The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,950
- 12,550
Hii imeandikwa na Mwananchi Online Newspaper leo..
Kwamba mji wa Dodoma makao makuu ya serikali ya nchi hii kuna shida ya maji kiasi cha wananchi kununua ndoo ya maji Tshs. 1,000?
Ni nini kinapaswa kuwa kipaumbele kuwekeza fedha kwa ajili ya maendeleo ya watu?
Je ni kujenga uwanja wa ndege kijijini kwa Rais Magufuli wa bilioni zaidi 70?
Je, ni kujenga uwanja wa michezo wa mabilioni kijijini kwa Rais Magufuli?
Hapo ni wananchi wakihangaika kusubiria maji kutwa nzima
Kama hapa ni Dodoma mjini, hali ikoje vijijini ndani huko Kongwa, Chamwino, Bahi nk?
Tukumbuke nchi yetu ina umri wa miaka 60 tangu kupata uhuru mwaka 1961.
Haiwezekani tabu ya maji iwe ni ishu kana kwamba nchi hii imepata Uhuru miaka 5 au 10 iliyopita. Nchi ina umri wa miaka 60 jamani..!
Haiwezekani nchi katika umri huu iwe bado imeshindwa kusambaza kwa watu wake huduma bora ya maji safi na salama ya kunywa nchi nzima.!!
Lipo tatizo mahali. Na tatizo hili ni mfumo mbovu wa utawala wa nchi chini ya CCM tangu uhuru mwaka 1961. Lazima tuliondoe tatizo hili!
===
Maji Dodoma dumu moja Sh1,000, mamlaka yafafanuaWakazi wa Jiji la Dodoma wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji kwa miezi miwili sasa.
Dodoma. Jiji la Dodoma limeendelea kukabiliwa na uhaba wa maji safi kwa muda mrefu sasa, dumu moja la lita 20 kwa sasa linauzwa Sh 1,000 kutoka Sh 50 ya awali.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa Jiji hilo wamesema hali hiyo inawafanya watumie muda mwingi kutafuta maji, wakati wana mabomba nyumbani.
Mkazi wa kata ya Nzuguni, Dotto Baliheza amesema dumu moja la maji la lita 20 walilokuwa wanachota kwa Sh 50, sasa wanalinunua kwa Sh 1,000 kutoka kwa watu wanaouza maji kwenye matolori.
Amesema dumu hilo hilo wananunua kwa Sh 500 kwa maji ya kisima vinavyomilikiwa na watu.
Kwa upande wake, Sekela Mwakalobo, mkazi wa Ndachi amesema ni muda mrefu sasa hawapati huduma ya maji, hivyo kulazimika kununua kwa watu wanaouza kwenye matolori bila kujua usalama wake.
Amesema awali walikuwa wanapata maji kila siku hata kwa saa 9, lakini hivi sasa wamekaa miezi miwili bila kupata huduma ya maji.
Advertisement
“Maji yote tuliyokuwa tumeyahifadhi kwenye matenki yameisha, tuna mabomba ambayo hivi sasa yamegeuka mapambo tu mpaka yameshika kutu maana hayatoi maji,” amesema Mwakalobo.
Naye mkazi wa Dodoma, Makulu Doris Matula amesema, “Naiomba Duwasa iangalie hili tatizo kwa jicho la tatu ili kuwaondolea wananchi hii adha kwa sababu huwezi kufanya kazi yoyote bila kuwa na maji ndani,” amesema Matula.
Akijibu malalamiko hayo, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Jijini Dodoma (Duwasa), Sebastian Warioba amesema shida ya maji kwenye kata ya Dodoma Makulu inatokana na kuhamishwa kwa bomba kubwa la maji ili kupisha ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR.
Amesema kazi ya kuhamisha bomba hilo likikamilika huduma ya maji itarejea kama kawaida, kwani mafundi wanafanya kazi usiku na mchana ili kuikamilisha.
Amesema pia kuna maeneo mengine yanayokabiliwa na shida ya maji imesababishwa na kuharibika kwa pampu za kusukumia maji.
Amesema ili kukabiliana na changamoto hiyo Duwasa imechimba visima kwenye maeneo ya Iyumbu na Zuzu ambako wamepata maji na kuna maeneo yatahudumiwa na nyongeza ya visima hivyo.
Chanzo: Mwananchi
Kwamba mji wa Dodoma makao makuu ya serikali ya nchi hii kuna shida ya maji kiasi cha wananchi kununua ndoo ya maji Tshs. 1,000?
Ni nini kinapaswa kuwa kipaumbele kuwekeza fedha kwa ajili ya maendeleo ya watu?
Je ni kujenga uwanja wa ndege kijijini kwa Rais Magufuli wa bilioni zaidi 70?
Je, ni kujenga uwanja wa michezo wa mabilioni kijijini kwa Rais Magufuli?
Hapo ni wananchi wakihangaika kusubiria maji kutwa nzima
Kama hapa ni Dodoma mjini, hali ikoje vijijini ndani huko Kongwa, Chamwino, Bahi nk?
Tukumbuke nchi yetu ina umri wa miaka 60 tangu kupata uhuru mwaka 1961.
Haiwezekani tabu ya maji iwe ni ishu kana kwamba nchi hii imepata Uhuru miaka 5 au 10 iliyopita. Nchi ina umri wa miaka 60 jamani..!
Haiwezekani nchi katika umri huu iwe bado imeshindwa kusambaza kwa watu wake huduma bora ya maji safi na salama ya kunywa nchi nzima.!!
Lipo tatizo mahali. Na tatizo hili ni mfumo mbovu wa utawala wa nchi chini ya CCM tangu uhuru mwaka 1961. Lazima tuliondoe tatizo hili!
===
Maji Dodoma dumu moja Sh1,000, mamlaka yafafanua