Pre GE2025 Shigongo amuomba Rais Trump wa Marekani asiifutie Misaada Tanzania kwani miradi mingi itakufa na Watu Wengi watapoteza Ajira!

Pre GE2025 Shigongo amuomba Rais Trump wa Marekani asiifutie Misaada Tanzania kwani miradi mingi itakufa na Watu Wengi watapoteza Ajira!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Eric Shigongo amemshauri Rais wa Marekani, Donald Trump kusitisha uamuzi wake wa kuzuia misaada kwa nchi za Afrika, kwa sababu akifanya hivyo Waafrika wengi watapoteza maisha.

Akiwa nchini Marekani kikazi, Shigongo amesema misaada ya Marekani kwa nchi za Kiafrika, inasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na changamoto mbalimbali zikiwemo za kiafya kwa nchi za Kiafrika ikiwemo Tanzania.

Soma Pia: Trump asimamisha misaada kwa nchi nyingine kwa siku 90 ili kupitiwa upya. Tanzania nayo kuathirika

Shigongo ni Mwandishi wa vitabu kama Yeriko Nyerere wa Chadema

Mlale Unono 😀

Shigongo jinga kabisa.

Mimi napinga sana hiyo misaada.

Nimeipinga tokea nianze kupata ufahamu.

Acha hiyo miradi ife na watu wapoteze ajira.

Misaada gani hiyo isiyo na kikomo?

Tokea tupate uhuru tumekuwa tukipewa misaada.

Ifike mahali hiyo misaada ikome kutolewa.

Marekani wao nani aliwapa misaada?
 
Kaka kajitafute baba kauza nyumba.
Aid debt Trap.
 
Mbunge wetu tunamtegemea atutoe kwenye umasikini Kwa kutumia Rasilimali tulizo nazo. Yeye amekazana kuomba misaada ya Condom na ARV

Bure kabisa.
 
Anawaza Ajira na sio zile huduma ambazo zinatolewa!?

Hii misaada ilikuwa haifiki Kwa walengwa au wahitaji husika .

Ikiwa itaandelea kuwepo USAID Ila wafikirie na kuona je misaada inawafikia wahitaji ? Ikiwezekana watoe materials things na sio PESA Kama pesa.
 
Mpina akina, Nchi ijitajidi kujitegemea iachane na mikopo.

Chawa wa mama waliokaribu naye wananiambia mama, tulo vizur, Piga kijembe
 
Mbunge wa Buchosa mh Shigongo amemuomba Rais Trump wa Marekani asitishe Nia yake ya kuzuia misaada Kwa Africa na Tanzania ikiwemo

Shigongo amesema miradi mingi inafadhiliwa na Marekani hivyo kuifuta misaada kutaliangamiza Taifa na Ajira nyingi zitapotea

Shigongo ni Mwandishi wa vitabu kama Yeriko Nyerere wa Chadema

Mlale Unono 😀
Ila ujinga mwingine bhana! Yaani watu wa Marekani walipe kodi wao hela mnalilia mpewe misaada waTz ni aibu. Ni sawa na mtu uwe na familia harafu huwezi kuilisha ilishwe na baba wa jirani🤔🤔🤔🤔
 
📌TURAMPU HUMO HUMO BABA,BADO HAWAJASEMA.

MIEZI MITATU KILIO HIVI MAAMUZI BAADA YA RIPORT YA UKAGUZI KUTOKA ITAKUWA NI MSIBA👋😀😀😀

HUYU NDO AINA YA WAWAKILISHI KUTOKA AFRICA ANALILIA MISAADA🤗

📌📌📌ELON MUSK NA NDUGUYE TRUMPET MMEFANYA VIZURI ONGEZENI SPEED!!!👏👏👏👏👏👏
 
Mbunge wa Buchosa mh Shigongo amemuomba Rais Trump wa Marekani asitishe Nia yake ya kuzuia misaada Kwa Africa na Tanzania ikiwemo

Shigongo amesema miradi mingi inafadhiliwa na Marekani hivyo kuifuta misaada kutaliangamiza Taifa na Ajira nyingi zitapotea

Shigongo ni Mwandishi wa vitabu kama Yeriko Nyerere wa Chadema

Mlale Unono 😀
That’s dependency syndrome! Tanzania itakuwa taifa ombaomba mpaka lini?
 
Back
Top Bottom