Shikamoo biashara

Shikamoo biashara

Biashara inahitaji watu wagumu na mabahili ,kuna mda inafika ata kula inabidi usile ili biashara iendelee

Hapo kama Umeajiriii watesiii na huna uzoefuuu subirii upukutishweeee...[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Yani biashara kama huna muda binafsi wa kuifatilia kwa karibu na huna experience nayo mwaka wa kwanza ni wa kujifunza kubali hasaraa
Raha ya biashara uijue kiundani wekeza muda wako mwingi pale ...datss waajiriwa wengi walio na biashara wanafail hapo wanatamani yale maokoto yanayopatikana bila kujua kuwa waliowaajiri wanafaidi sana nguvu zao bila wao kujua maana wanambinu zote za kuiba na aasikamatwe na mabosi zao..unakuta boss hajui chochote katika biashara yake anafungua hardware hajui kifaa hata kimoja ..anafungua saloon hajui kusuka..anafungua stationery hajui matumizi ya photocopy mashine wala computer.. msaidizi asipokuwepo shughuli zote zinasimama maana boss hana analololijua na hajawekeza muda wake katika biashara utaletewa hesabu za hovyo unajikuta mtaji umepukutika ..kwa hapo lazima upigwe na ulizwe
 
Mda,wasimamizi,kukosa uzoefu,washauri,umbali,timing,buy cheap ni baadhi TU ya factor zilizonikwamisha
Alafu kingine boss usipokuwa makini unajikuta huendani na bei za sokoni..eidha unauza bei chini zaidi au ya juu zaidi wateja wakakimbia msaidizi hana muda huo kufatilia anachojar ni maokoto...biashara ni kama mtoto inahitaji ukaribu ..uipende na uitumikie kwa kuwekza muda wako utajua muelekeo wake nn uboreshe zaidi ili kuhakikisha biashara inasimama na kukua,bado unayo nafasi simama jipange upya fanyia marekebisho hizo changamoto utatoboa
 
Kudumu kwa biashara inategemea na factors nyingi Location, demand, mtaji, msimamizi, sera za kiuchumi n.k

Mfano mwaka 2014 nilianzisha biashara ile biashara ilianza vizuri sana na akachanganya sana, ilifanya vizuri kwa sababu ya mazingira biashara ilipokuwepo kulikuwa hakuna access ya barabara pana ya kupita malori, barabara pana ilikuwa inaishia kwangu kwahiyo wateja walikuwa wanatoka maeneo mbalimbali kuja kununua bidhaa kwangu kwa jumla halafu wanasomba na mikokoteni kuingia huko ndani ndani.

Mwaka 2017 ukaja mradi wa kukarabati barabara za mitaani, watu wakalipwa na barabara zikapanuliwa kwa kiwango cha lami.

Nikapoteza wateja wa jumla wote, biashara yangu mauzo yakadrop ile mbaya mwisho ikafa.

Biashara ya pili ilikuwa ya duka baada ya barabara kukarabatiwa zilijengwa frame nyingi sana, yakafunguliwa maduka mengi biashara zinazofanana, bidhaa nyingi wateja wachache. Duka likaangukia pua.

Kwahiyo kudumu kwa biashara muda mrefu kuna sababu nyingi sana. Ila nilichojifunza jitahidi kuwa mfanyabiashara wa kati wa Jumla/mtaji mkubwa na sio mfanyabiashara wa mwisho.
Tuambie ni kwa namna gani uliweza kusimama tena mkuu... ili na sisi tujifunze
 
Ndugu pale matumizi ya kawaida ya familia yanapokuwa makubwa kuliko faida ni stress kubwa, huoni pakutokea tena kwenye biashara, halafu unatakiwa ulipe kodi za watu hujui unaipatia wapi, madeni ya mikopo kila siku hodiii dukani, huna backup, only option ilikuwa kujiondoa.

Nikatangaza kuuza biashara watu wengi wakajitokeza kuinunua kwa historia yake, nikaiuza bei nzuri sana.

Niliyemuuzia naye ameshaifunga [emoji3] sidhubutu hata kumsalimia ananiulaumu balaa.
Duuh.. Unanitisha mkuu😃😃
 
Back
Top Bottom