Shida ya Simba ni Mangungu kutumia busara zake badala ya Katiba ya Simba kuongoza timu.

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Mangungu inaivuruga Simba, anatumia busara kuongoza badala ya kuongoza kwa mujibu wa Katiba iliyopo. Tabia hii inampatia shida na lawama dhidi ya upande wa mwekezaji na chawa wake.

Mangungu anachelewesha ukamilishaji wa mchakato wa mabadiliko Simba, hafai.
 
Na upuuzi wake wa busara bila sheria wahun wanaenda kumng'oa, dunia hainaga fair!
 
Taasisi kubwa kama Simba huwezi kuiongoza kwa kutumia busara. Yeye anadhani anajenga kumbe ndio anabomoa. Wenzake wanamuona punguani, watamng'oa kweli na busara zake za hovyo.
 
Mangungu inaivuruga Simba, anatumia busara kuongoza badala ya kuongoza kwa mujibu wa Katiba iliyopo. Tabia hii inampatia shida na lawama dhidi ya upande wa mwekezaji na chawa wake.

Mangungu anachelewesha ukamilishaji wa mchakato wa mabadiliko Simba, hafai.
Hayo mabadiliko yanaivuruga vipi simba? Na yanasababisha vipi Mangungu kuwa kikwazo?
 
Katiba haitambui mwekezaji mmoja, inataja wawekezaji. Kuwa na nwekezaji mmoja ni kosa kwa mujibu wa Katiba ya simba. Katiba inampa nguvu kiongozi wa upande wa wanachama (51%), Mangungu, lakini Mangungu anaswagwa na Magori (49%). Kutekeleza haya ni sehemu muhimu ya kufikia mabadiliko ndani ya Simba.

Mangungu anatumia busara kumtambua mwekezaji mmoja na bodi yake. Mwekezaji na bodi yake haramu wanatumia nguvu ya fesha kumbonda na kumtweza Mangungu.

Mwekezaji ana mawazo kuwa Simba ni mali yake, ameinunua. Hivyo, anaeitaka Simba lazima ainunue kutoka kwake, ndiyo maana kila fedha anayotoa anasema anaikopesha Simba na kuutaka uongozi uidhinishe mkopo huo ilia baadae waulipe.
 
Back
Top Bottom