Watu wa mipango miji wao wanachojua ni kusubiri mishahara,semina,warsha,hafla na tafrija lakini suala la kufuatilia mambo ya ujenzi mtaani hawataki wakati ramani za mitaa wanazo. Kiukweli nyumba za ibada zinatakiwa zitengewe maeneo yake maalumu na ibada inahitaji utulivu,sasa unakuta mtaa una makelele ya bodaboda,baa,sherehe,yaani kero tupu. Pia sehemu za starehe zinatakiwa nazo zitengewe maeneo maalumu. Lakini haya yote yanasababishwa na wabunge na madiwani wao kwa kutowasimamia ipasavyo watendaji wa Serikali. Mwisho,siku hizi kuna SOUND PROOF kwa nini watu wasifunge ili kuzuia kelele kutoka nje..Naupongeza sana msikiti wa Taqwa Ilala Bungoni pamoja na ule wa pale karibu na Uwanja wa Uhuru,wao utasikia adhana tu kisha mambo mengine yanasikika ndani ya nyumba ya ibada tu nje huku husikii vile vipaza sauti..