Shetani huwa anatushtaki sisi wanadamu kwa Mungu kila tukivunja sheria ya Mungu



Umesema Shetani ndiye “asili ya dhambi”, lakini Biblia yako yenyewe haitoi fundisho hilo kwa namna unavyodai. Biblia inasema “kila mtu hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe” (Yakobo 1:14–15), na “mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23).

Pia, kama Yesu ndiye Mungu Mwana anayelipia dhambi kwa damu yake, swali ni: Mungu alijilipia nani? Na kwa nini Yesu mwenyewe alisema: “Baba ni mkuu kuliko mimi” (Yohana 14:28), na akamwomba Mungu wake (Yohana 17:3)?

Kuhusu Shetani, Yakobo 4:7 inasema: “Mpingeni ibilisi, naye atawakimbia.” Hilo halithibitishi kwamba kila jambo baya au kila dhambi imetokana na Shetani.

Kwa hiyo tusichanganye mafundisho. Lete aya ya Biblia inayosema wazi kwamba Shetani ndiye aliyeumba au kuanzisha dhambi, na kwamba Yesu ni Mungu aliyekuja kujilipia mwenyewe kwa damu yake.
 
YESU sio malaika.
 


Unasema mengi sana, lakini tatizo ni kwamba mengi hayamo katika Biblia kama ulivyoyasimulia. Tuchunguze Biblia yako yenyewe:

  1. Biblia haisemi Shetani alitaka kupata theluthi mbili ya malaika ili awe na nguvu kuliko Mungu. Ufunuo 12:4 inasema joka likavuta “theluthi ya nyota za mbinguni,” lakini aya hiyo haisemi kwamba hao ni malaika waliomfuata Shetani wala kwamba lengo lake lilikuwa kupata theluthi mbili.
  2. Biblia haisemi Mikaeli alimtupa Shetani kuzimu na kuanzisha ufalme wake huko. Ufunuo 12:7–9 inasema Mikaeli na malaika zake walipigana na joka, lakini joka akatupwa duniani. Hilo ni tofauti na simulizi lako.
  3. Biblia haisemi fallen angels walifundisha wanadamu uchawi, sayansi ya silaha na maasi yote. Mwanzo 6:1–4 inataja “wana wa Mungu” na Wanefili, lakini haisemi kwamba waliwafundisha wanadamu sayansi ya silaha au uchawi.
  4. Biblia haisemi watoto wanaopatikana kwa waganga wa kienyeji ni majini. Huo ni utafiti/madai yako, si fundisho la Biblia. Lete aya inayosema hivyo.
  5. Kuhusu Abadoni/Apolioni, Ufunuo 9:11 humtaja kama “malaika wa kuzimu” anayehusishwa na lile shimo lisilo na mwisho. Lakini Biblia haisemi kwamba yeye ataangamiza “robo ya dunia.” Ufunuo 9:15 inasema theluthi ya wanadamu waliuawa katika tukio hilo—si robo ya dunia.
Kwa hiyo usichanganye Biblia na simulizi za elimu ya uchawi, tafsiri zako na mafundisho ambayo hayajaandikwa.

Lete aya moja moja ya Biblia inayothibitisha madai yako: kwamba Shetani alilenga theluthi mbili ya malaika, Mikaeli alimpeleka kuzimu, fallen angels walifundisha uchawi na sayansi ya silaha, na watoto wa waganga ni majini.
Kama Biblia haisemi hayo, usiyape hadhi ya kuwa mafundisho ya Biblia.
 
1 Yoh 3:8 S
atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi

Ufunuo WA Yohana 12
7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;

8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.

9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.

Idadi ya hao malaika zake inatajwa kuwa ni theluthi moja.
Kutupwa Duniani na Theluthi ya Malaika: Katika Ufunuo 12:4 na Ufunuo 12:7-9, inaelezwa kuwa kukazuka vita mbinguni ambapo Mikaeli na malaika zake walipigana na lile joka (Shetani). Joka likashindwa na likatupwa chini duniani pamoja na malaika zake wote. Fungu la 4 linataja kuwa mkia wa joka hilo ulikokota theluthi moja ya nyota za mbinguni (zinazotafsiriwa kama malaika walioasi) na kuzitupa chini.

