Shikamoo ni salamu ya ovyo

Shikamoo ni salamu ya ovyo

Salamu ya kutakiana amani ambay haibagui umri unaeza mtolea mtu yyt awe mkubw wako au hata mdg wako mmeikataa. Pambaneni
Salamu ipi hiyo tuliyoikataa ?
 
Kuna nchi nilikuwa sasa jamaa wa huko ana hamu kinoma ya kujua kiswahili sasa akakariri kwamba shkamoo ni salamu kwa yeyote. Yule jamaa mkubwa kuliko mimi ila akiniona tu anakimbilia kusema SHKAMOO... Nikawa nakwepa kupita hata maeneo anayokaa.
Hata wakongo baadhi hudhani hivyo pia
 
Dah hii kitu ilishawahi nitokea kipindi nahudumu pale serena hoteli nilikua mlangoni nakaribisha wageni wa aina tofauti tofauti kiumri, jinsia na mataifa hivyo alikuja mzee wa makamo na gari moja kali sana kwa rafudhi yake tu nikajua huyu ni mTZ

Hivyo nikaanza kwa kumsalimu "habari boss shikamoo, karibu sana boss" Dah basi yule mzee alinijia juu anadai mimi ni sawa na mwanawe wa mwisho halafu namsalimu habari yaani mzee alinifokea mno muda wote huo mzee anafoka mimi nilishikwa na mshangao nisijue nianzie wapi kujitetea

Ukweli ni kwamba nilimsalimu habari kisha nikatanguliza na shikamoo ila yule mzee ile shikamoo hakuisikia
Watz hii salamu unaweza kudhani labda ina waleteaga chakula mezani wanaipenda mno
 
Tangu nimerudi nchini nimekuwa nikipata tabu sana kutambua yupi anastahili shikamoo na yupi hastahili, kuna nalingana nao umri ila wana maumbo makubwa hivyo najikuta nikiwapa shikamoo na hawaitikii.

Kuna watu ni wakubwa ila wanaonekana ni wadogo ki-umbo hivyo nimekuwa nawa-skip na huniona sina adabu, najiona nimekuwa.

Yaani kwa kifupi nimechoshwa na hii salamu,, ni salamu ya hovyo mnoo, nimechoshwa kila ninapokutana na mtu nianze kufikiria salamu ya kumpa.

Mbona wenzetu mfano Uganda salamu ni hiyo hiyo mdogo ana msalimia mkubwa na mkubwa ana msalimia mdogo..

Anyway, nguvu moja [emoji881]
Ujumbe wako uliotaka kuwasilisha kwa njia ya mzunguko bila shaka umefika, yaani ulikuwa nje ya nchi!! Sidhani kama ni sifa kuwa nje ya nchi!!
 
Kwakuwa nchi ya shangazi yako hii sio ?
 
Ishiiiiiy watembee na kadi za clinic.

Swali la kizushi: juzi tulikuwa na mashoga zangu umbea wa hapa na pale likazuka swali!

Let say mdada ana 30yrs ana date mbaba wa 55 yrs. Kabla ya kudate heshima kibao kama anapokea ekaristi.

sasa ndo ku date haswa hivi kikatiba isiyo rasmi huyu mwanaume shikamoo yafaa kuendelea kumzeesha tena?

Wanaume mkuje mjibu haraka mnatuchanganya. Sasa mtu umelala nae the same bed at asubuhi "shikamo" hii imekaaje?

Mko wapi wanaume nawasubiri hapa!!!
Shikamoo inabidi iendelee..alafu ina raha yake kama inatoka kwa babe,kuna katoto niliwahi kuwa nako yan kananiamkia ile shikamoo inatoka ndani kabisa,basi nikawa najiona dume mimi [emoji3]
 
Upo sahihi. Ni salamu ya kitumwa huwa siitumii. Haina maana yoyote katika kumjulia mtu hali.
Na ndio maana ya salamu ilenge katika kumjulia mtu hali, mpaka leo sijui shikamoo inalenga nini
 
Back
Top Bottom