sheria ya mirathi msaada please

sheria ya mirathi msaada please

Presumptions: As long as the the child was begotten during the subsistence of the marriage ie the spouses were co-cohabiting together the issues of their marriage are presumed to belong to the husband until it is disproved. Mama anaweza akasema kuwa mtoto huyu si wa mume wangu. But that would be a very contentious case!!! Otherwise watoto ni wa ndoa yenu, wanasheria wanasemaje!

Presumption: a belief that something is true even though it has not been proved.

SMH!
 
Katika mafao ya pensheni kwa sheria ya PSPF mtoto wa nje ya ndoa anahaki kama watoto wengine, natarajia una cheti cha kuzaliwa kinachomtaja babako ni huyo marehemu na mamako anaweza kuthibitisha hivyo

Hii basi haitakuwa sahihi. Maana kujiunga na pensheni kuna fomu mfanyakazi au mwanachama wa hiari anajaza. Je, mfuko wa pensheni unaweza kumtambua mtu ambae hajaorodheshwa? Na ndo maana kuna utaratibu wa ku-update taarifa na hii mifuko. Basi wengi watakuwa wanadhulumiwa na wengine kufaidi pasipostahili.

Kwa mfano mtoto wa nje akatambulika maana marehemu ni baba mzazi (kaleta uthibitisho wa cheti cha kuzaliwa), na tena upande wa pili mamake kaolewa na step father tena akamchukua huyo mtoto kama wa kwake.
 
SHERIA YA USIMAMIZI WA MIRATHI SURA YA 352 YA SHERIA ZA TANZANIA

1. SHERIA HII INASHUGHULIKA NA MAMBO YAPI NA INA LENGO GANI HASA?

Lengo kuu la sheria hii ni kutoa utaratibu wa kusimamia mali za marehemu baada ya kifo chake ikiwamo kuhamisha umiliki wa mali hizo kutoka kwa marehemu kwenda kwa watu wenye haki ya kuzipata mali hizo.Nia hasa ni kwamba mali alizoacha marehemu zisibaki zikiharibika na kupotea bure,au warithi halali au watu wenye maslahi na mali za marehemu,kwa mfano wale wanaomdai hawapotezi haki hiyo, bali awepo mtu ambaye atazisimamia na kuzigawa kwa wahusika wakiwamo wadai na kuepusha mgongano katika jamii husika.Hivyo sheria inamuweka msimamizi wa kugawa mirathi husika na mamlaka yake.

TANZANIA LAW AND ORDER: SHERIA YA MIRATHI YA TANZANIA
 
Masharti ya uandishi wa Wosia wa maandishi.

Ø Mwosia lazima awe na akili timamu.
Ø Awe ametimiza umri wa miaka 18 na kuendelea.

Je mtu wa miaka zaidi ya 90 anaweza kutambulika kama mwenue akili timamu kati kuandika wosia?
 
kwa m2 mwenye miaka 90 anaweza kuandika wosia as long as, kwa ule muda anaoandika will yake,anajua anachokifanya, back to yo topic mpendwa, kama mzee wako hakukutambulisha, ipo ishu, la kwanza binafsi cjafaham kua umebase kwenye dini gani bt la pili ni kujua kilicho maanishwa kwenye will ilioachwa na mzee pia DNA TEST ni muhim as evidencea, bt ol in
ol kama mkibase kwa sheria za kiislam itakula kwako mpk pale watakapoamua wenyewe kukufikiria
 
Sheria inasemaje ikiwa mtoa wosia hakuwataja kwenye wosia wake baadhi ya warithi ambao kimsingi wanastahili kurithi mfano watoto? je,sheria inasemaje ikiwa mtoa wosia hakuzitaja baadhi ya mali zake kwenye wosia wake? kwenye mazingira kama haya huwezi kwenda mahakamani?
Nijuavyo mimi kama kuna wosia wa maandishi basi huo huwa haupingwi wala kukiukwa kwa sababu hivyo ndivyo marehemu alivyotaka.

Na mahakama inatakiwa ifuate jinsi ambavyo wosia unasema.

Nimetoka kudili na haya mambo majuzi tu hapa. Hivyo najua walau mawili matatu kuhusiana na haya mambo ya mirathi.
 
Watoto wangu ni wangu tu,
Wawe wamezaliwa ndani, nje au katikati ya ndoa, ni wangu tu.

Mfano nina watoto wawili ambao nimewapata before ndoa, maisha yangu ni mazuri tu, najiweza kwa kila kitu na labda nitakapo kuja kufikiria kuoa miaka ijayo, mdada atakuja kukuta nimejikamilisha kwa kila kitu. Akija nkapata nae mtoto mwengine ndani ya ndoa, Upon my death hawa wa kwanza hawana haki??

There's a big difference between RIGHT & JUSTICE, so those kids will be having the RIGHT to inherent but unfortunately it can't be JUSTIFIED due to some technicalities!

