Elections 2010 Shibuda ahamia CHADEMA

Elections 2010 Shibuda ahamia CHADEMA

Sidhani kama Shibuda atakuwa amehamia CHADEMA kwa sasa labda kama na yeye atakuwa ameamua kuji-mpendazoe kwa hasira, nadhani busara ya mgombea yeyote yule aliyeshiriki kura za maoni za CCM kwa sasa ni kungojea maamuzi ya vikao ndipo mtu ajue for sure kwamba hakuteuliwa...kwa minajili hii sidhani kama SHibuda atakuwa amejilipua mapema hii...
 
dr. samahani....hivi ulifikia wapi kwenye jitihada zako kuwania ubunge??umepita kura za maoni??
 
Sipendi kuona watu wanaokataliwa na CCM na kubaki bila jinsi ndio wanakuwa wagombea wa CHADEMA. Naelewa kuna temptation kwa CHADEMA kuwachukua kwa sababu wana name recognition, lakini naweza kumsikia Makamba akisema "Upinzani hawna kitu, wanangojea makombo ya CCM" na katika hili atakuwa right.

Kama hii habari ni kweli, hapa ninachoona ni kwamba Shibuda anataka ubunge kwa hila zote, na wala hajali siasa za vyama. Jambo la hatari sana hili.

Hamna kumpa ugombea ubunge wa CHADEMA huyu. Kuna watu wako CHADEMA miaka yote viongozi wa wilaya, wamejenga uanachama, halafu leo mtu atoke CCM mara moja apewe ugombea ubunge? Hata maji ya kijani hayajamuisha mwilini? Hii itakuwa mbaya sana kwa party morale, unles hao watu wa CHADEMA wa wilayani humo nao ni stooges tu wanaofanya siasa za hero worship and stongmen seeking.

Piga chini Shibuda, from presidential ambitions to no constituency. That's what you get for chickening on Kikwete and having no principle.
Akisema huyo Makamba si mbwabwaji kila wakati! Chadema ni chama chenye fursa sawa kwa woote wasafi! Karamagi hawezi kukubaliwa kugombea kwa tiketi ya Chadema! jamani tusichanganye pumba na mchele hao wanaokubalika ni wale wenye kutaka kutetea maslahi ya nchi hii
 
Ndio hapa unaweza kuona umuhimu wa kuwa na wagombea binafsi (CJ ansema 'wa kujitegemea'). Wengi wapo kwenye vyama kwa sababu ndio route pekee unayoweza kutumia kupata haki yako ya kuchaguliwa. Pengine Shibuda ni mmoja wao!

Kama tunataka kuangalia maslahi ya nchi kwanza na vyama baadae then sio tatizo kwa mtu kuhama chama hasa kwa vile sheria haziruhuru kusimama kibinafsi bila chama.
 
chadema ikisimamisha wagombea 'mitumba' kutoka ccm watajizunjia credibility tu.................kinachokuja kichwani ni "hivi chadema yenyewe haina watu makini mpaka ichukue kutoka kwa ccm?" kiasi cha kuwa hata kura ya uraisi inaweza ikapotea

wanaoingia chama dakika hizi za uchaguzi wasipewe chance za kugombea KAMA INAWEZEKANA kikatiba ( if they change the katiba for this, they have my support)

Na hapa ndipo nilipokuwa nimesimamia. Chadema haina wagombea katika majimbo fulani. Narudia mifano, Mwanga, Same, Muheza,Kigamboni,morogoro mjini,n.k hizi ni sehemu potential sana, mfano mwanga,wapo watu hawapigi kura kwasababu hakuna mbadala.
Sasa kama kuna jimbo hakuna chadema original, kuna shida gani kupeleka ccm makapi kama anaweza!!!
Segerea kuna chadema ndiyo maana mpendazoe kapigwa chini, na wala hawezi gombea ubungo yupo mnyika, je kuna tabu gani akigombea kigamboni au mkuranga ambako hakuna mtu. Tuache uhafidhina tutumie logics zaidi.
 
Hakuna ubaya Chadema kupokea wakimbizi kutoka CCM kinachotakiwa ni kupokea wale wakimbizi wa kweli wanaotaka kuleta mabadiliko kwa taifa letu. Tukumbuke kuwa CCM imekuwa ni kambi ya mafisadi na si wote ndani ya CCM wanaopendezwa na ufisadi. Wapinzani wa kweli watatoka ndani ya CCM kwani wanajua uchafu unaofanyika. Dr. Slaa amekuwa mpinzani wa kweli kwasababu hizo hizo. Tahadhari tusijetukapokea akina Mrema. CHADEMA MOTO CHINI!!!!!!!!!
 
