Shetani na robo ya Malaika ndio waliasi Mbinguni na Mungu anahaingaika hivi kuwazuia, nafikiri wangeasi Nusu ya Malaika basi wangemuua kabisa Mungu

Mkuu nashukuru nimecheka Tu..Yaani wangekuwa wameasi nusu wangemuua MUNGU.!!!!! Kwamba Huyo MUNGU angekuwa dhaifu kiasi gani???
 
Ila wanadamu mmenishinda tabia 😃😃😃😃😃😃
 
Aisee
 
Ila kuna watu mnafikiriaga ujinga 🤣
Ngoja wafia dini waje.
 
bana wee unauhakika? binafsi nakuomba uni converse kwa hili.
 
Wewe ni Muongo na ni mzushi.

Nani dhalimu zaidi ya yule anayemzushia uongo Mungu?


Quran hakuna aya hata moja inayosema kuwa kuna kundi la malaika lilimuasi Mungu pamoja na shetani.

Malaika hawajaumbwa kumuasi Mungu bali wanatekeleza kila waliloamrishwa.


Malaika waneumbwa kwa Nuru.

Iblis ni jini ameumbwa kwa Moto

Adam ameumbwa kwa udongo.


Binadamu na Majini ndio viumbe viwili vilivyopewa uhuru wa kutenda na kuchagua kati ya mema na mabaya. Malaika wao wameumbwa kutenda yale waliyoamrishwa na Mungu tu.
 
Biblia na Quran zote Zina story za uwongo uwongo, haiingii akilini Kama una akili timamu
unaikataa Quran kwa kuwa huna akili timamu. Ila karibu utakuja jua.

Mungu kashawaelezea watu waliokufuru kama wewe


Quran

Al-Furqan 25:4

وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ إِنْ هَٰذَآ إِلَّآ إِفْكٌ ٱفْتَرَىٰهُ وَأَعَانَهُۥ عَلَيْهِ قَوْمٌ ءَاخَرُونَۖ فَقَدْ جَآءُو ظُلْمًا وَزُورًا

English - Sahih International

And those who disbelieve say, "This [Qur’ān] is not except a falsehood he invented, and another people assisted him in it." But they have committed an injustice and a lie.

Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani

Na wamesema walio kufuru: Haya si chochote ila ni uzushi alio uzua, na wamemsaidia kwa haya watu wengine! Hakika hawa wamekuja na dhulma na uwongo.

Al-Furqan 25:5

وَقَالُوٓا۟ أَسَٰطِيرُ ٱلْأَوَّلِينَ ٱكْتَتَبَهَا فَهِىَ تُمْلَىٰ عَلَيْهِ بُكْرَةً وَأَصِيلًا

English - Sahih International

And they say, "Legends of the former peoples which he has written down, and they are dictated to him morning and afternoon."

Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani

Na wakasema: Hivi ni visa vya watu wa kale alivyo viandikisha, anavyo somewa asubuhi na jioni.
 
Pengine hujui au unaamua kupotosha Tu

Malaika ni viumbe ambao hawana matamanio na hawamuasi MWENYEZIMUNGU na wao tangia wameumbwa kazi Yao ni kumtumikia na kumuabudu MWENYEZIMUNGU Tu

Ibilisi (shetani) ni miongoni mwa majini na sio malaika na hajawahi kua malaika ila alipata kuishi na malaika

Ujue kutofautisha Malaika,Jini, Binadamu hawa ni viumbe miongoni mwa viumbe alivoviumba MWENYEZIMUNGU

Sasa hayo mafundisho yenu kwenye vitabu vyenu vya KISHETANI (wazungu) na elimu zenu za kubumba na kwakua nyie kazi yenu ni kumeza tu kila mnachoambiwa na wazungu basi jua kua mnaingizwa chaka
 
Ulichokiongea unakijua?
 
Kwamba Mungu kamuacha shetani makusudi awe mtihani kwetu!? Mungu anayetupeda sana ametuumbia shetani atutese na tukishindwa kupambana naye anatuchoma moto! Kwanini asimteketeze huyo shetani Dunia iwe sehemu salama? Kama shetani ni jini sawa nakubaliana na wewe, ila Mungu si ana mamlaka juu ya majini kwakuwa kayaumba yeye?
 
Umekimbia swali ustaadhi, umeulizwa kwanini Mungu atupambanishe na shetani? Kuna faida ipi? Hiyo haihusiani na faida ya yeye kutuumba, issue ni kwanini tupambanishwe na kiumbe kingine ambacho angeweza kukidhibiti? Shida yenu mkikosa jibu mnakimbilia kwenye kufuru au akili yetu ndogo kuliko Mungu! Tunajua yote hayo ila tujibu hilo la kutupambanisha na shetani wakati anaweza kumdhibiti, faida yake ni nini?
 
Dah! tabu kweli!

Sio wewe tu, hata tukusanyike viumbe wote wa ulimwengu hatumnufaishi chochote Mungu ... yeye hatuhitajii bali sisi ndo tunaomuhitajia!
Umaweza kutengeneza kitu usichokihitaji!? Unaweza kununua kitu usichohitaji? Huna hoja.
 
Kwahiyo jini Shetani likaamua kumuasi Mungu na kumpinga ila akaliacha litambe tu!?
Mpaka sasa hapa Duniani tukitoa alama kwa Shetani na Mungu ni wazi kuwa shetani ana asilimia nyingi za ushindi, kwanini asimdhibiti? Na kwanini amuache aangamize viumbe wake wengine?
 
Tupe na ile aya ya jua kuzama matopeni.
 
Biblia ni kitabu cha Wayahudi, wewe mtu mweusi wa Kingugi unaijua historia ya Dunia hii na viumbe wake kuliko Wayahudi? Hiyo quran yenyewe imechota maandiko ya biblia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…