Shetani tunakukemea kwa Jina la Yesu: Waachie watu uliowateka

Shetani tunakukemea kwa Jina la Yesu: Waachie watu uliowateka

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Shetani amewatekaje watu?

1. Ni kwa kupitia vita vinavyoendelea kati ya Israel na Iran. Shetani ameutumia mgogoro uliopo katika nchi hizo kuwashawishi watu wachukiane, na wamemtii. Matokeo yake sasa kuna chuki kati ya mataifa, dini na watu binafsi. Watu wanawaza kulipizana kisasi.

2. Amewatumia watu kueneza habari na taarifa mbaya za vita. Habari hizo zimewafanya watu kujaa hofu kubwa badala ya imani.

3. Amewashawishi watu kuitumia mitandao ya kijamii kuandika mada za kejeli, dhihaka, matusi, na kauli za kutenganisha watu kwa misingi ya dini na mataifa.

4. Amewatumia watu kutengeneza na kutuma picha za uongo kuhusiana na mgogoro huo wa Israel na Iran.

Shetani ameleta uharibifu katika ulimwengu wa roho, kupitia vita vya Israeli na Iran. Ameweka mitego ya kuwanasa watu wengi waingie katika ufalme wake wa giza. Amewaingizia watu mashaka kuhusu uwepo wa Mungu wa Israeli.

Leo, tumezifunua hila zako shetani na udanganyifu wako. Na kwa mamlaka tuliyopewa na Yesu, tunakukemea: waachie watu uliowateka, warudi katika ufalme wa Mungu.
 
Kanisa la Mungu - amkeni! Huu siyo wakati wa kuangalia tu taarifa za vita. Ni wakati wa kusimama na kuwaonya kwa upole wale wanaopingana na Mungu. Ni wakati wa kupiga magoti na kuomba Mungu awajalie kutubu na kuijua kweli, ili fahamu zao ziwarudie tena, waponyoke katika mtego wa ibilisi ambaye amewateka wapate kufanya mapenzi yake (2 Tim 2:25-26)

Tuombe:
Ee Mungu wa mbinguni, Baba mwenye huruma. Tunakuomba kwa unyenyekevu utembee Israeli na Iran. Gusa mioyo ya watu wa nchi hizo. Wape moyo wa toba na ufunuo wa kweli.

Kwa Jina la Yesu Kristo, tunakukemea shetani uliyewateka watu na kuwaingizia hofu, chuki, na upofu wa kiroho. Tunavunja na kubatilisha kazi zako mbovu ndani ya watu uliowateka. Kwa Jina la Yesu, tunakuamuru, waachie warudi katika ufalme wa Mungu. Acha kuwapotosha watu ili waangamie motoni siku ile ya mwisho. Tunaharibu udanganyifu wako ulioueneza kupitia vita vya Israel na Iran.

Ee Mungu, achilia rehema zako na kuleta amani Mashariki ya Kati. Ingiza upendo palipojaa chuki, ukweli palipojaa uongo, na tumaini palipojaa hofu. Asante kwakuwa shetani ameshindwa kwa uwezo wako. Asante kwakuwa Jina lako litatukuzwa katika kila taifa, na mioyo mingi itakurudia kwa kutubu na kukuamini.

Tunaomba haya kwa jina la Yesu Kristo aliye Bwana wa Amani. Amina.
 
Shetani amewatekaje watu?

1. Ni kwa kupitia vita vinavyoendelea kati ya Israel na Iran. Shetani ameutumia mgogoro uliopo katika nchi hizo kuwashawishi watu wachukiane, na wamemtii. Matokeo yake sasa kuna chuki kati ya mataifa, dini na watu binafsi. Watu wanawaza kulipizana kisasi.

2. Amewatumia watu kueneza habari na taarifa mbaya za vita. Habari hizo zimewafanya watu kujaa hofu kubwa badala ya imani.

3. Amewashawishi watu kuitumia mitandao ya kijamii kuandika mada za kejeli, dhihaka, matusi, na kauli za kutenganisha watu kwa misingi ya dini na mataifa.

