Shikamoo kaka Juma Nyoso

Shikamoo kaka Juma Nyoso

Mwabhleja

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2016
Posts
1,351
Reaction score
2,061
Wahenga wanasema mtu husifiwa kwa kile akitendacho siyo ajuacho. Katika mtanange wa leo kati ya Simba Vs Kagera Sugar Mzee Mwenye Lindo Juma Nyoso ameonyesha kiwango cha juu sana.

Ilikuwa kama kuna ligi ndogo kati ya John Raphael Bocco na Juma Nyoso.

Hakika huyu mwamba leo amenikosha sana ukiacha kwamba aliwahi kucheza Simba amekuwa msaada mkubwa kwa Kagera na ameokoa hatari nyingi.

Awali niliwahi kupata taarifa kwamba mshikaji amepotea kwenye game halafu anakula ndumu vibaya lakini kwa leo moyo wangu umefurahi kuona jembe langu unakipiga vizuri na afya iko poa.

YANGA WANGEKUWA NA WACHEZAJI SITA wenye spirit kama yako, Msimbazi tusingepumua.

Keep it up Nyoso!

Juma Nyoso.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati mwingine kabla ya Kumsifia Nyoso mtambue Kwamba Bangi ni zao lenye umuhimu hatuna budi kuhalalisha mmea huo utumike kwa tiba na afya njema.
Waione wahenga kwenye Soka; Boban, Tegete, Yondani, Kado, Nyoso, Mkude, Wawa, Chujji, Mlipili na Wagumu wooote kwenye VPL.
 
Ukweli mchungu ni kuwa Nyoso na Kaseja ni wachezaji waliondoka Simba bado wakiwa na uwezo mkubwa. Sijui hata tatizo lilikuwa ni nini wakatupiwa virago wakati bado walikuwa na uwezo. Ila huyu mwamba Nyoso namkubali sana uwezo wake uwanjani anakaba kwa akili sana, panapohitajika nguvu anatumia na hata mpira wa kihuni/ kibabe pia anaweza sana tu. Pamoja na kufungiwa miaka 2 lakini mwamba bado yupo vizuri sana kuwazidi hata mabeki wa kigeni waliosajiliwa na hizi timu zetu pendwa kwa mkwanja mrefu.
 
Kwa iyo mnapendekeza arudishwe msimbazi! [emoji848]?
 
Kwa iyo mnapendekeza arudishwe msimbazi!
Iwapo tu kiwango chake kitakuwa kama cha jana au zaidi kwa msimu mzima na iwapo atajirekebisha nidhamu yake ndani na nje ya uwanja Simba wafikirie kumrudisha huyu mwamba. Uwezo wa Tairone Santos na Kennedy Juma wanasubiri sana kwa huyo Nyoso. Na haitakuwa ajabu kwake kurudi kama viongozi wataona anafaa kurudi kwani kwa siku za karibuni wamerudi Miraji "Sheva" na Shamte. Yote kwa yote viongozi ndio wanaojua mahitaji ya timu na ndio wenye dhamana ya timu na maamuzi ya mwisho nani asajiliwe nani asisajiliwe sisi wengine ni kutoa maoni yetu tu na kusubiri kuona burudani uwanjani
 
Back
Top Bottom