Elimu ya FALAKI pia inaelezea pia kuwa shetani aliwaza moyoni MWAKE awadangays 2/3 ila akaambulia 1/3
 
Katika Henoko Sura ya 7 na ya 8, inaelezwa jinsi kundi la malaika 200 walioasi chini ya kiongozi wao aitwaye Semyaza na Azazeli walivyoshuka duniani na kuanza kuwafundisha wanadamu mambo mbalimbali yaliyoharibu maadili yao:
• Semyaza: Alifundisha uchawi na uganga (enchantments) na jinsi ya kukata mizizi kwa ajili ya madawa na uchawi.
• Armaros: Alifundisha jinsi ya kufungua au kutegua vifungo vya uchawi (resolving of enchantments).
• Baraqiyal: Alifundisha mambo ya unajimu (astrology).
• Kokabiel: Alifundisha elimu ya makundi ya nyota.
• Azazeli: Alifundisha jinsi ya kutengeneza silaha za vita (panga, visu, ngao) na sanaa ya kujiremba (vipodozi vya macho na mapambo), jambo lililosababisha uzinzi na unyama kuongezeka duniani
 
. Chimbuko la Uchawi na Elimu ya Giza
Kwenye Biblia ya sasa (Mwanzo 6)*, inatajwa kwa ufupi sana kuwa "wana wa Mungu waliona binti za wanadamu ni wazuri wakawaoa." Lakini Kitabu cha Henoko kinaingia ndani zaidi:
Kinaeleza kuwa wale viumbe walikuwa ni Malaika walioasi (The Watchers) wakiongozwa na kiongozi wao aitwaye Semyaza na mwenzake Azazeli.
 

Ufu 12:4
Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake.
Nyoka JOKA =shetani/ibilisi...NYOTA za mbinguni alizozikokota/zidanganya zi asi zitupwe chini=MALAIKA WA ASI walio muasi Mungu wakatupwa chini...ndio hao wenzetu mnasema kuna majini wazuri na wabaya haya mashetwani...haya nitajie majina ya majini wazuri unaowajua taja majina Yao ili tuhakikishe kama ni mazuri kweli,HAKUNA JINI MZURI WOTE NI WABAYA.
 
Shetani Hana uzuri na mwanadamu, mashetwani hayana uziri KWA mwanadamu MAJINI HAYANA UzuRI KWA MWANADAMU,kama kuna. MTU anafuga majini aseme atuambie anafuga AINA GANI YA JINI jina la hilo jini analofuga halafu sisi tutamwambia ubaya wake kama haujui.

kama kuna MTU ana mizimu ya uganga WA kienyeji au uchawi aseme hapa mizimu yake inaitwaje ,tutamuelewesha ubaya wake WA mizimu,ndio atajua KWA Nini watu wanakataaga na kukimbia uganga WA kienyeji...mizimu inawalazimisha KWA kuwatesa wachukue mikoba ya uganga WA kienyeji...mizimu NAYO ni MAJINI ya ukoo.
 
Yesu ndio mtetezi KWA MAANA sisi wanadamu wote tumetenda dhambi na kafara ya sadaka ya wanyama haziondoi dhambi kabisa,ila damu ya Yesu inaondoka thambi kabisa KWA asilimia 100% bila ya Yesu sisi tusingepata kuhesabiwa HAKI na kusamehewa dhambi,damu ya Yesu ilikuwa inasubiriwa hata na waliokuwa kabla ya Yesu kuna duniani ili iwatakase hata mbinguni...
MATENDO makuu kabisa ni moja KUFUFUKA KWA YESU ,kusulubiwa KWA Yesu pale masalabani alibeba dhambi zetu zote na za watoto watakaokuja kuzaliwa MBELENI za DUNIA NZIMA ,mateso ya Yesu yalikuwa makali KIMWILI na KIROHO NA NAFSI kubeba dhambi za ulimwengu wote sio mchezo,Yani apigwe na kujeruhiwa KWA makosa ya dunia NZIMA na vizazi vijavyo vilivyopo na vilivyopita.BILA YA YESU hakuna wokovu,hakuna Uzima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…