Shida iko wapi kwenye kujiajiri

Upo sahihi sana mkuu

by emma mjasiriamali
 
Mnayo jadili yote sijui mitaji au sijui wazo yote yamejengwa kwenye AIBU NA UOGA.

Ondoa Aibu ondoa na Uoga utaona kila kitu kinawezekana

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi elimu yangu sio kubwa sana...ila nilijijengea dhana ya kuajiriwa ni utumwa,nilitamani kuwa na kuwa bosi wa wengine...miaka mingi ya kujenga jina na kutafuta kukubalika kulikuwa na mateso sana...sikukata tamaa,sina mafanikio sana ila angalau hela ninayoweza kuikusanya kwa mwezi ni sawa na mshahara wa mtu aliyeajiriwa mshahara wa kati...tofauti yangu mimi na yeye ni kwamba mimi nafanya mambo mwenyewe ila yeye anapangiwa,na asset nilizonazo zinaweza kunipa uhakika wa mkopo wa sio chini ya milion 10 hadi 50...sijataka kuchukua mkopo mkubwa maana pia naogopa kuwa mtumwa tena...ila biashara ikiweza kujitegemea kabisa nitachukua,i am working hard on that....

by emma mjasiriamali
 
Umefungua duka, bar au grocery ?

- Ndo kazi zetu za kujiajiri hizo.
 
Shida mtonyo,yaani kianzio cha kujiajiri..
Halafu kingine tuache kufikiria mambo juujuu,unajua kila mwanadamu hapa ni unique....mimi ukiniambia unataka mtonyo kwa ajili ya mtaji,nitakuuliza mtaji tsh ngapi...ukinitajia najua hilo wazo la kucopy,nitainsist udevelop wazi lako....mtu ambaye hajaajiriwa na analalamika hana mtaji wa kujiajiri na anamiliki smartphone namuona kabisa hayupo serious....hata laki moja unaweza ukaanza kitu kikasogea kikakuza mtaji....tuache aibu na uwoga,life isnt easy kama na wewe unakuwa lege lege...umepanga foleni kuuuubwa ya kuomba kazi,kwa saivi nilivyo naona hata aibu kwakweli.

by emma mjasiriamali
 
Kujiajiri na kuacha kazi za kuajiliwa inabidi ujitoe ufahamu kwanza chief....la sivyo ndo wanabakia kusema jiajirini wakati wao wameajiliwa.
Hahahahahah, ofcourse kazi za mshahara zina security zaidi na nyingi hazilazimishi creativity kubwa. Ukishakuwa kwenye payroll na ukaelekezwa kazi inafanyika hivi we ni kutuma emails na kuandaa report ya kumpa boss, kuingia kwenye seminars ama vikao vya idara uliopo hapo umemaliza. Mwisho wa mwezi hela inaingia aidha fixed ama ikiwa na increment kila baada ya mwaka, so kama unakula mil. 1.5 hata kampuni ipige hasara we upo safe na pia sehemu ya mapato yako utahifadhiwa na social security kama makato. Drawback kubwa ya kuajiriwa unakuwa mtumwa wa kumsujudia boss na kuripoti ofisini saa mbili asubuhi kila siku.

Ukijiajiri hali ni tofauti utakuwa na uhuru binafsi isipokuwa, utahitaji mtaji wa pesa, utashi wako zaidi na creativity ya hali ya juu ili upige hela(ujasiriamali). So hapa kuingiza hela kunategemea juhudi zako na akili zako na pengine ukiwa mbunifu wa kuziona fursa ukazigeuza kuwa biashara zenye tija utapiga hela nyingi kwa muda mchache mno...Shida ni kwamba kwenye kujiajiri kuna swala la kuhustle wakati mwingine unapigwa na jua sana hamnaga kutegea na kubwa zaidi ni hasara ambayo ikitokea inakuathiri moja kwa moja na inaweza kukurudisha nyuma ukaanza moja. Uoga wa wengi kujiajiri ni hapa kwenye "Hasara" ndio maana watu wanalilia kuajiriwa sana, au wasitolewe kwenye ajira. Mazingira ya kibongo bongo sio favourable sana kujiajiri hasa masoko bado hayaja stabilize. Purchasing power imezidi kudidimia hivyo kujiajiri gemu imezidi kuwa ngumu sahivi.

