto wake wa ndani ya ndoa ambao ni wadogo na wanaxoma? je kama ana haki ya kurithi ni pasu kwa pasu na mke wa marehemu au kwa kiasi anapaswa kupata huo urithi?plz ndugu zangu naomba mxada wenu.
MIRATHI & MFANO WA KUANDIKA WOSIA.
Imeandaliwa na:
Utti. A.Mwangamba:
Centre for Widows and Children Assistance (CWCA)
S.L.P. 60202, Simu: 0754 693892 or 0787 088513
Barua pepe : childrenwidows@yahoo.co.in or widows.children@gmail.com
Dar es Salaam,
Tanzania.
East Africa
1.0. Mirathi nini?
Ni taratibu mbalimbali za kisheria zinazoongoza uangalizi , usimamizi , umiliki na hatimaye ugawaji wa mali na pengine hata kumaliza madeni ya marehemu pamoja na mazishi.
1.1. Aina za mirathi.
a) Mirathi palipo na wosia .
b) Mirathi pasipo wosia.
2.0. Sheria za mirathi itumikayo Tanzania imegawanyika katika sehemu tatu:-
i) Sheria ya Urithi ya India1865.
ii) Sheria ya Kiislamu.
iii) Sheria ya Kimila.
i)Sheria ya urithi ya India ya 1865 :- Hii ni sheria ya kiserikali na inatumika pale ambapo itaonekana kwamba marehemu alikuwa hafuati sheria za kislamu wala taratibu za kimila na desturi. Na hutumiwa na watu ambao si waislamu , pamoja na watu wengine ambao si wazawa wala waislamu
Warithi katika sheria hii :-
Ø Mke/mume wa marehemu.
Ø Watoto.
Ø Wazazi, kaka na dada za marehemu.
Mgawanyo wa mali kwa mujibu wa Sheria ya Urithi ya India:-
Ø Kama marehemu ameacha mjane na watoto watapata kama ifuatavyo; mjane1/3 na watoto 2/3 ya mali yote ya marehemu ambayo hugawiwa sawasawa.
Ø Kama marehemu hakaucha watoto , mjane atapata ½ na ½ nyingine hugawanywa sawasawa kati ya wazazi , kaka na dada za marehemu.
Zingatia: Kwa mujibu wa sheria hii watoto wa nje ya ndoa hawana haki ya kurithi isipokuwa kama kuna wosia na katika wosia huo wawe wamerithishwa mali.
ii)
Sheria ya kiislamu
Hii hutumika kwa wafuasi/waumini wa dini ya kislamu.
Warithi katika sheria hii:-
Ø Mjane.
Ø Watoto.
Ø Wazazi, kaka na dada za marehemu.
Mgawanyo wa mali kwa mujibu wa Sheria ya Kiislamu :-
Ø Mjane /wajane 1/8 ya mali ya marehemu kama marehemu ameacha watoto. Kama hakuacha watoto wajane watapata ¼ ya mali iliyoachwa na marehemu.
Ø Watoto wa kiume 2/3.
Ø Watoto wa kike 1/3.
Ø Wazazi / ndugu 1/6
Zingatia:
Ø Mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa hana haki ya kurithi mali isipokuwa kama kuna wosia.
Ø Pia kwa mujibu wa sheria hii muislamu haruhusiwi kuwosia mali yake yote , anaweza kuwosia 1/3 tu ya mali yake na 2/3 ni lazima igawanywe kwa warithi halali kufuatana na sheria ya kiislamu.
ii)
Sheria ya kimila
Hii hutumika pale ambapo marehemu aliishi kwa kufuata mila na desturi za kabila lake.
Warithi katika sheria hii:-
Ø Watoto
Ø Kama marehemu hakuacha watoto mali yake itarithiwa na baba , mama , kaka ,dada ,wajomba na shangazi zake.
Mgawanyo wa mali kwa mujibu wa Sheria ya Kimila :-
Urithi katika sheria za mirathi ya kimila umepangwa katika madaraja matatu.
