Shikamoo biashara

Shikamoo biashara

Fafanua mkuu, haswa hapo kwenye Bold
Kidogo niko bize sana currently muda wa kuandika kwa mapana sipati.

Ila chukulia mfano unaanza biashara ya usafirishaji wa mizigo kwa kutumia Fuso, target yako unakuta ni kuanza na Fuso 3. Ili biashara yako isiyumbe inatakiwa ununue Fuso walau 5 au 6 ili ikitokea mbili zimekula mweleka unakuwa na zingine kama Back Up and the like.
 
Kudumu kwa biashara inategemea na factors nyingi Location, demand, mtaji, msimamizi, sera za kiuchumi n.k

Mfano mwaka 2014 nilianzisha biashara ile biashara ilianza vizuri sana na akachanganya sana, ilifanya vizuri kwa sababu ya mazingira biashara ilipokuwepo kulikuwa hakuna access ya barabara pana ya kupita malori, barabara pana ilikuwa inaishia kwangu kwahiyo wateja walikuwa wanatoka maeneo mbalimbali kuja kununua bidhaa kwangu kwa jumla halafu wanasomba na mikokoteni kuingia huko ndani ndani.

Mwaka 2018 ukaja mradi wa kukarabati barabara za mitaani, watu wakalipwa na barabara zikapanuliwa kwa kiwango cha lami.

Nikapoteza wateja wa jumla wote, biashara yangu mauzo yakadrop ile mbaya mwisho ikafa.

Biashara ya pili ilikuwa ya duka baada ya barabara kukarabatiwa zilijengwa frame nyingi sana, yakafunguliwa maduka mengi biashara zinazofanana, bidhaa nyingi wateja wachache. Duka likaangukia pua.

Kwahiyo kudumu kwa biashara muda mrefu kuna sababu nyingi sana. Ila nilichojifunza jitahidi kuwa mfanyabiashara wa kati wa Jumla/mtaji mkubwa na sio mfanyabiashara wa mwisho.

Jitahidi kuwa mfanyabiashara wa kati/jumla[emoji1417]
 
Sasa hawa wadada wa mitandaoni mbona wanatoboa sana na wanafanya biashara ionekane rahisi? Ma range wanayanunua kama baiskeli, mijumba wanajenga ya ukweli sana. Kila siku kushusha ma container, Kuna siri ambayo wanayo na sisi hatuijui? Mimi pia na struggle sana kusimama kwenye biashara but wenzetu wanapasua tu😳😳 anaeijua siri tupeane plz
 
Ndugu pale matumizi ya kawaida ya familia yanapokuwa makubwa kuliko faida ni stress kubwa, huoni pakutokea tena kwenye biashara, halafu unatakiwa ulipe kodi za watu hujui unaipatia wapi, madeni ya mikopo kila siku hodiii dukani, huna backup, only option ilikuwa kujiondoa.

Nikatangaza kuuza biashara watu wengi wakajitokeza kuinunua kwa historia yake, nikaiuza bei nzuri sana.

Niliyemuuzia naye ameshaifunga [emoji3] sidhubutu hata kumsalimia ananiulaumu balaa.
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Ilikuwa biashara gani Mkuu.
 
Sasa hawa wadada wa mitandaoni mbona wanatoboa sana na wanafanya biashara ionekane rahisi? Ma range wanayanunua kama baiskeli, mijumba wanajenga ya ukweli sana. Kila siku kushusha ma container, Kuna siri ambayo wanayo na sisi hatuijui? Mimi pia na struggle sana kusimama kwenye biashara but wenzetu wanapasua tu[emoji15][emoji15] anaeijua siri tupeane plz
Na sasa hivi naona wamejaa Instagram, china pa kugusa, Dubai kila mara.

Wamewezaje? [emoji2957]
 
Mkuu, nilijipiga 2023 kufika Nov nina Mil 3 ya mzigo nikatafuta na hela ya fremu nikalipa 3/6 miezi, nikampa fundi fenicha nusu aniandalie fremu, watu wa decorations na mabango, etc.. nikaingia mzigoni.. aisee..
1..Don't put all your eggs into one bucket....kwasababu kapu likidondoka unevunja mayai yote....kwenye biashara usiokuwa na uzoefu nayo huwa tunaanza kwa kutest mitambo kwanza.

2...ukiona hapaeleweki unatafuta plan nyengine,utakuwa umepoteza nusu na nusu nyengine umesave
 
Binti ukiona anafanya biashara sio wa kushindana naye! Kwanza kodi ya pango ni chupi! Mtaji ni chupi! Hawanaga mahesabu zaidi ya kukuelekeza kwenye 'V' ya mapaja yake ukitaka kudai kodi! Wanaofanya biashara za piga/ua/komaa ni wanaume!
Uko sahih kbsaa
 
Majuzi nilimtembelea rafiki yangu mmoja, amenunua mashine ya kudarizi 30m, nilimkuta anaweka nembo kwenye mashati 30, lakini malipo aliyopata ni shilingi 60,000/=; kwa mazingira hayo kama huna nidhamu ya pesa, unaweza kuhisi hiyo milioni 30 aliyowekeza kwenye mashine imepotea.
Hii itakuwa ile mega.

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Sasa hawa wadada wa mitandaoni mbona wanatoboa sana na wanafanya biashara ionekane rahisi? Ma range wanayanunua kama baiskeli, mijumba wanajenga ya ukweli sana. Kila siku kushusha ma container, Kuna siri ambayo wanayo na sisi hatuijui? Mimi pia na struggle sana kusimama kwenye biashara but wenzetu wanapasua tu😳😳 anaeijua siri tupeane plz
Mkuu maisha na biashara huwa sio za kuzishii Kupitia tunavyoona mitandaoni!! Ukija kwenye uhalisia vitu ni tofauti kabisaa na hayo unayoyaona kwenye social network!! Ya Kule tazama halafu kapambane kulingina na uhalisia ya mazingira uliyopo wala wala yasikuchanganye uhisi umechelewa kwenye maisha.
 
Back
Top Bottom