Shikamoo biashara

Shikamoo biashara

Wakuu
Wale mliofanikiwa kuanzisha biashara zenu na zimedumu mpaka sasa SHIKAMOONI WAKUBWA. Hili game sio la kitoto for beginners.
Ndugu yangu; siku zote hakuna mwanzo rahisi hata siku moja, kila mwanzo una ugumu wake ila tu uvumilivu, ujasiri na namna bora y a kuzikabili changamoto ndiyo huweza kutofautisha mafanikio ya kibiashara kutoka kwa Mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

Inawezekana wewe umejaribu mambo yakaenda ndivyo sivyo, lakini amini kuwa Kuna watu humu wakikusimulia safari zao za kibiashara na yapi wamepitia mpaka kufika hapo walipo, utacheka mnoo! [emoji38].

Watu wanapitia misukosuko mingi sana kwenye Biashara, lakini hilo wala haliwakatishi tamaa. Wameamua kuvaa sura ya Simba, hakuna kurudi nyuma kamwe, mpaka Biashara zao zisimame.

Hivyo, kuanguka mara moja isiwe inshu kubwa Sana kwako; kikubwa ni kujifunza na kusonga mbele, MUNGU atasaidia na mambo yatajipa tu mbele ya safari.
 
Mwanzo hua ni mgumu,endelea kukomaa utatoboa tu,usikate tamaa.
Yeah..ukiweza kuvumilia mwanzoni ni hatua muhimu ya kuizoea biashara (sio kufanikiwa). Ukifika hii hatua unakuwa huogopi hasara, huogopi kupoteza wateja, huogopi competition n.k .mindset yako unakua free kiasi kwamba the fear of failure becomes not an issue any more.

Hapa unakua tayari kukabiliana na challenge yoyote huku akili yako iki focus katika ku grow zaidi, nifanye nini kupiga hatua.

Muhim sana hii stage
 
Unafungua biashara bila kuwaza kodi ya mwakani hutoboi n'goo
Biashara asilimia zaidi ya 60 huwa zinakufa miaka 2 ya kwanza FACT
Ukipasua hapo basi jipange zaidi
Lazima ujue matumizi ya hiyo biashara yako la sivyo utajikuta unakula zaidi ya unachoingiza
 
Yeah..ukiweza kuvumilia mwanzoni ni hatua muhimu ya kuizoea biashara (sio kufanikiwa).
Ukifika hii hatua unakua huogopi hasara, huogopi kupoteza wateja, huogop competition n.k .mindset yako unakua free kiasi kwamba the fear of failure becomes not an issue any more. Hapa unakua tayar kukabiliana na challenge yoyote huku akil yako iki focus katika ku grow zaid, nifanye nini kupiga hatua.
Muhim sana hii stage
Sahihi kabisa,
Tatizo hawa vijana wa siku hizi anataka jambo alianze leo kisha faida aipate leo leo.
 
Huwa nawashangaa watu ambao sio wafanyabiashara na wanalia eti maisha magumu. Zamani nilikuaga nashangaa ndg yangu mmoja ana duka kubwa sana ila ukimuomba hata buku anasema hana, nikadhani ana roho mbaya. Miaka hii najionea mwenyewe, hadi natamani nikamuombe msamaha
 
Unafungua biashara bila kuwaza kodi ya mwakani hutoboi n'goo
Biashara asilimia zaidi ya 60 huwa zinakufa miaka 2 ya kwanza FACT
Ukipasua hapo basi jipange zaidi
Lazima ujue matumizi ya hiyo biashara yako la sivyo utajikuta unakula zaidi ya unachoingiza
Tatizo alijipanga kwa faida zaidi akasahau kua biashara ina hasara pia hasa mwanzoni unapoianza.
 
Hiyo kawaida sana, ila ukitaka kufanikiwa vizuri achana na biashara zinazohusisha kodi, ingia kwenye biashara ya ufugaji hasa (beef feedlot) utakuja nishukuru baadae...

Angalizo biashara hiyo inahitaji kupata eneo zuri lenye malisho na maji ya uhakika mengine yanatatulika kwa gharama ndogo sana...
 
Back
Top Bottom