Actually based on the nowadays life style we really need to revisit and amend some stuffs in the whole thing concerning inheritance issues, SPECIFICALLY the legal meaning of the term CHILD....
 
katika sheria ya mirathi kuna vitu viwili vya muhimu kama marehemu hakuacha maandishi/wosia navyo ni
  1. intention of deceased person.
  2. mode of life of deceased person.
vitu hivi vitatoa majibu ya kutambua ni sheria gani itumike, kama ni muislamu itatumika sheria ya kiislamu na kama ni mtu wa mila za kwao basi sheria za kimila zitachukua nafasi, na ikioneekana marehemu alikuwa mkristu au hana dini lakini siyo mtu wa mila basi sheria ya bunge itatumika, na sheria yenyewe ni Indian Succession Act, 1865. na kwa upande wa sheria za Kiislamu mtoto wa nje ya ndoa hana haki ya kurithi kwa baba na wala baba hana haki ya kumrithi mtoto wake, sheria za bunge wameshakuelezea hapo juu na kuhusu sheria za mila nayo ni kama sheria za kiislamu kwa mazingira ya kesi yako.
 
wana jf naomba kufahamu kama mtu mwenye umri uliozidi miaka 18 na ni mtoto wa nje ya ndoa ana haki ya kurithi mali za marehemu babake ikiwa babake hakuwahi kumthibitisha kuwa ni mtoto wake na alishathibitisha kwa mandishi kuwa mali zake fulani warithi watoto wake wa ndani ya ndoa ambao ni wadogo na wanaxoma? je kama ana haki ya kurithi ni pasu kwa pasu na mke wa marehemu au kwa kiasi anapaswa kupata huo urithi?plz ndugu zangu naomba mxada wenu.

Sasa mkuu apo kiswahili kina ugumu gani? Ameshase specify tayari nani apewe mali katika wasia, na ushasema kuwa mtoto huyo mwengine wa nje ya ndoa, vipi tena atapata share wakati marehemi kashataja kuwa wa ndani ya ndoa ndio wapate share? Uzuri ni kwamba huyo marehemu ameshataja hasa mali iende kwa nani, sasa ata kuchallenge sifikiri kama mtoto wa nje ya ndoa anawesa landa aombe tu!
 
Nenda ukapate msaada wakisheria.. Its obvious kunaela imetembea hapo. So nenda wlac ipo kinondoni au tawla ipo ilala. Wanatoa msaada wakisheria bure.
 
wana jf naomba kufahamu kama mtu mwenye umri uliozidi miaka 18 na ni mtoto wa nje ya ndoa ana haki ya kurithi mali za marehemu babake ikiwa babake hakuwahi kumthibitisha kuwa ni mtoto wake na alishathibitisha kwa mandishi kuwa mali zake fulani warithi watoto wake wa ndani ya ndoa ambao ni wadogo na wanaxoma? je kama ana haki ya kurithi ni pasu kwa pasu na mke wa marehemu au kwa kiasi anapaswa kupata huo urithi?plz ndugu zangu naomba mxada wenu.
ndugu, mtoto wa nje ya ndoa, kwa sheria ya kimila, kiserikali na kiislam hana haki ya moja kwa moja kurithi mirathi ya baba yake, ila anaweza kurithi mirathi ya mama yake tu..hasa pale ambapo hajahalalisha.

anaweza kurithi endapo baba yake alimhalalisha (alimthibitisha na kumtambulisha kwa ndugu either kumkomboa kimila kwa kulipa pesa etc njia zipo nyingi). kama alihalalishwa, anatakiwa kupata mafungu sawasawa na warithi wale wengine halali yaani watoto wa marehemu etc. kama hakuhalalishwa hatakiwi kupata chochote.

jambo la mwisho, mtoto wa nje ya ndoa, kama baba hakumhalalisha kabla ya kufa, anaweza kurithi kama ameandikwa kwenye wosia. mtu unaweza kuandika mtu yeyote arithi mali zako kwa kupitia wosia. na mtu akarithi pamoja na warithi wako halali, lakini , mtoto huyu ambaye hajahalalishwa atarithi kama mtu baki na si kama mrithi halali. kwasababu anarithi kama mtu baki, hatakiwi kupata fungu kubwa kuzidi warithi halali. hiyo ndiyo sheria ya wosia.

that means, kama baba yako hakukuhalalisha, na hakukuwekea kafungu kokote kwenye wosia ili urithi kama mtu baki, hautarithi chochote hapo. hautambuliki. kwa maana hiyo, kama wewe haukuhalalishwa na marehemu baba yako, na marehemu baba yako aliandika wosia akagawa mali kwa warithi halali tu wewe hakukugawia kwenye wosia, hautapata chochote hata ukienda mahakama zote tz hadi court of appeal. hauna haki yeyote hapo. MKOMBOZI WA WATOTO WA KAMBO AMBAO HAWAJAHALALISHWA NI WOSIA TU. kama wosia haupo, hakuna atakachopata.

zaidi ya yote, katika mirathi ya kiislam, mtoto wa nje ya ndoa ni haram, hatakiwi kurithi kabisa mirathi ya baba, ila ya mama atarithi. lakini, akiandikiwa wosia kama mtu baki na kama toto huyo ni muislam, basi anaweza kurithi lakini hata hivyo, kwenye wosia huo isizidi 1/3 ya mali zote, ukizidisha hapo watatakiwa warithi halali waridhie kwanza. wasiporidhia imekula kwako. kumbuka kwa waislam hakuna kuhalalisha mtoto wa kambo, hahalalishiki. vilevile, kafiri hamrithi mwislam na mwislam vilevile hamrithi kafiri hata kama wako close namna gani.