Sidhani kama Shibuda atakuwa amehamia CHADEMA kwa sasa labda kama na yeye atakuwa ameamua kuji-mpendazoe kwa hasira, nadhani busara ya mgombea yeyote yule aliyeshiriki kura za maoni za CCM kwa sasa ni kungojea maamuzi ya vikao ndipo mtu ajue for sure kwamba hakuteuliwa...kwa minajili hii sidhani kama SHibuda atakuwa amejilipua mapema hii...

dokta, ninakubalina nawe kabisa kuwa chini ya mfumo wa CCM, kura za maoni huwa hazina uzito wowote, kinachojalisha zaidi ni jinsi gani mgombea anavyothaminiwa na CCM kuliko anavyopwendwa na wananchi. Hata hivyo lingekuwa ni jambo la maana sana kwa CCM kuanza kujifunza kutumikia wananchi kwa kuweka wazi kuwa kura za mani ndiyo fainali yenyewe ya uteuzi unless kama kuna malalamiko ya kuwepo kwa uvunjanji wa kanuni ambao ndio uliosababisha kura za maoni kuwa vile. Nina mfano mbichi kabisa wa chama cha Demokrat hapo Marekani ambapo kipenzi cha chama alikuwa ni mama Klintoni lakini kwa vile kura za maoni zilimtaka Obama, ikabidi hata chama chenyewe kikubaline na wananchi na kumteua Obama kuwa mgombea wao; CCM pia wafanye hivyo.

BTW:
Vipi kwenye kinyang'anyiro cha Nzega, ulifikia wapi? Najua ndugu Seleli aliambulia kapa kwa Mheshimwa Bashe, ambaye ni mfanyakazi wa kampuni mojawapo za Rostam Aziz, je wewe ulikuwa msindikizaji tu au ulifikia kiwango gani kwenye kinyangayiro kile. Je CCM inaweza kukufikiria na kukuvuta mbele zaidi ya Bashe na Seleli
 
Sipendi kuona watu wanaokataliwa na CCM na kubaki bila jinsi ndio wanakuwa wagombea wa CHADEMA. Naelewa kuna temptation kwa CHADEMA kuwachukua kwa sababu wana name recognition, lakini naweza kumsikia Makamba akisema "Upinzani hawna kitu, wanangojea makombo ya CCM" na katika hili atakuwa right.

Kama hii habari ni kweli, hapa ninachoona ni kwamba Shibuda anataka ubunge kwa hila zote, na wala hajali siasa za vyama. Jambo la hatari sana hili.

Hamna kumpa ugombea ubunge wa CHADEMA huyu. Kuna watu wako CHADEMA miaka yote viongozi wa wilaya, wamejenga uanachama, halafu leo mtu atoke CCM mara moja apewe ugombea ubunge? Hata maji ya kijani hayajamuisha mwilini? Hii itakuwa mbaya sana kwa party morale, unles hao watu wa CHADEMA wa wilayani humo nao ni stooges tu wanaofanya siasa za hero worship and stongmen seeking.

Piga chini Shibuda, from presidential ambitions to no constituency. That's what you get for chickening on Kikwete and having no principle.
Well said mate......at least not for jokers like Shibuda for heaven's sake!!
 
kula tano mkuu
Huyu ni mtu amabaye hana msimamo na mnafiki mkubwa, alitegemea favor kwa kujitoa kugombea urais CCM, kama kuna mtu alimsikia akitoa hotuba yake baada ya kijtoa ataelewa hilo.... na mara kadhaa alisha kana upinzani na kwa kubeza,,, hana maana kabisa!!!
 
Unajuaje juu ya favour? Acha kubwata.
 
Sidhani kama Shibuda atakuwa amehamia CHADEMA kwa sasa labda kama na yeye atakuwa ameamua kuji-mpendazoe kwa hasira, nadhani busara ya mgombea yeyote yule aliyeshiriki kura za maoni za CCM kwa sasa ni kungojea maamuzi ya vikao ndipo mtu ajue for sure kwamba hakuteuliwa...kwa minajili hii sidhani kama SHibuda atakuwa amejilipua mapema hii...

Kwahiyo Dr. kama na wewe ikitokea hukufanikiwa kuteuliwana chama chako kuwa mgombea hata baada ya vikao vya CC yenu, utajilipua pia kwa kuhamia chama kingine ili mradi azma yako ya kuwa mbunge itimie?
 
Nilimsikia huyo Shibuda akizungumza TBC usiku huu kwamba vyama kadhaa vya siasa vimemuomba ajiunge navyo. Viko vitatu.
 
