Rashda Zunde
JF-Expert Member
- May 28, 2022
- 297
- 285
Kumekuwa na mijadala mikubwa kufuatia kauli zilizotolewa ndani ya Bunge la Umoja wa Ulaya (EU), zikilenga kuishinikiza Tanzania kuhusu masuala ya siasa za ndani, hasa yanayohusishwa na mwanasiasa Tundu Lissu. Hata hivyo, kuna mambo muhimu ambayo yanapaswa kuwekwa sawa ili kuepuka taswira potofu kuhusu Tanzania na misingi yake ya kikatiba.
Kwanza, ni vyema kukumbuka kwamba Tanzania ni nchi yenye mamlaka kamili ya kufanya maamuzi yake kama taifa huru (sovereign state). Hii ni misingi ya msingi katika mahusiano ya kimataifa – kila nchi ina haki ya kujiamulia mambo yake ya ndani bila kuingiliwa.
Aidha, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iko wazi kabisa katika kulinda amani, umoja na utulivu wa nchi. Inapinga vikali vitendo vyovyote vya uvunjifu wa sheria, hasa vinavyoweza kuchochea wananchi kuasi au kuichukia serikali yao. Sheria za nchi hazipo kwa ajili ya kuvunja demokrasia, bali kulinda utulivu wa kitaifa unaowawezesha wananchi wote kuishi kwa amani bila woga.
Kuhusu hoja za uchaguzi na ushiriki wa EU kama waangalizi, ukweli ni kwamba Umoja wa Ulaya haukutimiza matakwa ya kisheria yaliyowekwa na Tanzania. Walikataa kusaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi — nyaraka muhimu zinazotoa uhalali wa kisheria kwa taasisi za nje kushiriki kama waangalizi. Hatua yao ya kujitoa ilitokana na maamuzi yao wenyewe. Hivyo basi, kutoshiriki kwao hakukuathiri kwa namna yoyote uhalali wa mchakato wa uchaguzi uliofanyika kwa mujibu wa Katiba na sheria za Tanzania.
Hivi karibuni, akizungumza mbele ya Kamati ya Haki za Binadamu ya Bunge la Ulaya, Mbunge Michael Gahler aliomba bunge hilo lizingatie kuzinyima misaada nchi za Afrika ambazo, kwa mtazamo wake, “zinazuia wapinzani kushiriki kwenye uchaguzi” hadi pale hali hiyo itakaporekebishwa. Pia alitoa hoja kwamba EU mara nyingi haioni haja ya kutuma waangalizi wa uchaguzi katika nchi fulani kwa sababu, kwa maneno yake, “wanajua tayari matokeo yatakuwaje.”
Lakini hapa ndipo hoja ya msingi inapojitokeza: je, ni sawa kutumia misaada kama silaha ya kisiasa ili kuingilia maamuzi ya kisheria na kikatiba ya nchi huru? Na je, hoja kwamba kutotumwa kwa waangalizi kunamaanisha uchaguzi si huru, inasimama kweli wakati ni EU wenyewe waliokataa kutimiza taratibu za msingi zilizowapa nafasi ya kushiriki?
Ni wazi kwamba presha kama hizi, zinazoendeshwa kwa misingi ya kisiasa na propaganda, zinalenga kuyumbisha nchi zinazoendelea ili zifuate matakwa ya nje bila kuzingatia uhalisia wa ndani na uhuru wa kikatiba. Tanzania ina haki kamili ya kulinda amani, umoja na utulivu wake, na misingi hii haipaswi kutishiwa na mashinikizo kutoka nje yenye misingi ya kisiasa au maslahi binafsi.