Ø Daraja la Kwanza : Mtoto wa kwanza wa kiume wa nyumba hupata sehemu kubwa ya mali ya marehemu
Ø Daraja la Plil: watoto wa kiume waliosalia na mwisho
Ø Daraja la Tatu : watoto wa kike ambao hupata kiasi kidogo.
Ø Kwa mujibu wa sheria hii , wajane hawana haki ya kurithi , mjane mwenye watoto sheria inampa haki ya kuishi na kutegemea watoto wake ambao watarithi mali ya marehemu mume wake.
Zingatia:
Ø Watoto wa nje ya ndoa hawaruhusiwi kurithi mali /chochote isipokuwa kama walihalalishwa na marehemu baba yao kufuatana na mila za kabila husika.
Ø Mjane ambaye hana watoto atabaki katika nyumba ya marehemu na kuitumia wakati wa uhai wake , ambapo baada ya kifo chake hugawiwa kwa warithi halali wa mume wake.
3.0. WAJIBU WA MSIMAMIZI WA MIRATHI.
Ø Ndani ya miezi 6 baada ya kuteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi , msimamizi anawajibika kutoa orodha na kiasi cha mali alizoacha marehemu, fedha taslimu, madeni pamoja na idadi ya marehemu anaotegemea kuwagawia mali za marehemu.
Ø Kukusanya kwa uaminifu mali za marehemu.
Ø Kuorodhesha madeni yalioachwa na marehemu pamoja na kuyalipa madeni hayo toka kwenye mali alizoacha.
Ø Kulipa gharama za mazishi na gharama za kuendesha mirathi toka kwenye mali za marehemu.
Ø Kugawa mali za marehemu kwa warithi halali kama marehemu atakuwa ameacha wosia msimamizi atagawa kufuatana na wosia aliondika marehemu na kama hakuna wosia atagawa kulinganba na sheria inayotumika kwenye mirtahi9sheria ya kimila, kiislamu, au sheria ya mirtahi ya India.
Ø Kushtaki ambapo marehemu angeshtaki ili kudai haki zake au kujibu mashitaka ya madai pale ambapo kutakuwepo na madai dhidi ya msimamizi.
Ø Kusikiliza maelezo yanayotolewa na mahakama kuhusiana na mirathi anayoendesha.
Ø Kutoa taarifa mahakamani inayoeleza alivyoendesha mirathi na kugawa mali kwa warithi wa marehemu na hatimaye mirathi kufungwa.
WOSIA.
Maana ya Wosia:
Ni tamko au maandishi anayotoa mtu wakati wa uhai wake kueleza jinsi atakavyotaka mwili wake utendewe na mali zake zigawanywe atakapokuwa amefariki.
Umuhimu wa kuandika wosia.
Ø Unaweka mambo yako bayana kuondoa utata kwa familia na jamaa zako.
Ø Unamchagua msimamizi wa mirathi unayemtaka wewe.
Ø Unatoa maelezo juu ya mwili na mali yako kama upendavyo wewe na kwa mujibu wa sheria.
Aina za wosia:-
Ø Wosia wa maandishi.
Ø Wosia wa maneno ya mdomo/matamshi.
Taratibu za kuandika wosia katika sheria za mirathi .
a) Wosia katika Sheria za kimila: Zimo katika jedwali la 3 la sheria iitwayo: The Local Customary Law (Declaration) No. 4 Order, 1963.
b) Wosia katika sheria za kiserikali.
c) Wosia katika sheria za kiislamu Mwosia hawezi kuusia mali yake yote. Kisheria anaruhusiwa kuusia 1/3 ya mali yake. 2/3 lazima irithiwe na warithi halali.
Warithi halali ni nani kisheria?
Ø Mke/ mume.
Ø Watoto waliozaliwa ndani ya ndoa.
Ø Watoto waliohalalishwa kisheria.
Ø Wazazi nandugu wa karibu waliokuwa wakimtegemea mtoa wosia wakati wa uhai wake.
Masharti ya uandishi wa Wosia wa maandishi.
Ø Mwosia lazima awe na akili timamu.
Ø Awe ametimiza umri wa miaka 18 na kuendelea.