USHAURI: KAMA UNA MTOTO WA KAMBO, kamhalalisha mapema kama unampenda.
 
Sasa mkuu apo kiswahili kina ugumu gani? Ameshase specify tayari nani apewe mali katika wasia, na ushasema kuwa mtoto huyo mwengine wa nje ya ndoa, vipi tena atapata share wakati marehemi kashataja kuwa wa ndani ya ndoa ndio wapate share? Uzuri ni kwamba huyo marehemu ameshataja hasa mali iende kwa nani, sasa ata kuchallenge sifikiri kama mtoto wa nje ya ndoa anawesa landa aombe tu!
unachotakiwa kuelewa ni kwamba, wakati mwingine wosia unaweza kuwa batili au ukabatilishwa. kama una haki kurithi kwenye mirathi, na marehemu bila sababu ya msingi amekunyima kwenye wosia, you can challenge it ili wosia huo upigwe chini na mahakama iamue namna nyingine ya kugawa mirathi hiyo bila kufuata wosia huo.
 
Mkuu Justine kimbunga

Katika hali ya kawaida wosia wa marehemu hauwezi kupuuzwa isipokuwa unaweza kubadilishwa ikiwa hautakuwa na sifa za wosia.

Kwa mfano wakati Baba yako anaandika wosia halafu witness akawafanya ni wewe na mdogo wako ambao mnafaidika moja kwa moja na wosia wenye sheria inasema wosia utasimama kama ulivyo lakini nyinyi witness mnaondolewa uhalali wa kumiliki vitu mlivyoachiwa.Sasa sijui argument wanayotumia hao ndugu zenu ni kipengele cha wewe,mdogo wako na Mama yako mnakuwa witness wakati wosia unaandikwa na wakati huo huo wosia huo unawafaidisha nyinyi labda ungefunguka kidogo ningeweza kukusaidia nini cha kufanya.
 
Last edited by a moderator:
wana jf naomba kufahamu kama mtu mwenye umri uliozidi miaka 18 na ni mtoto wa nje ya ndoa ana haki ya kurithi mali za marehemu babake ikiwa babake hakuwahi kumthibitisha kuwa ni mtoto wake na alishathibitisha kwa mandishi kuwa mali zake fulani warithi watoto wake wa ndani ya ndoa ambao ni wadogo na wanaxoma? je kama ana haki ya kurithi ni pasu kwa pasu na mke wa marehemu au kwa kiasi anapaswa kupata huo urithi?plz ndugu zangu naomba mxada wenu.

Mtoto aliezaliwa nje ya ndoa hana haki yoyote ya kurithi hata kama ni kweli ni mtoto wa damu (DNA) hana haki ndani ya ndoa kwa mujibu wa sheria za Jamhuri. hana haki unless mzazi wa mtoto huyo amuombe mwana ndoa mwenzake
ili kwamba huyo mtoto aingizwe katika ndoa hiyo kwa kutambuliwa kwa maridhiano kisheria na akathibitishwa mahakamani kwamba ameingizwa rasmi kuwa sehemu ya familia hiyo kwa mujibu wa sheria na hati zikatolewa . kinyume cha hapo hana mgao wowote hata chembe kisheria
 
What? Mahakama wana mamlaka gani ya kumwambia hakuwa sahihi kugawa mali zake kama apendavyo?

Mahakama za ki'senge bana! Shida tupu! Mali azichume mwenyewe kwa jasho lake halafu mijitu ije impangie kuzigawa? Stupid.
jkama alishagawa na kuna hati kabla hata hajafa, izo alikuwa anawapa watu zawadi zake, na hivyo si mali zake tena, hizo si mali za marehemu ni mali za waliopewa zawadi, hivyo hazitakiwi kabisa kuorodheshwa kwenye orodha ya mali za marehemu zinazotakiwa kugawanywa katika mirathi. mahakama hiyo ilikosea sana, na kama hao walioporwa zawadi alizowapa marehemu watakata rufaa, uamuzi huo utatupiliwa mbali. si lazima kila kitu kigawanywe kwenye wosia. wakati marehemu yupo hai, anaweza kugawa mali zake apendavyo. kwa mali zile zinazobaki anaweza kuamua kuziandikia wosia wa nani apate siku atakapokufa. akishatoa zawadi imetoka, inakuwa si yake tena, ni ya yule mzawadiwa.
 
Back
Top Bottom