Mpiga Paspoti
JF-Expert Member
- Dec 29, 2022
- 309
- 1,273
Habari JF?
Siku hizi kumeibuka wimbi la kufungua Baa/ groceries na nyumba za ibada katikati ya makazi ya watu! Mwisho wa siku, zinageuka kuwa kero kwa kufungua sauti kubwa kwa wananchi wanaozizunguka ambao kimsingi hizi bar au nyumba za ibada zimewakuta hawa wanachi!
Mfano mzuri, ninapoishi nimefanya ujezi wa hii nyumba miaka tisa iliyopita, hakukuwa na bar wala nyumba ya ibada katika eneo hili na mtaa ulikuwa ni tulivu sana.
Hivi karibuni kuna bar imefunguliwa, walinunua nyumba ikavunjwa na kujengwa bar. Mie ni jirani wa pili kutoka ilipo. Jamani....!! Natamani niuze nyumba nihame tu! Kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa kumi alfajiri wao wanafungulia muziki kwa sauti ya juu kabisa! Ni kero! Ni kero haswa!! Watoto mpaka wamekonda, hawana muda wa kupumzika!! Nikiwa ndani mwangu hata simu siwezi kupokea!
Papo hapo kuna nyumba ya sita kutoka nilipo kwa upande wa pili! Jirani kafungua kanisa ambalo usiku kucha nalo wanaweka CD ya maombi kwa sauti ya juu kabisa!! Hatuna pa kupumulia!!
Mamlaka husika hebu muangalie umuhimu wa kudhibiti na kuweka sheria kali kwenye ufunguzi wa hizi huduma na biashara katikati ya makazi ya watu! Zimekuwa kero kubwa kwa sasa!