Sheria ya Uchaguzi ibadilishwe kuruhusu Wagombea kwenda Mahakamani kupinga maamuzi ya NEC na zaidi mchakato wa kupatikana Wagombea uanze mwaka mmoja

Sheria ya Uchaguzi ibadilishwe kuruhusu Wagombea kwenda Mahakamani kupinga maamuzi ya NEC na zaidi mchakato wa kupatikana Wagombea uanze mwaka mmoja

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Kwa yanayoendelea sasa kuhusu kesi za uchaguzi na malalamiko mengine yanayohusiana na uchaguzi hasa kuhusu wagombea kuenguliwa,ni matokeo ya kuwa na sheria mbovu ya uchaguzi inayotoa mwanya wa wagombea kupita bila kupingwa huku Tume ya Uchaguzi ikiwa ndio alpha na omega katika kuamua nani agombee na nani asigombee.

Dawa ni kubadil sheria ya uchaguzi na kanuni zake kwa lengo la kuondoa vipengele vinavyohalalisha mgombea kuenguliwa kwa kufanya makosa madogomadogo kwenye ujazi wa fomu za uchaguzi .

Dawa nyingine ni kubadili sheria na kuruhusu wagombea kwenda mahakamani kupinga maamuzi ya wasimamizi wa uchaguzi na yale ya Tume ya Uchaguzi iwapo mgombea hatoridhika na maamuzi ya Tume.

Ili kuwe na muda wa kutisha wa haya kufanyika,inatakiwa mchakato wa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi zianze mwaka mmoja kabla ya tarehe ya uchaguzi ili kuruhusu wagombea kupata nafasi ya kwenda mahakamani kufungua kesi za kupinga kuenguliwa iwe na Tume ya Uchaguzi au na vikao husika vya vyama vya siasa vinavyokata majina ya walioshinda kura za maoni huku maamuzi hayo yakiwa hayahojiwi popote jambo ambapo ni kinyume kabisa na katiba ya nchi.

Kinachofanywa na Tume ya Uchaguzi na wasimamizi wa uchaguzi katika maeneo yao, ni sawa na kinachofanywa na vyama vya siasa pale vinapoengua walioshinda kura za maoni huku vyama vikiwa havilazimiki kutoa sababu za kukata majina huku maamuzi hayo akiwaonya ni ya mwisho(hayahojiwi popote)

Hata kama kesi zitakuwa ni nyingi lakini ni Bora kuliko huu ujinga na uonevu unaondelea sasa.
 
Back
Top Bottom