Hivi unapohama chama kwa ghfla hivi(kama amehama ) ni kwa kuwa anaamini in both sera za ccm na chadema au?
Au anaamini kuwa yeye tu ndie anaeweza kuwatumikia wananchi wa jimbo Hilo?
Wanaohama vyama ghafla wamegawanyika kwenye makundi tofauti, kulingana na mtazamo wangu.
Kundi la kwanza ni opportunists, ambao wako kwenye vyama kwa ajili ya kutaka ulaji, sasa ulaji ukiingia mchanga inabidi ahame kwenda kutafuta sehemu nyingine.
Kundi jingine, wako wanachama wa CCM ambao wanaendelea kuwa wanachama lakini kiundani wamechoshwa na madudu ya humo ndani, so ikitokea opportunity ya ku-trigger kuhama kwake, anaitumia kuondoka. Tatizo la kundi hili ni ngumu kuwatofautisha na opportunists na hasa wanapohama baada ya ulaji kuingia mchanga.
Kundi jingine, wako wana CCM ambao wakionewa na mfumo mbaya wa chama chao, huamua kuondoka na kwenda kujiunga na chama ambacho wanahisi labda mfumo wake ni mzuri. Mfano, assuming mtu ameshinda kihalali kwenye kura za maoni, halafu jina linaenda CC na NEC, jamaa wanalikata bila kutoa maelezo ya kueleweka, hakuna mtu anaweza kuvumilia hayo mambo.
Kwenye hili kundi la mwisho ndipo sasa watu hupozwa na nafasi za kuteuliwa. Hivi majuzi JK amesema kwamba wale waliokosa wawe na subira, kuna nafasi nyingi za kuteuana maana mvumilivu hula mbivu. Mfano, Dr. Tizeba alishinda mwaka jana kwenye kura za maoni, jina halikurudi. Zikaanza chokochoko za wana CCM wao wenyewe kushitakiana mahakamani, baada ya hizo chokochoko Dr Tizeba akapewa ukuu wa Wilaya Sikonge. Bwana Kangoye baada ya kugaragazana kwenye kura za maoni na uchaguzi mdogo wa Tarime, alipigiwa pande la ukuu wa Wilaya. Kuna watu wengi wanapewa post za kuwapoza ili wasiondoke, lakini inaonekana wazi kwamba wako frustrated.
Swali ambalo ninajiuliza kila siku, mtu ni Mkuu wa Mkoa/Wilaya kazi ambazo ni za kuwatumikia wananchi lakini bado anakwenda kusaka Ubunge, kwenye Ubunge kuna nini? Nina orodha ndefu sana ya hao wakuu wa wilaya na mikoa ambao wanakimbilia kwenye Ubunge na wengine huwa wana kofia mbili kabisa, yaani Mkuu wa Mkoa na Mbunge. Mfano Bwana Lukuvi, Monica Mbega, Mohamed Abdulaziz na Dr. James Msekela (hawa wote ni wakuu wa miko) na mwaka huu walienda kuomba ridhaa ya kugombea. Orodha ya wakuu wa wilaya ni ndefu zaidi. Hivi jamani kwani mtu akiwa mkuu wa wilaya/mkoa siyo kwamba anatumia umma huo huo? Au mishahara na marupurupu ya Ubunge ni makubwa sana?