Extrovert,
Ba-Marketing & Entreprenurship
 
Umefungua duka, bar au grocery ?

- Ndo kazi zetu za kujiajiri hizo.
Hilo ni wazo lako ambalo umeniongezea nimeadd to cart....later on nitafungua hiyo kitu kwa ajili ya washkaji wakija kunitembelea tuwe tunakaa sehemu yangu....

by emma mjasiriamali
 

Acheni kuigana igana kiss mmesikia ana smart4n. Wengine smart4n za kupewa sio kila mwenye simu kanunua.
Sio kila atakae kutajia wazo basi eti Ka copy, OK tell me what's me in the world?? Biashara za sasa kuna jipya gani zaidi ya kendeleza katika aina tofauti na zilizopo?
Huwezi mwambia mtu eti kacopy huwezi kumsaidia ulimuulizia ya Nini? Muulize,akuelezee strategies zake,plans and ending point anataka iweje,returning iweje akamilishe cycle yake ya kibiashara.

Sio kila mtu lazima atoe majibu kuhusu hili,wengine mnatoa boko.
 
Umepanic....na wala sijamlenga mtu,nimezungumzia in total.....kwakuwa tunajengana kila jambo tunalisikiliza...kama halikukugusi wewe Basi linamgusa mwingine...na niliposema mtu mwenye smartphone bila kujal amenunua au amenunuliwa nilimaanisha ni udhembe kulalamika maisha magumu na umeng'ang'ania vitu ambavyo unaweza kubadirishana na mtaji....that is it

by emma mjasiriamali
 
Hilo ni wazo lako ambalo umeniongezea nimeadd to cart....later on nitafungua hiyo kitu kwa ajili ya washkaji wakija kunitembelea tuwe tunakaa sehemu yangu....

by emma mjasiriamali
Kwa akili hizo ndo mnajiita wajasiriamali na waasisi wa UBER wajiiteje ?
 
Mnajua hili swala la kujiajiri sio rahisi kama tunavyofikiria na kuwaza,

Nimeona tunalalamikiana na kushangaana kwamba kwakuwa mtu anamiliki smartphone basi huyo hapaswi kusema hana mtaji...si sahihi,

Kwa ulimwengu wa sasa SMARTPHONE ni muhimu sana hasa kwa sisi wajasiriamali na hata wanaotaka kuwa wajasiriamali, najua wengi wanasema uza smartphone upate mtaji sasa smartphone nyingne watu wanamiliki akiuza hata laki.2 haifiki....huyo utamwambia afanye biashara ni biashara gani unaweza ukaiendesha kwa kiasi hicho ktk ulimwengu huu wa ss,

Zingatia kuna mambo mtu atahitaji kujifunza...kusoma vitabu, kusoma makala za wajasiriamali wengne mtandaon kama humu JF, na hata kujua dunia inaendaje ktk swala zima la uchumi,

Kwahyo kwenye swala la mtaji hapakwepeki kwakwer hili ni tatizo,
Mimi wakat nasoma nlikua nasema ntajiajiri ila lazima niajiliwe kwanza na nkajiwekea naziri kwamba sitakaa ktk ajira zaidi ya miaka 5,

Ndani ya miaka hiyo 5 ingetosha kabisa kunipa Starting Capital ya kujiajiri, so twende mbele turudi nyuma kuajiliwa mwanzoni kupo unless kama utapata kianzio either kwa wazazi au ndugu jamaa na marafiki.

Ni vema tukaelewana na kushauriana tuache kusemana na kusimangana vijana....tupo tofauti kiakili, kiumri na hata kimazingira,

Na kuhusu ishu ya kukopi mawazo ya biashara hilo ni kawaida...hakuna biashara mpya duniani zote zilikuwepo sema tu zinafanyiwa Modification/Innovation....ndio maana ya ujasiriamali,
 
Kwa akili hizo ndo mnajiita wajasiriamali na waasisi wa UBER wajiiteje ?
We bwana wewe...uelewa mdogo sana,unajifananisha na watu.Fanya mambo yako....kama unaamini kwenye kuajiriwa endelea huko mkuu

by emma mjasiriamali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…