sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
LGBTQ = UPINDE
Hakuna tatizo pale mtu anaridhiana ama kusapoti lgbtq akiwa yeye kama yeye ama akiwa anatumia sheria za serikali lakini suala la mtu kujivika ukristo kwenye kufanya maridhiano ama kusapoti na hata kuhalalisha lgbtq hio haikubaliki hata kidogo.
Nashangaa kuliona kanisa kubwa leo hii viongozi wake wakiwa wanakaa meza moja kuwapa moyo, kuwapa matumaini, kufanya maridhiano na kwa baadhi yao wamefikia hadi steji ya kuhalalisha Lgbtq kwamba ni sawa Hii haikubaliki kabisa, Panya ukimpa maziwa atahitaji siagi na vingine, Yalianza mambo ya kuwasikiliza leo hii tulipo hawa lgbtq wanapaziwa sauti na viongozi kwamba wakaribishwe makanisani na hata kufungishwa ndoa makanisani !!
Kinachofanyika ni kwamba Mamlaka ya Mungu yanaanza kubadilishwa yaendane na wanachotaka watu flani, kama leo hii kanisa linaona ndoa ya mwanaume kwa mwanaume ama mwanamke kwa mwanamke ni sawa, Je ni kipi kinawazuia kuhalalisha ndoa ya mbwa na mwanamke / mwanaume ?
Mungu pekee ndie anaetengeneza sheria, Hata tunapoenda makanisani ni sisi ambao tumeenda kujikumbusha kubadilika ili tuweze kuwa katika vigezo anavyovitaka Mungu na sio sisi kumbadili Mungu akidhi vigezo tunavyotaka.
Hapo mwezi uliopita niliona kiongozi wa kanisa kubwa tu anawapigia debe lgbtq kwamba eti wakaribishwe makanisani, Nikiri sina tatizo kwa hawa watu kushiriki lakini tatizo lilipo ni kwamba watashiriki vipi kanisani huku wakiendelea kufanya ufuska wao na kuona kwamba hakuna shida yoyote ?
Kanisa lipo wazi kwa watenda dhambi wote kuanzia malaya, wezi, wazinzi, n.k. Kanisa lipo kwajili ya kuwasafisha kwa kutoa mafundisho ya, kukemea dhambi, n.k. lakini sio kuwahamasisha kundi flani la watenda dhambi kwamba ni sawa wanachotenda.
Ieleweke kwamba ukweli mchungu kwa wapenda dhambi ni kwamba ufalme wa Mungu ni lazima wauone una Ubaguzi nae pia Mungu ni mbaguzi kwa watu wasiozifata sheria zake, Kashaweka sheria zake endapo unataka umuabudu na kuwa sehemu ya ufalme wake. Kwa lugha nyepesi kabisa ni kwamba Ufalme wa Mungu sio kwa kila mtu, ni kwa wale tu wenye nia ya kufanya anachotaka na sio wao kufanya wanachotaka kwa kuzirekebisha Sheria zake. Ni jukumu la kila mkristo kutubu dhambi zake, kuzijutia, kuzigeuka kwa kuziacha na kufata njia impendezayo Mungu,
Kinachomchukiza Mungu ni dhambi na sio mtu alietenda maana sisi wote ni watoto wake tulioumbwa katika mfano wake na ndio maana huruma yake huwa ni kubwa sana kwetu kiasi cha kuwa tayari kutusamehe Lakini kwa sharti kwamba tuzifate sheria zake zinazotukemea dhambi ambazo alishaziorodhesha ikiwemo ushoga na usagaji, hata kanisani wanaotenda dhambi wanakaribishwa lakini hujutia dhambi walizofanya na kutambua kwamba wamemkosea Mungu, hivyo kuwashirikisha lgbtq sio shida lakini wao kuendelea na dhambi wakiona ni sawa ndipo penye tatizo linalowafanya wabaguliwe.
Niwaombe wakristo na hasa viongozi wasiwe mbwa mwitu walivaa vinyago vya kondoo kuwapeleka kondoo wao mahali siko, wasiwe walimu wa mchongo ambao biblia imeshatuonya, kumbukkeni wajibu wenu wa kulinda imani, acheni kufundisha mambo ya usawa ama kuwashirikisha watu wanaofanya dhambi bila kuwa na nia ya kubadilika na kutambua wanachofanya hakimpendezi Mungu.