Tusipoteze mwelekeo, Shibuda alikuwa ni subject tu, mjadala ni je '' CCM masalia'' wapewe au wasipewe uanchama pindi wakitamani mapinduzi na ukombozi wa kweli!!!!!
Kundi A] Waachwe wafie ''uwanja wa ndege'' hawana nafasi kabisa ktkt upinzani
B] Katika masalia tuchague mchele na tuache pumba. Wapiganaji wanakaribishwa
c] Wakaribishwe ila vetting process iwe ya wanachama. Mamluki wapigwe marufuku

Hint: Shibuda ni trouble maker mzuri as long as he benefit, kaanzia mbali tokea Jumuiya ya wazazi, hata CCM imeshukuru kubwaga kwake.
Hivi tunaweza kuwahukumu Selelii, Mpendazoe, Mwambalaswa, Mwakyembe, Lembeli,Shelukindo, kwa kuwafananisha na SHIBUDA.!!!!
Hivi tunawezasema Shelukindo, Selelii, Kimaro wameshindwa kura za maoni?????? Leo tumesahau EL,RA na pesa zao wamefanya nini,
bali tunawaita wanamapinduzi hawa ccm masalia!!
 
Wakuu:

Hivi kuna mtu anamchukulia John Shibuda kuwa mtu makini?

Hata juzijuzi nilikutana naye pale Rombo Bar - Sinza: Mainly alikuwa anaongea kama "anasubiri ofa"!
 
Nona ccm kupinga vikali sana wagombea binafsi walikuwa wamelenga mbali sana.Walijua wanachama wao watakaokutwa na mambo kama ya kina shibuda lazima wangepata nafasi ya kugombea na hapo ccm ingekuwa kwenye wakati mgumu sana.

Kuhusu Shibuda kutaka kuhamia Chadema ni vizuri watu kama hawa tukaangalia rekodi zao ilikuwaje wakati wlaipokuwa ccm? kama rekodi yake ilikua inaendana na mafisadi basi ni vizuri kumtosa kwani anajaribu kulinda tumbo lake na sio kutaka kuokoa taifa.

kama rekodi yake ni safi basi sio mbaya kujiunga na upinzani na tunaweza kumsamehe kwani inaweza kuwa katoswa kule kutokana na kuyapinga maovu ya wakuu wa ccm.
 
Karamagi hawezi kukubaliwa kugombea kwa tiketi ya Chadema! jamani tusichanganye pumba na mchele hao wanaokubalika ni wale wenye kutaka kutetea maslahi ya nchi hii

Mhh...on thing I have learned kuhusu Tanzania yetu ya leo ni kuwa katika siasa hakuna kitu kisichowezekana. Unapokuwa na siasa zisizojali itikadi na maadili, oppurtunism tu ndio hushika hatamu ya maamuzi na hilo lipo hata CHADEMA
 
Sipendi kuona watu wanaokataliwa na CCM na kubaki bila jinsi ndio wanakuwa wagombea wa CHADEMA. Naelewa kuna temptation kwa CHADEMA kuwachukua kwa sababu wana name recognition, lakini naweza kumsikia Makamba akisema "Upinzani hawna kitu, wanangojea makombo ya CCM" na katika hili atakuwa right.

Kama hii habari ni kweli, hapa ninachoona ni kwamba Shibuda anataka ubunge kwa hila zote, na wala hajali siasa za vyama. Jambo la hatari sana hili.

Hamna kumpa ugombea ubunge wa CHADEMA huyu. Kuna watu wako CHADEMA miaka yote viongozi wa wilaya, wamejenga uanachama, halafu leo mtu atoke CCM mara moja apewe ugombea ubunge? Hata maji ya kijani hayajamuisha mwilini? Hii itakuwa mbaya sana kwa party morale, unles hao watu wa CHADEMA wa wilayani humo nao ni stooges tu wanaofanya siasa za hero worship and stongmen seeking.

Piga chini Shibuda, from presidential ambitions to no constituency. That's what you get for chickening on Kikwete and having no principle.

Kutokana na kile tulichokisikia CCM kuhusu kura za maoni, na rushwa iliyotanda, na mpaka TAKUKURU wenyewe kupokea rushwa, kuna uwezekano mkubwa sana watu makini, wachukia ufisadi wakaachwa nje. Mimi sioni shida kwa watu kama Shibuda, Selelii kuingia CHADEMA, hao kila mtu anajua ni wapambanaji, nitashtuka kama CHADEMA watakubali watu wa design ya Malecela, ama Mungai.
 
Mbona Dr Slaa mwenyewe alikataliwa na ccm kabla ya kuhamia CHADEMA na sasa ndiye lulu? mimi naona hoja ya kwamba kakataliwa ccm kwanza na hivyo asihamie CHADEMA haina uzito stahiki. Ndio maana hatutegemei mtu kama karamagi akaribishwe chadema.
 
Neno Demokrasia ni gumu sana kueleweka!
Naona watu wameshachanganya DEMOKRASIA na DOMOKRASIA!!!
 
Back
Top Bottom