Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Taarifa zaidi za operesheni ya kuokoa mateka 4 wa Israel zimezidi kutoka na kuonesha ilikuwa ni shughuli mbaya ya uokoaji iliyosababisha vifo vya watu 274. Wengi wao walikuwa ni wanawake na watoto na hata kama kulikuwa na Hamas kadhaa tukio hilo limelaaniwa na mataifa kadhaa na kuliona halikustahiki.
Mateka hao walikuwa wakiishi maisha ya kawaida na hawakuwa katika hatari yoyote ile ndio maana wamepatikana wakiwa katika afya nzuri.
Zaidi ya tukio hilo ni kuwa kulishawahi kupangwa operesheni kama hizo kadhaa huko nyuma na baadae zikafutwa kutokana na ugomo uliokuwa ukijitokeza katika hatua za mwisho za utekelezwaji.Hiyo ni kwa mujibu wa makamanda wa vita wa Israel.
Uokoaji huu ulifanywa kwa ushirikiano wa maafisa wa kimarekani na kwa kutumia gati la kutolea misaada.Askari wa Israel wajivika mavazi ya kipalestina na Hamas na yawezekana katika mavazi ya kike ili kufika eneo la tukio.
Mara baada ya kuonekana dalili za uokoaji huo wapiganaji wa Hamas badala ya kukimbia mbio walitoka na kila aina ya silaha walizonazo na kupambana.Ndege za jeshi zilitumika kupiga maeneo yote karibu na nyumba walizokuwa wakiishi mateka hao na hivyo kusababisha vifo vya wasiohusika.
Katika purukushani hiyo ambayo walionusurika wamesema ilikuwa ni operesheni ya hatari na iliyokosa umakini inaaminika pamoja na kuokolewa mateka basi na askari wa Israel hawakutoka salama wote na ushahidi ni gari yao waliyokuja nayo kutoweza kutoka na kuungua moto karibu na eneo la tukio.
israel haijataja maafa upande wao lakini imekiri kufariki kwa mateka mwengine aliyejeruhiwa vibaya katika opreresheni hiyo.Uokoaji huo ulihitimishwa na kuonekana kwa gari la kupeleka misaada ya chakula likielekea eneo la gati ba muda mfupi baadae helkopta kuruka kutoka eneo hilo kuelekea Israel.
Kwa kujua kwamba jeshi la Israel limelazimika kujivika mavazi ya kipalestina na mavazi ya kike na kujifanya Hamas sambamba na kutumia magari ya misaada,kwa sasa operesheni kama hizo zitakuwa ni ngumu zaidi kutekelezeka.
Ukipenda ongeza maarifa hapo chini.