Shida iko wapi kwenye kujiajiri

Changamoto kubwa kwenye kujiajiri biashara 90% zina chukua muda kusimama na kufaidi matunda,ni chache sana ambazo ukianzisha leo faida unaanza kupata leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Lakini ukishasimama si ndio umeinuka maisha,unajua kinachowaponza wastaafu wakirudi mtaani licha ya kuwa na pesa wanafirisika na kufa mapema...coz wanakuwa hawajapata elimu dunia ya mtaani

by emma mjasiriamali
 
Ha ha ha ha. Stop kidding
[emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124]
Unaamini unaweza kupata mtaji kwa kuyauza mawazo yako....have u ever imagine watu walianza na wazo kwa kutokuwa na uoga wakatusua....

by emma mjasiriamali
 
Sijakuelewa hapo. Hebu funguka vizuri
Yaani wazo lako ndilo mtaji wenyewe,hela sio mafanikio....kwahiyo ukiwa na wazo sahihi ni mtaji tosha kabisa,kuna baadhi ya mawazo yanahitaji vitu vinavyokuzunguka....

by emma mjasiriamali
 
Reactions: SDG
Kwa mfano?
Hayo mawazo yanadepend na unazungukwa na nini...tatizo tunawaza mambo makubwa tu,hatuyapi nafasi mambo madogo ambayo kimsingi ndio chanzo cha hayo makubwa

by emma mjasiriamali
 
Shida mtonyo,yaani kianzio cha kujiajiri..
Pale ulipo...uwe kwenye group la masomo,mazoezi au lolote lile ndipo ulipo mtaji wako.
Mtaji mkubwa sio wazo pekee bali ni TAARIFA sahihi kuhusu kitu,jambo au biashara fulani.
Kumbuka kila kitu duniani ni biashara...Je ww unajua nini kwa undani ?
Hicho unachokijua kigeuze kiwe biashara na mtaji wa biashara hiyo ni huo ujuzi wako(Taarifa sahihi kuhusu unachokijua)
Mifano ni mingi kwa waliotumia wanachokijua kupata mitaji na kuifanya hiyo ndio biashara.
Mf.Dada mmoja aitwa Jamila ni mnene sana ...ktk kutaka kupungua akajiunga na group la WhatsApp linaitwa Loose weight. Pale akakutana na member wenzie wa mikoani (yy yuko Dsm)ilipokua wanazungumza biashara yy akawa anawaelekeza maeneo mazuri ya kupata bidhaa wanazozitaka hapa Dsm..na alikua anaelekeza mpka bei na ubora wa bidhaa husika..(kwamba ukitaka bei nafuu ni mtaa flani duka flan lkn quality kanunue duka flani.Ikaenda mpka akawa anawapokea baadhi ya wafanyabiashara na kuwapeleka madukani..ukizingatia hakua busy sana na shighuli zake.
Hivi ninavyoandika hapa account yke inasoma mzunguko wa mil 20 mpka 70 kila mwezi.
Anatumiwa pesa anawanunulia bidhaa na anawasafirishia mikoani na ameshafungua duka lake Tabata..kila mwezi hakosi mil 3 .

Huo ni mfano mmoja tu ambao umetokana na kua taarifa sahihi na kugeuza kua mtaji.

Inawezekana!

Kitu ambacho mm nakiona ni kwamba watu hawapotezi muda kujua chochote...Hii ni mbaya sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Juzi kati kuna Mkenya kaja Arusha na baada ya kufika akawa na wazo la kuuza Yogurt ila hana jinsi ya kuanza.

Ila jamaa kaka kafikiria kaja na njia ya kuuza Yogurt na katafuta vifungashio vya Yogurt na kavilebo kabisa.

Sasa ikabakia kupack ila hana yogurt anafanyaje?

Ikabidi ae nde awafuate makampuni yanayo zalisha Yogurt hapa Tanzania hasa Arusha.

Kwa sasa jamaa yuko mbali sana



Sent using Jamii Forums mobile app
 
sasa unategemea nini mtu anaajiriwa ili akufundishe ww kujiajiri ww unafikiria kwa akili za kawaida utatamani kujiajiri ili hali aliekufundisha kujiajiri kaajiriwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…