wana jf naomba kufahamu kama mtu mwenye umri uliozidi miaka 18 na ni mtoto wa nje ya ndoa ana haki ya kurithi mali za marehemu babake ikiwa babake hakuwahi kumthibitisha kuwa ni mtoto wake na alishathibitisha kwa mandishi kuwa mali zake fulani warithi watoto wake wa ndani ya ndoa ambao ni wadogo na wanaxoma? je kama ana haki ya kurithi ni pasu kwa pasu na mke wa marehemu au kwa kiasi anapaswa kupata huo urithi?plz ndugu zangu naomba mxada wenu.
ndugu, mtoto wa nje ya ndoa, kwa sheria ya kimila, kiserikali na kiislam hana haki ya moja kwa moja kurithi mirathi ya baba yake, ila anaweza kurithi mirathi ya mama yake tu..hasa pale ambapo hajahalalisha.
anaweza kurithi endapo baba yake alimhalalisha (alimthibitisha na kumtambulisha kwa ndugu either kumkomboa kimila kwa kulipa pesa etc njia zipo nyingi). kama alihalalishwa, anatakiwa kupata mafungu sawasawa na warithi wale wengine halali yaani watoto wa marehemu etc. kama hakuhalalishwa hatakiwi kupata chochote.
jambo la mwisho, mtoto wa nje ya ndoa, kama baba hakumhalalisha kabla ya kufa, anaweza kurithi kama ameandikwa kwenye wosia. mtu unaweza kuandika mtu yeyote arithi mali zako kwa kupitia wosia. na mtu akarithi pamoja na warithi wako halali, lakini , mtoto huyu ambaye hajahalalishwa atarithi kama mtu baki na si kama mrithi halali. kwasababu anarithi kama mtu baki, hatakiwi kupata fungu kubwa kuzidi warithi halali. hiyo ndiyo sheria ya wosia.
that means, kama baba yako hakukuhalalisha, na hakukuwekea kafungu kokote kwenye wosia ili urithi kama mtu baki, hautarithi chochote hapo. hautambuliki. kwa maana hiyo, kama wewe haukuhalalishwa na marehemu baba yako, na marehemu baba yako aliandika wosia akagawa mali kwa warithi halali tu wewe hakukugawia kwenye wosia, hautapata chochote hata ukienda mahakama zote tz hadi court of appeal. hauna haki yeyote hapo. MKOMBOZI WA WATOTO WA KAMBO AMBAO HAWAJAHALALISHWA NI WOSIA TU. kama wosia haupo, hakuna atakachopata.
zaidi ya yote, katika mirathi ya kiislam, mtoto wa nje ya ndoa ni haram, hatakiwi kurithi kabisa mirathi ya baba, ila ya mama atarithi. lakini, akiandikiwa wosia kama mtu baki na kama toto huyo ni muislam, basi anaweza kurithi lakini hata hivyo, kwenye wosia huo isizidi 1/3 ya mali zote, ukizidisha hapo watatakiwa warithi halali waridhie kwanza. wasiporidhia imekula kwako. kumbuka kwa waislam hakuna kuhalalisha mtoto wa kambo, hahalalishiki. vilevile, kafiri hamrithi mwislam na mwislam vilevile hamrithi kafiri hata kama wako close namna gani.
USHAURI: KAMA UNA MTOTO WA KAMBO, kamhalalisha mapema kama unampenda.