Sehemu ya 18
Siku iliyofuata kwanza nilikwenda kwa huyo mchungaji nyumba ya 12 toka nakaaa, nilipoona maisha yake niliwaza yani huyu na kijumba cha nyasi kweli ndio aje kunibabaisha et anajikita nani?
kipindi nasema hivyo mimi sijui sura yake, na wala sikutajiwa jina lake na ndugu zake
chapchap nikabisha kageti kadogo na maraaaaaa haaaaa
Shunie
Nilisema kwa sauti
Shunie: ooooooh ndio umekuja, umejuaje?
Mimi: Nakaa mtaa wapili tu hapo nilisikia kuna mchungaji alikuja nyumbani
Shunie: Nisubiri
Alitoka na viti vitatu
tukakaaa kibarazani yeye na mimi
Wananchi yule mtoto ni mzuriiiii sana sana sana alikuwa nananiongelesha ila kiuhalisia sikumbuki hata alichonieleza kabisa
mimi ni kutingisha bichwa langu kama kenge maji
Wewe, Shunie alisema
Mimi: Naam
Shunie: Nijibu basi sio eee
Mimi: uliza tena mke wangu
Shunie: Unafanya biashara gani? maana baba alinieleza kuwa kwako ni tajiri sana
Mimi: (Najiwazia: huyo mzee asingezaa kisu ningemtoa kafara shenzi) Mimi nimfanyabiashara kariakoo
Shunie: Ohhhh kwaiyo siku ile ulitoka kazini
Mimi: Yeah Mrembo, hv unamchumba nataka nikuoe
Shunie: (kuchekacheka tu)
Mimi(UBoBo): kweli nataka nikuoe
Kipindi nasema hivyo nilisikia bonge la msonyooo MSIYUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU NAONA UNAJIKUTA MWAMBA NISIPOWEPO SHAURI YAKO KIAZI WEWE
Shunie: kweli basi nichumbie maana nimependa swaga zako sanaaaaa, unaitwa nani?
Mimi: Binadamu Mtakatifu
Shunie: Aaaaaaaaa mm sijapenda hilo jina halina swaggggg
OHHHH upo na mgeni
Mzee mmoja mwenye suti mpauko, upara, mfupi mnene, vidole kama chips za pizza hut, kiatu kirefu, rafudhi ya kimangi
Shunie: Huyu ndio baba yangu anaitwa Askofu. Gily
Mimi: Shkamoo, wewe ndio mzee uliokuja nyumbani kwangu
Gily: Yaaap ndio mimi, kijana unashida sana
Mimi: Kwaherini kuna mahali nawahi
Gily: chukua namba yangu
Nilichukua ila sio kwamba nilitaka basi tu, kumuona yule mzee kulinitoka hamu
Shunie: Ngoja nikusindikize
Kweli tuliongozama mpaka nje nilipopaki ndiga V8 SAHARA
Shunie: Oooooooooh my god my dream car
Mimi: Usijali utapata tuwe mwili mmoja tu
ITAENDELA