Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Hatua hiyo imekuja baada ya Mbunge wa Buchosa Eric Shigongo kukagua ujenzi wa nyumba ya Mkunga kwenye zahanati ya Kafunzo iliyopewa fedha hizo kwa jiali ya kumaliziajia nyumba na kukuta kazi iliyofanyika hainalingani na thamani ya fedha zilizotolewa kwa ajili ya ukamilishaji wa nyumba hiyo.
Huku shigongo akitoa saa 48 kwa watumishi wa Halmashauri ya Buchosa waliokula fedha za mfuko waziliejeshe mara moja akida fedha hizo siyo shamba la bibi bali zinachochoa maendeleo.
Mfuko wa Jimbo la Buchosa unatoa fedha nyingi kwa kila kata kwa ajili ya kuchochea miradi ya maendeleo kwenye kata hizo lakini zimekuwa hazifanyi kazi inayotakiwa na kuishia mikoni mwa watu.
Shigongo amesema baada ya kumalizika kwa vikao vya Bunge atarejea jimboni na kufanya ziara kila kata iliyopewa fedha za mfuko wa jimbo kwa ajili ya kuchochea maendelea na kusema kuwa akikuta fedha hizo zikiwa zimeliwa wahusika wote watazitapika.
"Serikali inatoa fedha nyingi kwa ajili ya kuchochea maendelea wanatokea watu wachache wanazichea fedha hizo mimi sitawavumilia nitawashughurikia," amesema Shigongo.