Makirita Amani
JF-Expert Member
- Jun 6, 2012
- 1,915
- 3,422
Rafiki yangu mpendwa, linapokuja kwenye fedha, kila mtu anajua umuhimu wake.
Na umuhimu wa fedha siyo kwa sababu ni fedha, bali kwa sababu ya matumizi yake.
Fedha ni muhimu kwa sababu inatuwezesha kupata mambo muhimu ya maisha yetu.
Na fedha ndiyo kitu ambacho kinawagusa watu wote.
Fedha haina ubaguzi, watu wanaweza kukubagua kwa dini yako, rangi yako, kabila lako, lakini hawataibagua fedha yako.
Kila mahali watu wamegawanyika kwenye makundi mawili,
Kuna kundi la watu matajiri, ambao wana uwezo mkubwa wa kifedha.
Na kuna kundi la watu masikini, ambao hawana uwezo wa kifedha.
Watu hao huwa hawatofautiani sana kwa nje, wote wanakuwa eneo moja, wakifanya shughuli zinazofanana, lakini kwenye fedha wanatofautiana.
Tofauti za watu matajiri na masikini zinaanzia ndani yao, kuna namna matajiri wanafikiri na kufanya ambayo ni tofauti kabisa kwa masikini.
Mwandishi Richard Templar kwenye kitabu chake cha RULES OF MONEY ameshirikisha sheria za fedha ambazo watu matajiri huwa wanazifuata na zinawawezesha kutengeneza na kushikilia pesa.
Hapa tunakwenda kupata masomo yenye sheria hizo ambazo tunapaswa kuzijua na kuziishi ili tuweze kujenga utajiri kwenye maisha yetu.
Sheria za fedha zimegawanyika kwenye sehemu nne ambazo ni KUFIKIRI KITAJIRI, KUJENGA UTAJIRI, KUKUZA UTAJIRI, KUTUNZA UTAJIRI NA KUSHIRIKISHA UTAJIRI.
SEHEMU YA KWANZA; KUFIKIRI KITAJIRI.
Utajiri ni zao la fikra ambazo mtu anakuwa nazo kwa muda mrefu. Fedha huwa ni wazo tu, thamani ya fedha siyo karatasi au sarafu tunayoshika, bali ile imani tunayokuwa nayo juu ya karatasi au sarafu hiyo.
Ili uweze kujenga utajiri kwenye maisha yako, unapaswa kuanza na kufikiri kitajiri. Hapa ni sheria za kufikiri kitajiri ili kuweza kujenga utajiri.
SHERIA YA 1; Kila mtu anaweza kuwa tajiri, unapaswa kuweka juhudi.
Fedha haina ubaguzi, huwa inaenda sawa kwa watu wote. Kinachowatofautisha wanaotajirika na wanaobaki kwenye umasikini ni imani na mitazamo.
Jenga imani na mitazamo sahihi ili uweze kujenga utajiri kwenye maisha yako.
SHERIA YA 2; Amua maana ya utajiri kwako.
Kila mtu ana maana yake ya utajiri, kuiga maana ya wengine ya utajiri ni kujitesa. Amua maana ya utajiri kwako kisha ifanyie kazi.
SHERIA YA 3; Weka malengo yako.
Baada ya kuwa na maana ya utajiri, weka malengo ya jinsi unavyofikia maana hiyo ya utajiri. Malengo ni jinsi ya kufikia utajiri unaoutaka.
SHERIA YA 4; Ifanye kuwa siri yako.
Unapoamua kuwa tajiri na kuweka malengo, unaweza kusukumwa kuwaambia wengine malengo hayo. Lakini usifanye hivyo, wengi hawatakuelewa na watakukatisha tamaa. Fanya lengo lako la utajiri kuwa siri yako.
SHERIA YA 5; Watu wengi ni wavivu, hawawezi kujenga utajiri.
Kujenga utajiri kunamtaka mtu kuweka kazi kwa juhudi kubwa sana, kuamka asubuhi na mapema, kufanya kazi kwa muda mrefu na kuchelewa kulala. Wengi hawapo tayari kulipa hiyo gharama. Wewe ilipe na utapata utajiri kwa uhakika.
SHERIA YA 6; Kabaliana na uhalisia.
Safari ya kujenga utajiri ni ngumu na wewe mwenyewe una madhaifu yako ambayo yatakukwamisha. Ukijidanganya kwamba ni rahisi na itatokea tu, hutafanikiwa. Kabiliana na uhalisia wa ugumu wa safari na changamoto zako binafsi ili uweze kujenga utajiri kwa uhakika.
SHERIA YA 7; Elewa imani zako kuhusu fedha na zinatoka wapi.
Imani nyingi ulizonazo kuhusu fedha ni hasi na zinakukwamisha. Imani hizo umeiga kutoka kwa wazazi na walezi ambao nao hazijawasaidia. Kuwa tayari kuachana na imani potofu ulizonazo kuhusu fedha na kujenga imani sahihi.
