Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Ameeleza kuwa hali hii inahatarisha uchumi wa wazalendo na kuacha historia ya umiliki wa kiuchumi mikononi mwa wageni.
"Leo ninavyozungumza Mhe. Mwenyekiti, wazawa wako kando ya uchumi wao. Uchumi unaingia mikononi mwa wageni, hawafurahii jambo hili. Nimesimama hapa leo kuomba, tulitunga sheria ya manunuzi hapa ndani kwamba biashara yoyote ambayo ni ya bilioni 50 kushuka chini isifanywe na mgeni. Nimesimama hapa leo, bado biashara zinafanywa na wageni, wanasajili makampuni BRELA, wanajiita wao ni wenyeji lakini ni wageni."