Ø Uonyeshe tarehe, mwezi na mwaka uliondikwa.
Ø Mwosia ahusiye mali zake binafsi na si za mtu mwingine.
Ø Ushuhudiwe na mashahidi wawili, na kwa yule asiyejua kusoma na kuandika wake lazima wawe wanne na wajue kusoma na kuandika.
Ø Mwosia lazima aweke saini yake, na kama hajui kusoma na kaundika aweke alama ya dole gumba.
Ø Uandikwe kwa kalamu ya wino au kalamu isiyofutika au upigwe chapa.
Ø Mwosia ataje mtu/watu ambao angependa asimamie ugawajki wa mali baada ya kifo chake.
Sifa /masharti ya wosia wa maneno ya mdomo.
Ø Awe mtu ambaye ametimiza umri wa miaka 18 na kuendelea na mwenye akili timamu.
Ø Ushudiwe na mashahidi wasiopungua wanne. Watu wawili kati ya mashahidi hao wawe ni wa ukoo wa mwosia, na wawili wanaweza kuwa watu baki nje ya ukoo wa mwosia.
Kumbuka:
1. Mwosia hawezi kumnyima mrithi wake mali zake isipokuwa tu kama mrithi amefanya mambo yafuatayo :-
Ø Kama amezini na mke na mwosia.
Ø Kama mrithi amejaribu kumuua , kumshambulia , au kumdhuru vibaya mwosia (au kumtendea mama wa mwosia mambo yaliyotajwa )
Ø Mrithi bila sababu na hakumtunza mwosia wakati wa shida na njaa au maradhi.
2. Mtu anaweza kumrithisha rafiki yake vitu au vyombo vyake alivyokuwa akivitumia mwenyewe au sehemu ya mali yake . Lakini fungu la rafiki lisizidi la kila mrithi halali.
3. Wosia ni siri hufichuka wakati mtu aliyeutoa anapokuwa amefariki.
4. Anayeweza kuandika / kutoa wosia wa mdomo ni mtu aliyetimiza umri wa miaka 18 na awe na akili timamu.
Mahali pakutunzia wosia : Benki , kanisani au msikitini , kwa mwanasheria , kwa mtu yeyote ambaye si mrithi katika wosi huo na anaaminika kuwa ana uwezo wa kutuza siri. n.k.
MFANO WA JINSI YA KUANDIKA WOSIA.
- Huu ni wosia wangu wa mwisho mimi
wa S.L.P
- Namchagua
.
wa S.L.P.
.
Simu
ambaye anaishi
.kuwa msimamizi wa mirathi yangu.
- Nitakapokufa mwili wangu ukazikwe
..
Wilaya
Mkoa
...
- Mali yangu ni:
(a)
..
(b) Nina akaunti zifuatazo:
.
5. Natamka kwmaba mali zangu zote zinazohamishika na zisizohamishika zitamilikiwa
na mke/ mume wangu aitwaye
iwapo atakuwa hao baadaya kufa kwangu.
6. Iwapo mke/ mume wangu aitwaye
..atafariki mapema kuliko mimi , mali zangu zitarithiwa na watoto wangu wafuatao:-
(a)
.
S.L.P
Simu
(b)
S.L.P
Simu
..
(c)
.
S.L.P
Simu
..
(d)
S.L.P
.
Simu
.
Katika mafungu yaliyo sawasawa .
Imetiwa saini hapa
.
Siku ya
Mwezi wa
mwaka
Saini ya mwosia
Shahidi wa Kwanza:
Jina:
.
Saini:
Anuani:
Kazi
..
Shahidi wa Pili :
Jina:
.
Saini:
Anuani:
Kazi
..
Mbele ya
...
Mshuhudi viapo/Saini:
ANGALIZO: Kuandika wosia si uchoro , bali ni kujizatiti katika kuhakikisha mambo yako yanakuwa sawa hata usipokuwepo , ukiwa ni mmojawopo wa wanajamii chukua hatua ya kuandika wosia na uwashawishi wengine kufanya hivyo
Mwisho.
View attachment mirathi_wosia.doc