SHERIA YA 8; Elewa kwamba utajiri ni matokeo na siyo zawadi.
Hakuna kamati inayokaa na kuamua kukupa utajiri kwa sababu unastahili sana. Bali utajiri ni matokeo unayopaswa kuyazalisha kwa juhudi ambazo unaweka. Weka juhudi kubwa kuzalisha matokeo makubwa.
SHERIA YA 9; Amua unataka fedha kwa ajili ya nini.
Kila mtu anataka fedha kwa sababu zake binafsi. Ndoto za kila mtu ni tofauti na hivyo hakuna jibu moja sahihi kwa wote. Anza kwa kujua ndoto zako kisha zitumie hizo kama msukumo wa kupata fedha.
SHERIA YA 10; Elewa kwamba fedha huzalisha fedha.
Fedha huwa haipendi upweke, huwa inaenda kule ambapo kuna fedha zaidi. Ndiyo maana matajiri huendelea kuwa matajiri huku masikini wakiendelea kuwa masikini. Hakikisha unatumia kila fedha unayokuwa nayo kuzalisha fedha zaidi ili utajiri ujengeke na kudumu kwako.
SHERIA YA 11; Kokotoa marejesho kamili.
Kabla hujafanya uwekezaji wa fedha zako, kokotoa marejesho kamili unayoweza kupata kwenye uwekezaji husika. Hapo ni baada ya kutoa gharama zote za kodi na tozo mbalimbali. Marejesho kamili ndiyo yatakuonyesha kama uwekezaji ni sahihi au la.
SHERIA YA 12; Kama unaona fedha kama suluhisho, itageuka kuwa tatizo.
Fedha ni zana tu ya kufanya maisha yaende, ni kilainishi cha tairi za maisha na siyo injini ya maisha. Maisha ni wewe na kuna mambo mengi kwenye maisha ambayo fedha haiwezi kuyafanya moja kwa moja, lazima uyafanye wewe kama mtu. Mfano kujenga mahusiano, kuboresha afya n.k.
SHERIA YA 13; Unaweza kuingiza fedha nyingi, huku ukifurahia kazi yako na kulala vizuri.
Wengi wana kasumba kwamba kujenga utajiri ni lazima ujitese. Siyo kweli, unaweza kujenga utajiri huku ukiyafurahia maisha yako. Unafanya hivyo kwa kufanya kile unachopenda kufanya.
SHERIA YA 14; Usipate fedha kwa kuwa mwovu.
Kasumba nyingine ni kwamba kupata fedha lazima uwaibie au kuwadhulumu wengine. Utajiri unaopatikana kwa njia hizo huwa haudumu. Jenga utajiri kwa njia za haki na utadumu.
SHERIA YA 15; Elewa uhusiano wa fedha na furaha.
Wengi husema fedha hainunui furaha, kama vile kazi ya fedha ni kununua furaha. Kazi ya fedha ni kufanya maisha yako yaweze kwenda vizuri, furaha ni kitu kingine kinachotokana na wewe kuridhika na maisha yako. Jua nafasi ya fedha na usiizidishie majukumu.
SHERIA YA 16; Jua tofauti ya bei na thamani.
Bei ni kile unacholipa, thamani ni kile unachopata. Unaponunua, angalia thamani na siyo bei. Na unapouza, toa thamani kubwa kuliko bei unayotoza.
SHERIA YA 17; Jua jinsi matajiri wanavyofikiri.
Unajifunza utajiri kutoka kwa matajiri. Na kitu muhimu cha kujifunza kwao ni jinsi wanavyofikiri. Ongea na matajiri ujue jinsi wanavyofikiri ili na wewe uweze kufikiri kwa usahihi kama wao.
SHERIA YA 18; Usiwaonee wengine wivu.
Wewe mwenyewe ndiye umechagua kufanya hivyo unachofanya sasa. Na wengine wamechagua kufanya yale wanayofanya. Kuwaonea wengine wivu kwa kutaka yale wanayopata ndiyo ungepata wewe haina maana kwako na wala haitakusaidia. Jifunze kutoka kwa wengine, lakini usiwaonee wivu.
SHERIA YA 19; Ni vigumu kujisimamia mwenyewe kuliko kusimamia fedha.
Huwa unadhani tatizo la wewe kutokuwa tajiri ni fedha. Lakini huo siyo ukweli, tatizo lako siyo fedha, tatizo lako ni wewe mwenyewe. Uvivu, uzembe, mazoea na kukata tamaa haraka ni vikwazo vikubwa kwako. Kujenga utajiri, anza kujisimamia wewe mwenyewe kwanza na fedha itakuwa rahisi kusimamia.
Hizo ndiyo sheria za sehemu ya kwanza ya kitabu, zizingatie ili uweze kujenga utajiri kwenye maisha yako.
Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani,
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi
+255 678 977 007 / amakirita@gmail.com