4. Amewatumia watu kutengeneza na kutuma picha za uongo kuhusiana na mgogoro huo wa Israel na Iran.

Shetani ameleta uharibifu katika ulimwengu wa roho, kupitia vita vya Israeli na Iran. Ameweka mitego ya kuwanasa watu wengi waingie katika ufalme wake wa giza. Amewaingizia watu mashaka kuhusu uwepo wa Mungu wa Israeli.

Leo, tumezifunua hila zako shetani na udanganyifu wako. Na kwa mamlaka tuliyopewa na Yesu, tunakukemea: waachie watu uliowateka, warudi katika ufalme wa Mungu.
Ukitaka kumpata shetani, mtukuze Yesu kwa jina la shetani kwa vile wanafahamiana na ni ndugu walioumbwa na Mungu mmoja.
 
2 Timotheo 2:24-26
"Tena haimpasi mtumishi wa Bwana kuwa mgomvi, bali inampasa awe mwema kwa kila mtu, awezaye kufundisha, tena mvumilivu. Inampasa kuwaonya kwa upole wale wanaopingana naye, kwa matumaini kwamba Mungu atawajalia kutubu na kuijua kweli, ili fahamu zao ziwarudie tena, nao waponyoke katika mtego wa ibilisi ambaye amewateka wapate kufanya mapenzi yake."
 
Ukitaka kumpata shetani, mtukuze Yesu kwa jina la shetani kwa vile wanafahamiana na ni ndugu walioumbwa na Mungu mmoja.
Ee Mungu mkumbuke Leo X katika ufalme wako. Mfungue kutoka katika minyororo ya Ibilisi. Katika Jina la Yesu, amen.

Yesu hakuumbwa. Yesu ni Mungu, hana mwanzo wala mwisho. Shetani ndiye aliyeumbwa.
Soma Ufunuo 1:8
“Mimi ni Alfa na Omega,” asema Bwana Mungu, “aliyeko, aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.”

Soma tena Ufunuo 1:17-18:
Yesu anasema wazi hapo:
"Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, naye aliye hai; nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele, tena ninazo funguo za mauti na za kuzimu."
 
Mwinjilisti ellen g white-utuombee
Kikwete-utuombee
Martin luther-utuombee
Moses kulola -utuombee
Mwamposa-utuombee
Pastor tony -utuombee
 
Eewe Mungu mkumbuke Setfree. Mfungue toka kwenye minyororo ya uzwazwa aache kuamini na badala yake aelewe.
 
Mwinjilisti ellen g white-utuombee
Kikwete-utuombee
Martin luther-utuombee
Moses kulola -utuombee
Mwamposa-utuombee
Pastor tony -utuombee
Ellen G White, Martin Luther na Moses Kulola hawapo duniani. Kwanini unawaomba wakuombee? Hata Bikira Maria aliyekuwa mama wa Yesu hatupaswi kumuomba atuombee. Jifunze kuomba mwenyewe.
 
Eewe Mungu mkumbuke Setfree. Mfungue toka kwenye minyororo ya uzwazwa aache kuamini na badala yake aelewe.
Mungu hawezi kusikia hayo maombi, ni batili. Yameishia hewani tu.
Hujiulizi kwanini naitwa Setfree? I have truly been set free from the bondage of sin and Satan
 
Binti njoo inbox nimemkamata shetani nataka umuone.
Shetani si wa kuchezewa. Biblia inasema shetani ni simba angurumaye, akitafuta mtu wa kummeza (1 Petro 5:8). Tunamshinda kwa damu ya Yesu na kwa neno la ushuhuda wetu – si kwa ‘kumkamata’ inbox.”
 
Shetani si wa kuchezewa. Biblia inasema shetani ni simba angurumaye, akitafuta mtu wa kummeza (1 Petro 5:8). Tunamshinda kwa damu ya Yesu na kwa neno la ushuhuda wetu – si kwa ‘kumkamata’ inbox.”
Kwanza acha kutumia AI
 
Kwanza acha kutumia AI
Niliokoka kabla AI haijazaliwa. Maneno ya Mungu yamejaa ndani yangu.
Kol 3:16-17
Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.
 
Toka hapa kadanganye wajinga
 
Huu si ni Muda wa kukaa dogiee au kifo Cha Mende Binti?
1 Kor 6:9-10
Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi
 
Back
Top Bottom