Umeuliza swali zuri! Let us first define Tusi/matusi, this will make our arguments focused!Tafsiri ya tusi/matusi ni nini?
Sidhani kama wataweza kumshtaki mtu atakaekuwa mgombea kwa maneno aliyoyatoa kwenye kampeni, hapa wao wenyewe watapoteza focus hivyo wasidhani watawapoteza wapinzani peke yao.
Hasa nikijaribu kufikiria hilo neno "tusi" naona linatofautiana maana kati ya mtu mmoja na mwingine, yupo anaeona kupingwa hoja zake kwake ni sawa na tusi, yeye amezoea kusifiwa tu kwa kila atachoongea, sasa unapokuwa na mgombea wa aina hii kidogo inakuwa ni tatizo.
Muhimu wapinzani watatikiwa wawe makini na lugha watakazotumia wakati wa kampeni ili kutompa sababu mtu yeyote ya kuwapeleka mahakamani.
sahihiNi uoga wa CCM wa kukosa hoja ndiyo unawafanya watake kuwawekea hofu ya kujieleza kwa uwazi wapinzani.
Walio na hofu ya matusi watoe orodha ya matusi hayo ili yasisemwe!
Hiyo ndiyo hofu kubwa kwa watenda haki.Watafunguliwa kesi za matusi za kuwatosha ili wapoteze focus.Umeuliza swali zuri! Let us first define Tusi/matusi, this will make our arguments focused!
Kuna kumwambia mtu kuwa wewe unavunja katiba kwa moja, bili, tatu.. akasema umenitukana! Haya yatajitokeza sana maana kuna mtu hataki kukosolewa na kuambiwa ukweli..
Wanadhalilisha wapinzani kila mahali kuanzia mitaani,majukwaani,Bungeni na hata kutoka kwa Mzee Baba na watoto wake waliotapakaa nchi nzima.Mbona ccm ndio wanaongoza kwa matusi, lugha za kejeli na hata kutishia wenzao maisha!
Kujinyea lws lilikuwa tusi au hapanaSijui kila kitu kinafanywa kiuharakati? Au labda matusi yaweze kuhalalishwa?
Nafikiri kama mtu hajui matusi ni nini basi consult mwanasheria before you comment.
Sheria kubwa inayohusiana na masuala ya jinai ni penal code. Hivyo matusi na mengineyo Soma hapo utajua, sio mtu kusema katiba imevunjwa eti ni tusi.
Yapo maneno mengine ya dhihaka hata kwa watu waliofariki, kama mwlm Nyerere ambayo huyo kiongozi anayatoa huku akijua ni uongo na dhihaka.
Lakin km mtu akishtakiw kwa matusi na sheria zipo, itapimwa Hilo neno na kama ni tusi atapata adhabu na kama sio tusi basi hatafungwa. Mbona ni simpo tu?
Ila inaonekana mhusika alietoa comment yake hapa anapenda matusi yatumike kma njia ya kawaida kupata kura, sijui kazoea matusi