Sheria za Soka za FIFA: Ifahamu Sheria namba Mbili ya FIFA inayohusu Mpira wa Soka

Sheria za Soka za FIFA: Ifahamu Sheria namba Mbili ya FIFA inayohusu Mpira wa Soka

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Kwa mujibu wa Sheria za FIFA (Shirikisho la Soka Duniani) mwaka 2015/16, mpira unatakiwa uwe wa Mviringo wenye Mzingo/Mzunguko wa Sentimita 68 hadi 70 (Mpira Namba 5), ukitengenezwa kwa ngozi au malighafi yoyote inayofaa

Mwanzo wa mechi, mpira unatakiwa uwe na uzito usiopungua Gram 410 na usiozidi Gram 450 na uwe na Mgandamizo wa hewa wa kati ya 600g/cm2 na 1,100 g/cm2 katika usawa wa Bahari

2.PNG

Ikiwa mpira utapasuka au kuwa na kasoro wakati wa mechi basi mechi imesimamishwa na itaendelea tena kwa kudondosha mpira mpya katika eneo ambalo mpira wa kwanza ulipata kasoro

Iwapo mpira ulisimama ndani ya eneo la goli, Mwamuzi wa mchezo atadondosha mpira mpya kwenye mstari wa eneo la goli (Goal Area line) sambamba na Mstari wa goli (Goal line), sehemu itakayokuwa karibu na mpira uliposimama

Mpira ukipata kasoro wakati wa kupiga penati au ukiwa ndio umepigwa kutoka kwenye alama ya penati, ukiwa unaelekea golini kabla ya kuguswa na mtu yeyote au kugusa mwamba wa goli, penati inarudiwa

Mpira ukiharibika wakati Kona, Faulo, Kurushwa Ndani ya Uwanja, Penati au 'Goal Kick' inaenda kupigwa ikiwa bado haijapigwa mpira mpya utaendelea na tukio hilo

Mpira unaweza usibadilishwe wakati wa mechi inaendelea bila maamuzi ya Mwamuzi wa mchezo husika

2.PNG


Pia Unaweza kusoma; Sheria za Soka za FIFA: Ifahamu Sheria namba Moja ya FIFA inayohusu Uwanja wa Soka
 
Saf

Lakini punde, akakwingilia Jack Chan shashaaa
 
Back
Top Bottom