Shetani yuko wapi? Nani alimshawishi Aasi huko kunakoitwa Mbinguni?

Shetani yuko wapi? Nani alimshawishi Aasi huko kunakoitwa Mbinguni?

Shetani hayupo kiuhalisia, shetani ni kiumbe wa kufikirika aliyetengenezwa na mwanadamu ili yeye mwanadamu akikosea kitu fulani apate wa kumsingizia.
Siyo kila kitu usichokiona basi hakipo
Mfano upepo, umeme
Lakini macho yetu yana uwezo wa kuona vitu na vingine hayana uwezo wa kuviona
Baadhi ya wanyama wana uwezo wa kuona vitu zaidi yetu
Shetani ni viumbe wa kiroho huwezi kuwaona

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Maswali yanaendelea....

Mungu ndiye chanzo cha yote[kwa wale wanaoamini] je ndio chanzo cha mbegu ya uasi wa shetani?

Kwanini laana ya Mungu iendelee kutafuna vizazi hata vizazi kwa kosa lililofanywa na watuwawili waliombwa na Mungu mwenyewe?

Kuna mahali kokote kwenye biblia pameonesha shetani aliko? Ni wapi kama hapajaoneshwa tunaanzaje kumchora shetani kama ndio chanzo cha haya maasi yote?

Au shetani ni sisi wenyewe? Na hapa duniani ndio makao yetu?

Nitaendelea na maswali kadri mada itakavyo endelea

MUHIMU÷ Naomba swali la thibitisha kwanza kama mungu yupo lisubiri kwanza. Tumsake kwanza huyo shetani kama kweli yupo.

Karibuni
Mungu ni Roho na Shetani pia Roho, binadamu tuna Roho na mwili. Binadamu ni physical lakini Mungu na Shetani ni upepo tu. Shetani na Mungu wanaishi Mali pote.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Kwani mkuu huwezi kufikiria nje ya vitabu vya dini??

Mm katika halmashauri ya kichwa Changu, baada ya kufanya kufikria kivyangu bila external influence, NILIJIRIDHISHA KUWA SHETANI SI HALISI, NI KIUMBE CHA KUFIRIKA TU. ALL EVILS AND GOODS ORIGINATE IN OUR OWN CONSCIOUSNESS

Gold is the money of the kings
Your right, shida tunalazimisha kuthibitisha kitu ambacho siyo physical

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Mnaposema shetani alishindwa vita mbinguni na kutupwa duniani, ina maana Mungu ni mpenda vita. Na kauli ya "samehe 70×70 hata mara moja Mungu hakumsamehe shetani, itakuwaje binadamu tusamehe mara 70 ? Hadithi nyingine ni uwongo mchana kweupe.

Kama hadithi za othmani maalim
 
Waweza soma pia hapo juu
 
Back
Top Bottom