Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 324
- 649
Mijadala mingi muda hautoshi. Nimeona nishiriki kidogo mjadala wa aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Ndg Makonda. Nimeona watu wengi wanajaribu kulijadili jambo hili kwa upambe na tofauti zao za huko nyuma.
Wanaoweza kushangilia hili la Makonda ni wale tu ambao wanategemea kuishi leo na kesho hawataki kuishi. Wanaoweza kushangilia hili la Makonda ni wale ambao hata wakifa leo wanajua hawana familia itakayoendelea kuishi kesho.
Hoja za Makonda zinatakiwa kuongeza kasi ya upatikanikaji wa sheria imara ambazo zinajengwa na msingi wa katiba imara. Katiba tuliyonayo sasa haikidhi matarajio ya kizazi hiki. Tukiwa na katiba imara inayosimamia misingi ya umoja wa kitaifa tutakuwa tumepata kuondokana na haya ya akina Makonda.
Taifa la kuviziana haliwezi kukua bali kuendelea kudumazwa Kwa kuwa Kila mtu atakuwa anafikiria kisasi akipata fursa.
Niwarejeshe nyuma kidogo, kabla ya mwaka 2009 Mhe Dkt Mwakyembe aliumwa ugonjwa uliosadikika ni kuwekewa sumu. Wengine walidai ni visasi. Baadaya mwaka 2015 tumeona akina Lugumi kuwekwa ndani, Lugemalila lakini pia tukio BAYA la Mhe Lisu kupigwa risasi. Huku mtaani watu waliongea mengi.
Siku za hivi karibuni tumeona akina Sabaya na Sasa Makonda. Ukiunganisha doti unaweza kuona kitu. Inawezekana 2030 kuendelea wapo wengine wataanza kufanyiwa haya.
Tiba ya haya ni kuwa na Sheria ambayo kila mtu zitamsimamia. Yanayomtesa Makonda leo ni udhaifu wa Sheria zetu zilizoshindwa kumdhibiti akiwa RC. Tunakumbuka kipindi hicho aliyekuwa Rais aliwapa wasaidizi wake kufanya chochote hata kama watavunja Sheria kuliko kutokufanya kabisa.
Sasa vijana nao bila kujua wakawa miungu watu ambayo Leo inawatesa. Sheria zetu hususani katiba ingekuwa imedhibiti haya JPM asingewaruhusu kufanya chochote kuliko kutofanya kabisa.
Ushauri wangu, haya mambo Kila mtu yanaweza kumkumba ni swala la wakati tu. Hatupaswi kushangilia bali kuandaa Sheria za kutulinda.