Uchaguzi 2020 Sheria zinazozuia matusi katika Uchaguzi Mkuu ni zipi?

Uchaguzi 2020 Sheria zinazozuia matusi katika Uchaguzi Mkuu ni zipi?

Gellangi

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2016
Posts
2,782
Reaction score
3,018
Ninajiuliza ni sheria zipi zinazosimamia na kuzuia matusi wakati wa Uchaguzi ujao wa Udiwani, Ubunge au Urais hapo Oktoba 2020. Tafsiri ya tusi/matusi ni nini? Je,hawa watakaotuhumiwa kuwa wametukana watawezaje kuthibitishwa?

Je, haiwezekani mtu akamtuhumu mshindani wake katukana ili asiwe mshindani wakati wa kampeni. Kesi zitajaa mahakamani kwa jambo ambalo ni vigumu sana kulithibitisha na gharama, muda mwingi wa mahakama vitatumika kusikiliza mashauri yasiyo na tija.

How come matusi yakawa kitisho cha uchaguzi wa haki kuliko ukosefu wa Tume Huru ya Uchaguzi au vitisho vinavyoendelea kwa wapinzani?

Badala ya kujadili na kukukubaliana bila kuburuzana juu ya umuhimu wa kuwa na uwanja sawa wa mchezo kwa washindani wote, tunaanzisha jambo ambalo litaenda kuongeza migogoro zaidi?

Tanzania ni Yetu sote, siyo mali ya CCM au watu wachache wanaofanya wapendavyo.
 
Sidhani kama wataweza kumshtaki mtu atakaekuwa mgombea kwa maneno aliyoyatoa kwenye kampeni, hapa wao wenyewe watapoteza focus hivyo wasidhani watawapoteza wapinzani peke yao.

Hasa nikijaribu kufikiria hilo neno "tusi" naona linatofautiana maana kati ya mtu mmoja na mwingine, yupo anaeona kupingwa hoja zake kwake ni sawa na tusi, yeye amezoea kusifiwa tu kwa kila atachoongea, sasa unapokuwa na mgombea wa aina hii kidogo inakuwa ni tatizo.

Muhimu wapinzani watatikiwa wawe makini na lugha watakazotumia wakati wa kampeni ili kutompa sababu mtu yeyote ya kuwapeleka mahakamani.
 
Ni uoga wa CCM wa kukosa hoja ndiyo unawafanya watake kuwawekea hofu ya kujieleza kwa uwazi wapinzani.
Walio na hofu ya matusi watoe orodha ya matusi hayo ili yasisemwe!
 
Sijui kila kitu kinafanywa kiuharakati? Au labda matusi yaweze kuhalalishwa?

Nafikiri kama mtu hajui matusi ni nini basi consult mwanasheria before you comment.

Sheria kubwa inayohusiana na masuala ya jinai ni penal code. Hivyo matusi na mengineyo Soma hapo utajua, sio mtu kusema katiba imevunjwa eti ni tusi.

Yapo maneno mengine ya dhihaka hata kwa watu waliofariki, kama mwlm Nyerere ambayo huyo kiongozi anayatoa huku akijua ni uongo na dhihaka.

Lakin km mtu akishtakiw kwa matusi na sheria zipo, itapimwa Hilo neno na kama ni tusi atapata adhabu na kama sio tusi basi hatafungwa. Mbona ni simpo tu?

Ila inaonekana mhusika alietoa comment yake hapa anapenda matusi yatumike kma njia ya kawaida kupata kura, sijui kazoea matusi
Sidhani kama wataweza kumshtaki mtu atakaekuwa mgombea kwa maneno aliyoyatoa kwenye kampeni, hapa wao wenyewe watapoteza focus hivyo wasidhani watawapoteza wapinzani peke yao.

Hasa nikijaribu kufikiria hilo neno "tusi" naona linatofautiana maana kati ya mtu mmoja na mwingine, yupo anaeona kupingwa hoja zake kwake ni sawa na tusi, yeye amezoea kusifiwa tu kwa kila atachoongea, sasa unapokuwa na mgombea wa aina hii kidogo inakuwa ni tatizo.

Muhimu wapinzani watatikiwa wawe makini na lugha watakazotumia wakati wa kampeni ili kutompa sababu mtu yeyote ya kuwapeleka mahakamani.
 
Umeuliza swali zuri! Let us first define Tusi/matusi, this will make our arguments focused!

Kuna kumwambia mtu kuwa wewe unavunja katiba kwa moja, bili, tatu.. akasema umenitukana! Haya yatajitokeza sana maana kuna mtu hataki kukosolewa na kuambiwa ukweli..
Hiyo ndiyo hofu kubwa kwa watenda haki.Watafunguliwa kesi za matusi za kuwatosha ili wapoteze focus.
Tuelezwe ni matusi gani haya yanayozuia maendeleo yetu hadi tushindwe kuambiana ukweli.
 
Mbona ccm ndio wanaongoza kwa matusi, lugha za kejeli na hata kutishia wenzao maisha!
Wanadhalilisha wapinzani kila mahali kuanzia mitaani,majukwaani,Bungeni na hata kutoka kwa Mzee Baba na watoto wake waliotapakaa nchi nzima.
Wamejimilikisha vyombo vyote vya maamuzi na usimamizi wa sheria na mihimili kwa manufaa yao.Gharama zote hizo zinabebwa na wanyonge.
 
Sijui kila kitu kinafanywa kiuharakati? Au labda matusi yaweze kuhalalishwa?

Nafikiri kama mtu hajui matusi ni nini basi consult mwanasheria before you comment.

Sheria kubwa inayohusiana na masuala ya jinai ni penal code. Hivyo matusi na mengineyo Soma hapo utajua, sio mtu kusema katiba imevunjwa eti ni tusi.

Yapo maneno mengine ya dhihaka hata kwa watu waliofariki, kama mwlm Nyerere ambayo huyo kiongozi anayatoa huku akijua ni uongo na dhihaka.

Lakin km mtu akishtakiw kwa matusi na sheria zipo, itapimwa Hilo neno na kama ni tusi atapata adhabu na kama sio tusi basi hatafungwa. Mbona ni simpo tu?

Ila inaonekana mhusika alietoa comment yake hapa anapenda matusi yatumike kma njia ya kawaida kupata kura, sijui kazoea matusi
Kujinyea lws lilikuwa tusi au hapana
 
Muhimu tunataka sera na nini utawafanyia watanzania na siyo kumshambulia mtu binafsi kwa kudhalilisha. Hiyo ndiyo demokrasi ya kampeni tunayotaka sisi wananchi.
 
ukiitaja ccm kushindwa kuleta maendeleo hilo tayari ni tusi
 
Back
Top Bottom